Papa Francisko kwa ESNE:kuna hitaji la wanafunzi kuendeleza utume wa Yesu Kristo aliokabidhi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko akutana na wawakilishi wa ‘El Sembrador - Nueva Evangelización’ yaani ‘Mpanzi - Uinjilishaji Mpya’, (Ni Mtandao wa Mawasiliano ya Uinjilishaji Mpya), Alhamisi tarehe 28 Novemba 2024 mjini Vatican. Katika hotuba yake alianza na salamu kwa Noeles Díaz” Mwanzilishi ambaye alisafisha viatu vyake na kumshukuru kwa kuanzisha utume huo wa mawasiliano ambao ulimpekelea kuunda Chaneli ya Runinga ya ESNE. Papa ameeleza jinsi ambavyo bado anakumbuka alipokutana naye, kwenye ndege iliyowapeleka kutoka Roma hadi Cuba na kisha Mexico, mnamo Februari 2016.
Papa alikuwa alisema kwamba alikuwa amemaliza mazungumzo na kuwatembelea waandishi wa habari, alipomuona mmoja wao akiwa anasafisha viatu vyake, yaani aliinama chini na kuanza kusafisha viatu vyake. Noel alikuwa amemuahidi mama yake kwamba angesafisha, viatu vya Papa. Kwa kumkubuka Mama yake amesema “Na hapa ninatulia kwa muda, ili kila mmoja wenu afikirie mama yake. Wengine wanao hai, wengine wanao huko Mbinguni, lakini kwa moyo wa shukrani kwa kila kitu ambacho wamepokea kutoka kwa mama yao. Urithi huo ambao akina mama pekee wanaweza kutoa.”
Papa Francisko alisema alivyovutiwa na sura ya imani aliyonayo na kujitolea kwa Mungu mpaji. Na hivyo chaneli ya runinga ya ESNE ilianza. Hivi ndivyo ndoto hiyo ilianza, ambayo inawezekana na inaendelea kutokana na kujitolea kwa jumuiya hii ya wawasilianaji, na hao waliokuwa mbele yake na washiriki wengine wengi. Papa ameuliza swali “Je! unajua mlinzi mkuu wa mawasiliano ni nani? Ni Utatu Mtakatifu, kwa sababu wanaishi kwa kuwasiliana wao kwa wao.” Fikirieni juu yake! Asante kwa kuendelea kuota! Asanteni kwa kuendelea kuinjilisha, waaminifu kwa wito wa Mtakatifu Yohane Paulo II kwa uinjilishaji mpya! Papa Francisko alithibitisha alivyosikia kuhusu mpango mzuri “Yo soy el 73” yaani “mimi ni wa 73” ni wakfu maalum kwa Yesu ili kujenga jumuiya ya wainjilishaji wenye uwezo wa kuwasilisha furaha ya Injili na huruma ya Mungu. Hii ni kutaka kutukumbusha jinsi ambavyo Yesu baada ya wale, Bwana alichagua wafuasi sabini na wawili zaidi.(Rej Lk 10)
Na leo tuna hitaji kubwa la wanafunzi wanaoendeleza utume aliokabidhiwa na Bwana kwa Yesu Kristo, pia kuinjilisha kwa njia ya mawasiliano. Asante kwa kazi mnayofanya. Na asante kwa kuleta sauti na ujumbe wa Papa kwa watu wengi nchini Marekani na nchi nyingine zinazozungumza Kihispania. Asante kwa kuwasaidia ndugu wengi kusali, kufuata Misa Takatifu kutoka nyumbani kama hawawezi kusafiri, kupokea malezi ya Kikristo na habari za kikanisa. Ninakushukuru pia na zaidi ya yote kwa sababu kwa kazi yenu mko karibu na wahamiaji wengi kutoka nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini ambao wanahitaji kuwa na vituo vya kumbukumbu, ujumbe wa faraja katika lugha yao ya asili. Msiache kutenda.
Papa amewashukuru pia kwa ushirikiano ambao umedumisha kwa miaka mingi na vyombo vya habari vya Vatican vya Baraza la Mawasiliano. Amewahimiza kusonga mbele, bila kukoma kutazama Mbinguni na ndugu zao wanaohitaji sana, Papa alisema: “mtazameni Yesu, watazame walio na uhitaji zaidi,” na fanyeni hivyo kwa ukarimu na ubunifu, mkiwa mmejikita kwenye mwamba wa Petro, daima mkiwa wanyenyekevu kwa ishara za Kanisa.” Papa anawaombea na kuwasindikiza kwa baraka zake. Wasisahau kumuombea.