2024.11.14 Wawakilishi wa Waisraeli waliotekwa nyara na Hamas huko Gaza ambao waliajiliwa huru. 2024.11.14 Wawakilishi wa Waisraeli waliotekwa nyara na Hamas huko Gaza ambao waliajiliwa huru.  (Vatican Media)

Papa alikutana na kundi la Waisrael waliotekwa nyara na kuachiliwa huru huko Gaza

Wanaume na wanawake waliotekwa na Hamas kwa miezi kadhaa baada ya shambulio la tarehe 7 Oktoba 2023 walipokelewa na Baba Mtakatifu Mjini Vatican tarehe 14 Novemba 2024.Watoto wawili pia walikuwepo.Wengi walileta ishara yenye nyuso na majina ya wanafamilia waliokuwa wamefungwa au kutoweka.

Vatican News

Baada ya miezi kadhaa ya utumwa huko Gaza, kundi la mateka wa Israel waliotekwa nyara na Hamas wakati wa shambulio la kikatili la tarehe 7  Oktoba 2023, walipokelewa mnamo tarehe 14 Novemba 2024 na Baba Mtakatifu  Francisko mjini  Vatican. Waliohudhuria katika kikao hicho, katika Ukumbi wa Maktaba ya Jumba la Mitume, walikuwa watu kumi na sita, wakiwemo wanawake kumi, wanaume wanne na watoto wawili. Mmoja wao alimpatia Papa jezi ya mpira wa miguu lililokuwa na jina la Tal Shoham, jamaa aliyetekwa nyara pamoja na mkewe, watoto, mama mkwe na jamaa wengine, ambao baadhi yao waliachiliwa kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda kati ya Hamas na Israel, iliyopatanishwa na Qatar, Misri na Marekani.

Manusura wa utekwaji nyara huko Gaza
Manusura wa utekwaji nyara huko Gaza

 

Uso wa kijana huyo, pamoja na umri wake (miaka 38 wakati wa utekaji nyara, umri wa miaka 39 akiwa kifungoni) ulioneshwa kwenye bango ambalo baadhi ya waliokuwepo walimletea Papa Francisko mabango yenye nyuso za wanafamilia wao, na majina, umri, maandishi Bring him home, "Mlete nyumbani", wito yaani  kuwaruhusu kurudi nyumbani, na nembo ya “Mateka na Familia Zilizopotea", uratibu wa jamaa za mateka na watu waliopotea kwa zaidi ya mwaka mmoja. Papa Francisko aliweka mkono wake juu ya kila moja ya nyuso hizi kama ishara ya baraka. Kisha alitaka kukaa kimya katika maombi kwa muda mchache.

Mkutano wa kugusa

Ubalozi wa Israel unaowakilisha nchi yake mjini Vatican  ulifafanua kuwa ni mkutano wa "kugusa" katika chapisho lililotolewa na akaunti yake ya X, ambayo inasomeka kuwa Papa alionesha ukaribu wake na kujitolea kwa kuachiliwa kwa mateka wengine ambao bado wako utumwani huko Gaza.

Maombi ya mara kwa mara ya Papa

Tangu mwanzo, Papa Francisko amekuwa akisisitiza katika kila tangazo la umma ombi la kuachiliwa kwa watu waliotekwa nyara, kama hali ya dharura na ya lazima - pamoja na usitishaji wa mapigano katika Ukanda huo na ufikiaji wa idadi ya watu kwa misaada ya kibinadamu - kwa suluhisho la mzozo uliotokea baada ya shambulio la Oktoba 7. Shambulio lililosababisha vifo vya zaidi ya 1,100 na kupelekea watu 240 kutekwa nyara, wakiwemo wanawake, wazee na watoto.

15 November 2024, 11:52