Tafuta

2024.11.17 Kitabu cha Papa " Matumaini hayakatishi tamaa kamwe" 2024.11.17 Kitabu cha Papa " Matumaini hayakatishi tamaa kamwe" 

Matumaini hayakatishi tamaa:ni kitabu cha matazamio ya mwaka mtakatifu 2025

Katika kitabu cha Jubilei ya 2025,Papa anazungumzia masuala ya sasa,ikiwa ni pamoja na mateso ya kuongezeka kwa vita na njaa huko Palestina.Anasisitiza umuhimu wa kuheshimu utu wa binadamu.Kitabu kinatoka Jumanne 19 Novemba Italia,Hispania na Amerika Kusini na nchi zingine zitafutia."Tumeitwa kuiga maisha ya usawa na endelevu yanayoipatia Dunia mapumziko inavyostahili,pamoja na riziki za kutosha kwa wote ambao hawaharibu mifumo ikolojia inayotuunga mkono.

Vatican news

Kitabu kipya cha Papa Francisko kwa ajili ya Jubilei ya 2025 kinaakisi mada, "Matumaini hayakati tamaa kamwe. Mahujaji kuelekea ulimwengu bora" na kitachapishwa na Hernán Reyes Alcaide, wachapishaji wa nyumba ya vitabu ya Piemme. Kitabu hicho kitotolewa Jumanne tarehe  19 Novemba 2024 nchini Italia, Hispania na Amerika Kusini, na baadaye hata katika  nchi nyingine. Katika moja ya kifungu Papa anataja juu ya mzozo wa kibinadamu huko Gaza akisema kwamba kilichotokea ni lazima kichunguzwe. Akizungumzia mataifa yanayopokea wakimbizi wa kivita, alisema "Katika Mashariki ya Kati, ambapo milango wazi ya mataifa kama Yordan au Lebanon inaendelea kuwa wokovu kwa mamilioni ya watu wanaokimbia migogoro katika eneo hilo. “ Ninafikiria zaidi ya wale wote wanaoondoka Gaza katikati ya njaa ambayo imewakumba kaka na dada zao Wapalestina kutokana na ugumu wa kupata chakula na misaada katika eneo lao." "Kwa mujibu wa baadhi ya wataalam," Papa Francisko anaandika, "kinachotokea Gaza kina sifa ya mauaji ya halaiki. Kinapaswa kuchunguzwa kwa makini ili kubaini iwapo kinalingana na ufafanuzi wa kiufundi uliotungwa na wanasheria na mashirika ya kimataifa."

Hata hivyo Papa Francisko kuhusiana na Jubilei 2025 anaandika kuwa “Tumaini daima huwa na sura ya kibinadamu. Hii itakuwa Jubilei ya kwanza itakayoadhimishwa na ujio wa teknolojia mpya na itafanyika katikati ya dharura ya hali ya tabianch kama hii tunayopitia. Kila siku tunaona jinsi nyumba yetu ya  kawaida  ya pamoja inavyotuomba tuseme vya kutosha kwa mtindo wetu wa maisha ambayo yanalazimisha sayari kupita mipaka yake na kusababisha mmomonyoko wa udongo, kutoweka kwa mashamba, upanuzi wa majangwa, asidi ya bahari na kuongezeka kwa dhoruba na mengine mengi ya  matukio makali ya tabianchi. Ni kilio cha Dunia kinachotupatia changamoto. Katika Maandiko, wakati wa Jubilei, watu wa Mungu walialikwa kupumzika kutoka katika kazi yao ya kawaida, ili kuruhusu Dunia itengeneze na ulimwengu ujipange upya, kutokana na kupungua kwa matumizi ya kawaida. Tukumbuke maneno ya Mungu kwa Musa kwenye Mlima Sinai: “Itakuwa Jubilei kwenu; kila mmoja wenu atarudi kwenye mali yake na familia yake. Mwaka wa hamsini utakuwa Jubilei kwenu; Msipande mbegu wala kuvuna mazao ya shambani peke yake, wala kuvuna mizabibu ambayo haijakatwa. Kwa maana ni Jubilei; itakuwa takatifu kwenu; lakini mtaweza kula mazao ya mashambani” (Mambo ya Walawi 25, 10-12).

Baba Mtakatifu anaendelea kuwa “Tumeitwa kuiga maisha ya usawa na endelevu ambayo yanaipatia Dunia mapumziko inavyostahili, pamoja na riziki za kutosha kwa wote ambao hawaharibu mifumo ikolojia inayotuunga mkono. Hata kabla ya janga la Uviko 19 tuliamini ilikuwa muhimu “kutafakari juu ya mtindo wetu wa maisha na jinsi chaguzi zetu za kila siku kuhusu chakula, matumizi, usafiri, matumizi ya maji, nishati na bidhaa nyingi za kimwili mara nyingi ni za kutojali na zina madhara" (Ujumbe kwa Siku ya Dunia ya Maombi kwa Huduma ya Uumbaji, 1 Septemba 2019). Sasa hebu tuongeze hitaji la tafakari ambayo inajumuisha pia mustakabali wa teknolojia mpya na ni maamuzi gani tutafanya, kama ubinadamu, ili yasiendane na ulimwengu wa udugu na matumaini. Tumeitwa kuondoka katika eneo letu la faraja na kupendekeza masuluhisho ya kibunifu na mbadala, ili sayari ibaki kuwa na uwezo wa kuishi na kuwepo kwetu duniani kusiwe hatarini. Matatizo mapya yanahitaji ufumbuzi mpya. Ni lazima tutafakari kuhusu matatizo ya kimaadili yanayoletwa na matumizi ya kila mahali ya teknolojia, tukivutia maarifa jumuishi ili kuzuia dhana ya kiteknolojia kuendelea kutawala.

Heshima ya kila mwanamume na kila mwanamke ndio jambo letu kuu tunapojenga mustakabali ambao hakuna mtu ametengwa. Si suala tena la kuhakikisha uendelevu wa aina ya binadamu kwenye sayari inayozidi kutishiwa, bali ni kuhakikisha kwamba uhai huo unaheshimiwa nyakati zote. Na kama hatukuweza kuguswa kwa wakati tulipokabiliwa na suala la mazingira, badala yake tunaweza kufanya hivyo tunapokabiliwa na kile kinachochukuliwa kuwa moja ya mabadiliko makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni ya ubinadamu, kupenya kwa AI katika maeneo yote ya maisha yetu. maisha ya kila siku. Hivyo wito wa kuwa mahujaji wa matumaini. Napenda taswira ya hujaji, “anayejiweka madarakani na hivyo anaweza kuvuka mipaka. Anatoka mwenyewe, anafungua upeo mpya, na akirudi nyumbani hayuko sawa, na nyumba yake haitakuwa sawa pia” ("Hebu turudi kuota", Piemme, 2020).

Zaidi ya hayo, safari ya hujaji si tukio la mtu binafsi, bali ni la jumuiya, inaashiria chapa ya mabadiliko yanayoongezeka ambayo yanaelekea msalabani, ambayo daima hutupatia uhakika wa uwepo na usalama wa matumaini. Kuweka nje "ni kawaida ya wale wanaoenda kutafuta maana ya maisha" (Hati ya Jubilei 2025). Kumbuka niliyowambia hapo mwanzo: tumaini ni nanga yetu na tanga yetu. Tuchukuliwe nayo twende hija kuelekea ujenzi wa ulimwengu huo wa kidugu zaidi tunao uota, ambamo utu wa mwanadamu unatawala kila taifa na unawiana na Mama Dunia.

Kitabu cha Papa Jubilei 2025
18 November 2024, 13:22