Papa amtembelea Emma Bonino nyumbani,aliyetoka hospitali hivi karibuni
Vatican News
Akiwa njiani kurudi nyumbani Mtakatifu Marta mjini Vatican, huku akitokea Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, ambapo Jumanne tarehe 5 Novemba 2024, alikutana na Jumuiya ya wasomi, katika fursa ya ufunguzi wa mwaka wa masomo, Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika gari jeupe la Fiat 500L, ilionekana likipinda kuelekea barabara ya katikati ya Roma. Na huko alikwenda na kumtembelea aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia na kiongozi wa Kisiasa wa chama cha (+ Europa), yaani "Ulaya Zaidi " ambaye alilazwa hospitalini katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu kwa matatizo ya kupumua na kisha kuhamishiwa katika kituo cha kibinafsi. Alikuwa amerejea nyumbani hivi karibuni.
Katika taarifa zilizochapishwa katika ukurasa wa kiongozi huyo wa zamani, amebainisha kwamba amepokea kutoka kwa Baba Mtakatifu zawadi na salamu za mtu wa Piemonte: "Kutoka kwake nguvu na uelewa." Bi Emma Bonino, mwanaharakati anayejulikana sana ambaye sasa ndiye kiongozi wa chama cha kisiasa kiitwacho + Europa, mwenye umri wa miaka 76, ambaye kwa hiyo aliruhusiwa kutoka katika kituo cha afya mwishoni mwa Oktoba alikokuwa amelazwa. Hii ni kufuatia matatizo ya kupumua, ambapo Bi Bonino alilazimika kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha Hospitali ya Roho Mtakatifu jijini Roma tarehe 17 Oktoba 2024; Juma moja baadaye alihamishiwa kwenye kituo cha kibinafsi katika mji mkuu Roma na katika siku za hivi karibuni alirudi nyumbani. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu alipendelea kumtembelea. Matembezi ya ghafla. Mwishoni mwa matembezi hayo Papa Francisko alipotoka nje ya mlango wa nyumba hiyo, alifikiwa na baadhi ya watu waliokuwa wadadisi na kumuuliza ni katika hali gani amemkuta Bonino ambaye alikuwa amepona uvimbe wa siku za nyuma. Papa alijibu "Vizuri sana, Yeye daima ni rafiki siku zote."