2024.11.29 Papa akutana na uwakilishi wa Kitengo cha Meno cha Mafunzo katika Chuo Kikuu cha Napoli, Italia. 2024.11.29 Papa akutana na uwakilishi wa Kitengo cha Meno cha Mafunzo katika Chuo Kikuu cha Napoli, Italia.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:madawa hayapaswi kupuuza utu wa binadamu kwa maslahi ya soko!

Hekima ya kiutamaduni inakutana leo hii na teknolojia inayokua kwa kasi ambayo haipaswi kamwe kuendelea bila maadili.Vinginevyo,utu wa binadamu,ambao ni sawa kwa kila mtu,ungepuuzwa!dawa inahatarisha kujikopesha kwa maslahi ya soko na itikadi,badala ya kujitolea kwa manufaa ya maisha machanga,maisha ya mateso na maisha duni.Ni katika Hotuba ya Papa Francisko kwa ujumbe kutoka Idara ya Mafunzo ya Meno ya Chuo Kikuu cha ‘Federico I,Napoli Italia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amekutana na ujumbe kutoka  Idara ya Mafunzo ya Meno ya Chuo Kikuu cha ‘Federico II’ cha  Napoli nchini Italia Ijumaa tarehe 29 Novemba 2024 mjini Vatican. Katika Hotuba yake alianza na salamu kwamba  katika hafla ya kumbukumbu ya miaka ambayo inawaheshimisha hasa kwa sababu hiyo, inahusisha uwajibikaji wao kwa  miaka mia nane imepita tangu kuanzishwa kwa Msingi wa Chuo Kikuu cha Napoli. Taasisi hii bado ina jina la Frederick II, mfalme wa Swabian ambaye alijenga studio ya kwanza ya jumla katika jiji la Napoli, na hivyo kusababisha moja ya vyuo vikuu vya zamani zaidi duniani. Na Wanapoli ni wema. Papa amewasifia. Maadhimisho ya miaka wanayosherehekea yanawaalika madaktari, hasa, kukumbuka mila ya kitabibu ambayo wao ni warithi.  Na imefupishwa vyema katika kauli mbiu inayounganisha Funzo la  Hippocrates la Kigiriki na mamlaka ya Scribonius ya Kilatini: primum non nocere, secundum cavere, tertium sanare, yaani kwanza usidhuru, pili kuwa makini au tahadhari, tatu kuponya.  Kwa njia hiyo Papa amependa kusema hii ni nzuri ambayo awali usidhuru, kisha  ya kuwa na tahadhari  na baadaye kuponya. Ni Programu nzuri ambayo ni ya sasa kila wakati!

Usidhuru: ukumbusho huu unaweza kuonekana kuwa wa kupita kiasi, lakini badala yake unatii uhalisia wa afya: kwanza kabisa ni juu ya kutoongeza uharibifu na mateso kwa yale ambayo mgonjwa tayari anapitia. Kwa hisia ya kutofanya madhara.  Kujihadhari: hii ni hatua ya kiinjili  kuweka ubora kama ule wa Msamamria mwema; lakini ni lazima ifanywe kwa ‘mtindo wa Mungu’. Je Mtindo wa Mungu ni upi? Ukaribu, huruma na upole. Papa amekazia kwamba wasaisahahu hili kuwa Mungu yu karibu, mwenye huruma na mpole. Mtindo wa Mungu daima ndiyo huo wa  ukaribu, huruma na upole.” Zaidi ya hayo, mtu huyo anayetibiwa kwa ujumla wake, si sehemu tu. Kwa kufafanua zaidi Papa ameeleza kisa kimoja ambacho anakikumbuka daima akifikiria kuhusu Hospitali kwamba alipokuwa na umri wa miaka 20 alifanyiwa operesheni na kuota sehemu ya pafu lililokuwa haribifu na hivyo  nguvu zaidi ilikuwa ni mkono mwa wauguzi ambao, baada ya kumdunga sindano walikuwa wakimshika mkono... Kwa hiyo upole huu wa kibinadamu hufanya vizuri sana, kwa wagonjwa wanaupokea. Papa ameeleza la tatu kuhusu kuponya kwamba katika hili wanaweza kufanana na Yesu, aliyeponya kila aina ya magonjwa na udhaifu kati ya watu. Wawe na furaha kwa mema yaliyofanywa kwa wale wanaoteseka (Katekisimu ya Kanisa Katoliki, n. 1421).

Papa Francisko amesisitiza kwamba, hekima ya kiutamaduni inakutana leo hii  na teknolojia inayokua kwa kasi, ambayo haipaswi kamwe kuendelea bila maadili. Vinginevyo, utu wa binadamu, ambao ni sawa kwa kila mtu, ungepuuzwa!, dawa inahatarisha kujikopesha kwa maslahi ya soko na itikadi, badala ya kujitolea kwa manufaa ya maisha machanga, maisha ya mateso, na maisha duni. Daktari yupo kuponya uovu: kuponya daima! Hakuna maisha yanapaswa kutupwa. "Jihadharini kila wakati! “Lakini hiyo itafanikiwa kwa kuwasindikiza hadi mwisho.” Papa amewasihi kukuza sayansi ambayo daima iko  katika huduma ya mtu. Na amewashukuru kwa umahiri wao na kushukuru kwa uthabiti wa kazi wao: baada ya miaka mia nane, waendele kufundisha! Amewabariki kutoka ndani ya moyo wake na kuwaomba wasisahau kumuombea.

Papa na madaktari wa Napoli
29 November 2024, 16:11