Tafuta

2024.11.13 Papa amekutana na kundi kutoka Ufaransa. 2024.11.13 Papa amekutana na kundi kutoka Ufaransa.  (Vatican Media)

Papa:kumgusa na kumsaidia maskini ni kisakramenti katika Kanisa!

Katika Mkutano wa Papa na washiriki wa Foyer kutoka ufaransa wa Mama Yetu wa Abri na Jumuiya ya Marafiki Gabriel Rosset,alisisitiza umuhimu wa kusindikiza maskini zaidi,kutoa uso thabiti kwa Injili ya Upendo.Papa ametoa mwaliko wa kuwa mafundi wa huruma kwa kufuata mfano wa Maria kwa kuruhusu kugundua upya heshima na matumaini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Wajumbe wa Foyer ya Mama Yetu wa Mtakatifu Abri na Chama cha Marafiki wa Gabrieli Rosset Jumatano tarehe 13  «Novemba 2024. Akianza Baba Mtakatifu amesema Wapendwa kaka na dada, nitazungumza kwa kitaaliano lakini mkatakuwa na mfasiri hapa. Asante kwa uwepo wenu, watoto ni wazuri sana. “Nina furaha kuwakaribisha na kutoa shukrani za Kanisa kwa ajili ya misheni zenu. Ninyi ni mashuhuda wa huruma na upole wa Mungu kwa wale wanaohitaji zaidi. Mambo matatu ya Mungu: ukaribu, huruma na upole.” Papa Francisko amesema Mwanzilishi wao, Gabriel Rosset, wanayemkumbuka mwaka huu katika kumbukumbu ya miaka hamsini ya kifo chake, aliwahurumia sana ndugu zake; alisikiza kilio cha maskini wala hakugeuza kichwa chake wala kufumba macho. Alijibu kwa imani na ujasiri, kwa njia thabiti, akianzisha Notre-Dame des Sans-Abri.

Kujua uwepo wa kristo katika maskini

Alijua jinsi ya kutambua uwepo wa Kristo katika maskini: ni ndugu zetu. Hebu tukumbuke daima: “Katika kila mmoja wa hawa “wadogo” Kristo mwenyewe yupo. Mwili wake unaonekana tena kama mwili ulioteswa, uliojeruhiwa, uliopigwa mijeledi, unaokimbiwa... kutambuliwa na sisi, kuguswa na kutunzwa” (Misericordiae Vultus, 15). Kumgusa mtu maskini, kusaidia maskini, ni “sakramenti” katika Kanisa. Leo hii wanaendelea na kazi ya Gabriel Rosset. Papa aidha alisema wao pia ni mafundi wa huruma na upole wa Mungu: kwa kuwasindikiza na watu wasio na makazi, mnatoa uso thabiti kwa Injili ya upendo. Kwa kuwapa makao, chakula, tabasamu, kunyoosha mikono yao bila hofu ya kuchafuka, unawarudishia heshima yao na kujitolea kwao kugusa moyo wa ulimwengu wetu ambao mara nyingi haujali. Mwanzilishi wao alitaka utume wao uwekwe chini ya mtazamo wa Mama wa Kristo, Mama ambaye haachi kuwaangalia wale wote wanaoteseka katika mwili na moyo. “Ninaamini hili ni la msingi kwa sababu, kulingana na Biblia, huruma inahusiana kwa karibu na tumbo la uzazi.

Huruma,upole na uwazi

Papa Francisko kwa kukazia amesema "Huruma na upole, udugu na uwazi, mkono ulionyooshwa na kukataa utamaduni wa kutupa: ni katika ishara hizi thabiti za upendo ambapo Kanisa linakuwa ni ishara hai ya huruma ya Mungu kwa watoto wake wote. Papa amewaalika utafakari Bikira Maria, sura kamili ya Kanisa, anaakisi huduma yao kwa maskini zaidi. "Papa amependa kutafakari Mama Maria wa Wasio na Makazi kama Bikira wa Huruma, ambaye anafungua mikono yake wazi kuwakaribisha kila mtu, kwa sababu kila mtu ana nafasi karibu na Mariamu, karibu na Kristo. Haogopi kufungua vazi lake, na kulifanya kuwa kimbilio dhidi ya mvua na moto mkali wa jua. Anatoa mali yake yenye thamani zaidi, ambayo ni Yesu, akiwaacha maskini waje karibu naye iwezekanavyo ili kupokea huruma na kitulizo kutoka kwa mikono yake iliyonyoshwa.

Mama Maria anajibu mahitaji ya ndugu katika mazingira magumu

Papa amewaomba waende katika shule ya Maria. “Maria kwanza kabisa ni mwanamke wa maisha ya ndani: anatafakari na kuliweka moyoni mwake Neno la Mungu ambalo humtia nguvu katika kila tendo. Yeye pia ni mwanamke wazi, mwanamke anapatikana kwa mshangao wa Mungu.”  Hii ndiyo sababu yeye anatazama na kutembea. “Maria anajibu mahitaji ya kaka na dada walio katika mazingira magumu, lakini zaidi ya yote anatarajia mahitaji yao: kama huko Kana, ambapo anajua kwamba divai imeisha. Anamfuata Mwanawe njiani, hadi Kalvari; haogopi kugusa mateso ya ulimwengu anapoyakaribisha mikononi mwake chini ya msalaba”. Papa alisema hao marafiki wapendwa wa Notre-Dame des Sans-Abri, kwa wengi ni picha hai ya huruma hii ya uzazi.

Kikundi kutoka ufaransa
Kikundi kutoka ufaransa

Kwa kuwepo kwao na kusikiliza kwao, kunaonesha kwamba Maria na Yesu hawaachi kutembea pamoja na ndugu zao, wale ambao mara nyingi husahauliwa. Papa ameomba watekeleze huduma yao kwa nguvu ya upendo. Waruhusu wanaume na wanawake wengi kugundua tena utu wao na tumaini lao, hata katikati ya majaribu. Papa amewakabidhi kwa sala ya mama ya Mama, ambaye anawaangalia wao na watu wote wanaowasindikiza. Papa wabariki wote kutoka ndani ya moyo wao . Na tafadhali wasisahau kumuombea.

Papa amekutana na kundi moja kutoka uranasa
13 November 2024, 18:41