2024.11.21 Nembo ya Ziara ya Kitume ya Papa Francisko kwa Jimbo la Ajaccio  kisiwani Corsca. 2024.11.21 Nembo ya Ziara ya Kitume ya Papa Francisko kwa Jimbo la Ajaccio kisiwani Corsca. 

Papa Francisko atatembelea Ajaccio,Corsica tarehe 15 Desemba 2024!

Baba Mtakatifu Francisko atafanya Ziara ya Kitume katika kisiwa cha Mediterania cha Corsica nchini Ufaransa,tarehe 15 Disemba 2024 kufunga Kongamano la Kimataifa kuhusu "Udini maarufu wa Mediteranea lililoandaliwa na Jimbo Katoliki la Ajaccio.Hata maaskofu wa Italia,Ufaransa na Hispania watashirik.Papa ataongoza kikao cha mwisho,atakutana na Makleri katika Kanisa Kuu na kuadhimisha Misa.Kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege atakutana na Rais Macron.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 23 Novemba 2024, Msemaji mkuu wa vyombo habari vya Vatican kwa waandishi wa habari amethibitisha kuhusu Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifukatika Jimbo la Ajaccio mnamo tarehe 15 Desemba 2025 kwamba: “kwa kupokea mwaliko kutoka kwa Mamlaka ya raia na ya kikanisa ya nchi, Papa Francisko atatimiza katika fursa ya kuhitimisha Kongamano  linaoongozwa na mada “Udini maarufu katika Mediterrania (La religiosité populaire en Méditerranée.)

Pamoja na hayo ratiba kamili ya siku hiyo moja ya Dominika tarehe 15 Desemba 2024 imeambatanishwa, ambapo Papa Francisko anatarajiwa kuondoka saa 1.45 Asubuhi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa huko Roma/Fiumicino Roma  hadi  Ajaccio na kuwasili katika Uwanja wa Ndege kimataifa  wa Ajaccio saa 3.00 kamili asubuhi na makaribisho rasimi. Saa 4:15 atashiriki katika Kikao cha mwisho cha Kongamano na Hotuba ya Papa inatarajiwa katika Jumba la Mkutano huko Ajaccio. Saa 5.20, itafanyika sala ya Malaika wa Bwana akiwa na Maaskofu, mapadre, mashemasi, watawa kike na kiume na waseminaria katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mpalizwa, ambapo pia Papa anatarajiwa kutoa hotuba yake. Saa 9.30 alasili, Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa “Place d’Austerlitz” (“U Casone”)Wakati saa 11.30, jioni atakatuna na rais wa Jamhuri  ya Ufaransa, Bwana Emmanuel Macron, katika Uwanja wa Nde ge wa Ajacco. Itafuatia sherehe za kuanga, saa 12.00 jioni na 12.15 kuanza safari katika Uwanja wa Kimataifa wa Ajaccio kurudi mjini Roma ambapo anararajiwa kufika saa 1.05 jioni katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa Fiumicino Roma.

Alama za kauli mbiu ya Ziara hiyo

Katika ziara ya siku moja ya Baba Mtakatifu katika kisiwa cha Mediterania, alikozaliwa Napoleon, ambapo  mkutano ulioandaliwa na Jimbo la Ajaccio kuhusu “Udini Maarufu katika Bahari ya Mediterania vilevile  maaskofu wa Italia, Ufaransa na Hispania pia wanashiriki. Nembo na Alama za Ziara ya Baba Mtakatifu inatawaliwa na Rangi ya kijani-bluu kabisa kuwakilisha bahari, Corsica imechorwa kwenye sehemu ya juu kushoto kwa kutumia mistari ya wima ya samawati.Mstari wa juu zaidi unaishia katika umbo la msalaba, unaoashiria imani katika Kristo, na umefungwa kwenye mstari wa njano unaoshuka kutoka juu, kiashiria cha Roho Mtakatifu.

Kwa upande wa kulia wa kisiwa kilichochorwa tunapata, rangi ya njano sawa, rangi ya mwanga na ya Vatican, jina la Papa Francisko limeandika kwa lugha ya Kicorsika “Papa Francescu”na, chini, kuna maandishi meupe ya kauli mbiu ya Ziara ya Kitume isemayo: “Jésus passa en faisant le bien” (Mndo 10:38), yaani “Yesu wa Nazareti, alipita akitenda kazi njema” ambayo ni usemi wa Matendo ya Mitume ulitumika kwa tukio hilo, na ambao unataka kukumbusha kwamba Papa atalitembelea Kanisa la Corsica kama Mchungaji anayepita miongoni mwa watu wake. Katika sehemu ya chini kuna Mama, Malkia wa Corsica, katika rangi ya bluu sawa na kisiwa hicho. Bikira Maria anaoneshwe kwenye upande kwa mtazamo na mikono yake imeelekezwa juu kwa kuzingatia mandhari ya nyuma, anaonekana kana kwamba amezama baharini. Chini  kulia, pia  kuna maneno ya manjano ambyo ni tarehe ya Ziara ya Papa Francisko.

Papa atafanya hija huko Corsca
23 November 2024, 13:35