Papa Francisko:matendo ya nje hayahesabiki bali upendo wa moyo kwa ndugu na imani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 3 Novemba 2024, akiwa katika dirisha la Jumba la Kituma ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Papa akianza amesema “Injili ya liturujia ya leo(Mk12, 28-34)inatunzungumzia moja ya majadiliano ambayo Yesu alifanya katika hekalu la Yerusalemu. Mmoja ya waandishi alimkaribia na kumuuliza: “Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? Yesu alijibu akiwapatia pamoja maneno mawili msingi ya sheria ya Musa:“nawe mpende Bwana Mungu wako” na “mpende Bwana jirani yako”(Mk 12, 30-31).
Katika swali lake, mwandishi anatafuta amri ya kwanza,yaani msingi ambao upo katika misingi yote; kiukweli, kama tujuavyo, wayahudi walikuwa na sheria nyingi kana kwamba walikuwa wakitafuta msingi wa yote, ule ambao ulikuwa wa msingi na kukubaliana juu ya mojawapo, na kulikuwa na majadiliano kati yao, majadiliano mazuri kwa sababu walikuwa wakitafuta ukweli”, Papa amesisistiza na kuongeza “na mara nyingi walikuwa wakijadiliano kuhusu amri gani iliyo kuu ambayo inategemea yote yanayobakia. Amri hii ni muhimu hata kwa ajili yetu, kwa ajili ya maisha yetu na kwa ajili ya safari yetu ya imani.”
Papa Francisko amesema kuwa “Hata sisi, kiukweli wakati mwingine tunahisi kupotea katika mambo mengi na tunajiuliza: lakini mwisho wa yote, jambo muhimu zaidi ya yote ni lipi? Ni wapi ninaweza kupata kiini cha maisha, na imani yangu, ambacho kinaaakisi yote hayo? Na Yesu anatupatia jibu, kwa kuunganisha amri mbili pamoja: ‘Kumpenda Bwana Mungu na kumpenda jirani’ ndiyo moyo kidogo wa imani yetu, ambapo hapo awali zilizikuwa zimetengenishwa yaani upendo wa Mungu na upendo wa jirani.”
Papa amesisiza tena kwamba “Hiyo inachukua sheria yote na manabii; na tunaweza hata sisi kusema: huo ndiyo moyo wa maisha ya kikristo.” Baba Mtakatifu aliendelea kwamba “wote tunahitaji kurudi katika moyo, wa maisha na ya imani, kwa sababu moyo ni kisima na mzizi wa nguvu zote, kwa utambuzi, shauku na chaguzi (Dilexit nos, 9). Na Yesu anatuambia kuwa kisima cha yote ni upendo ambao hatupaswi kamwe kuutengenisha Mungu na binadamu. Mambo mengi yanapaswa kufanywa kwa upendo.
Kwa wafuasi wa kila wakati, Bwana anawambia: Katika safari yao, kinacho hesabiwa si mazoezi ya kijujuu, kama sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia(Mk 12,33), bali tabia ya moyo ambayo kwayo unajifungua kwa Mungu na kwa ndugu zako kwa upendo. Tunaweza kufanya mambo mengi, kiukweli, lakini kuyafanya kwa ajili yetu wenyewe tu na bila upendo, kwa moyo uliokengeushwa au kwa moyo uliofungwa. Papa ameomba kukumbuka hilo kwamba: “Bwana atakapokuja, na atauliza awali ya yote, upendo je ulipendaje, ambapo tunatambua kuutoa na ule ambao hatukuweza kutoa.
Ni muhimu kwa hiyo kukazia katika moyo, wa amri kuu zaidi ya Mpenda Bwana Mungu wako, na mpende jirani kama unavyojipenda mwenyewe na kila siku ili kufanya kila siku zoezi la dhamiri yetu na kujiuliza: upendo kwa Mungu na kwa jirani ni kiini cha maisha yangu? Sala yangu inanisukuma kwa Mungu kuelekea ndugu na kuwapenda bure? Ninatambua uso wa wengine kwa uwepo wa Bwana? Bikira Maria aliyekuwa anapeleka sheria ya Mungu iliyokita katika moyo wake safi, atusaidie kupenda Bwana na Ndugu.