Papa Francisko amkumbuka Ayuso:Bidii katika udugu kati ya watu na dini
Na Angella Rwezaula-Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Novemba 2024, alituma salamu za rambirambi kwa Padre David Costa Domingues, Mkuu wa Shirika wa Wasimisionari Wakomboniani wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Roma. Katika telegramu hiyo Papa aliandika kuwa baada ya kupokea habari za kifo cha mpendwa Kardinali Miguel Angel Ayuso Guixot, Mwana wa Kiroho wa Mtakatifu Daniel Comboni, kilichowadia baada ya ugonjwa wa muda mtefu ambao alivumilia kwa imani kuu katika Bwana, anaeleza ukaribu wake kwa Shirika la Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, ambalo alijiunga mnano 1973 na kama ilivyo kwa familia nzima inayoombolezwa kwa ajili ya Kardinali na wote ambao walimfahamu na kumpenda. Papa anamkumbuka kwa upendo na mshangao wa Kaka yetu ambaye alihuduma Injili na Kanisa kwa kujitoa kabisa na kwa unyeti wa roho. Papa Francisko alifikiria kwa shukrani huduma aliyotoa bila kujibakiza, kwanza kabisa kwa ari ya kimisionari huko Misri na Sudan, baadaye kama Rais wa Taasisi ya Kipapa Mafunzo ya Kiarabu na Kiislamu,(PISAI) na hatimaye katika huduma ya Curia Romana katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo ya Kidini kama Mwenyekiti ambapo alikuwa amechaguliwa mnamo 2019.
Baba Mtakatifu Francisko alibainisha kuwa, kwa kila kazi ya kitume alikuwa daima akiongozwa na shauku ya kushuhudia, kwa unyenyekevu na hekima, upendo wa Mungu kwa binadamu, kwa kujikita katika Udugu kati ya watu na dini. Papa Francisko kwa njia hiyo anainua sala zake kwa Baba wa Huruma ili kwa maombezi ya Bikira Maria, apokee mtumishi wake mwaminifu katika Yerusalemu ya Mbingu na kwa moyo, Baba Mtakatifu anatoa baraka zake kwa wote wanaoomboleza kuondoka kwake. Mazishi ya Kardinali Ayuso yatafanyika tarehe 27 Novemba 024 saa 8 alasiri katika Madhabahu ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Liturujia imeabainisha kwamba maadhimisho yataongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Decano wa Makardinali pamoja na Makardinali, Maaskofu wakuu na Maaskofu. Na hatimaye Ibada na sala za mwisho zitaongozwa na Papa Francisko (Ultima Commendatio na Valedictio.)