Papa Francisko:Ni kwa njia ya Roho Mtakatifu tunaweza kuita Baba

Ni katika maombi hasa ambapo Roho Mtakatifu anajidhihirisha kama "Paraclete",mtetezi wetu.Yeye hatushitaki mbele za Baba,anatutetea.Ndiyo,anatutetea, anatusadikisha ukweli kwamba sisi ni wenye dhambi lakini anafanya hivyo ili tuweze kufurahia furaha ya huruma ya Baba,na si kutuangamiza.Ni katika tafakari ya Katekesi ya Papa tarehe 6 Novemba 2024 kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kama kawaida ya kila Jumatano Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 6 Novemba 2024. Katika mwendelezo wa mada ya Roho Mtakatifu, kwa kufuata somo lililosomwa Papa amesema “Tendo la utakaso la Roho Mtakatifu, na zaidi  kwa njia ya Neno la Mungu na Sakramenti, linaoneshwa katika sala, na ni kwa hili ambapo tunataka kujikita nalo katika tafakari ya leo hii ya sala. Papa amesema kuwa Roho Mtakatifu ni wakati huo huo fundisho  na lengo la maombi ya Kikristo. Yaani Yeye ndiye mwenye  kutoa sala na ndiye aliyepewa maombi. Tunaomba ili kupokea Roho Mtakatifu na tunapokea Roho Mtakatifu ili tuweze kuomba kweli, yaani, kama watoto wa Mungu, si kama watumwa. Hebu tufikirie jambo hili kidogo: ombeni kama watoto wa Mungu, na si kama watumwa.

Ni lazima kila wakati tuombe kwa uhuru, Papa ameongeza kusema: “ inawezekana mwingine akafikiri kwamba: “Leo lazima niombe hivi na hivi  kwa sababu niliahidi hivi na  hivi. La sivyo, nitakwenda kuzimu.” Hapana, hayo siyo maombi! Maombi ni ya  bure. Unaomba  na wakati huo huo Roho anakusaidia kuomba. Unasali unapohisi hitaji la kuomba moyoni mwako na unapohisi hakuna kitu, wewe simama na ujiulize: “Kwa nini sihisi hamu ya kuomba? Nini kinatokea katika maisha yangu?” Papa ameshauri. Lakini siku zote, hiari katika maombi ndiyo hutusaidia zaidi. Hii ina maana ya kuomba kama watoto, si kama watumwa.”

Papa Francisko na wanahija
Papa Francisko na wanahija

Kwanza, ni lazima tuombe ili kupokea Roho Mtakatifu. Kuhusiana na hilo Papa Francisko ameongeza kusema “, kuna neno lililo sahihi kabisa kutoka kwa Yesu katika Injili: “Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu mema, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa Roho Mtakatifu hao wamwombao” ( Lk 11:13 ). Papa amesisitiza kuwa: “Kila mmoja wetu, anajua jinsi ya kuwapa watoto vitu vizuri, wawe watoto, wajukuu au marafiki. Watoto wadogo daima hupokea mambo mazuri kutoka kwetu. Na jinsi gani? Baba hatatupatia Roho! Na hii inahitaji kutupatia ujasiri na kusonga mbele.”  Baba Mtakatifu amesema kwamba “Katika Agano Jipya tunaona Roho Mtakatifu akishuka kila wakati wa maombi. Anamshukia Yesu katika ubatizo wake katika Yordan, alipokuwa“akiomba”(Lk 3:21); na anawashukia wanafunzi siku ya Pentekoste, huku “wakidumu na kukubaliana katika kuomba” (Mndo 1:14). Ni "nguvu" pekee tuliyo nayo juu ya Roho wa Mungu.

Nguvu ya maombi: yeye hapingi maombi. Tunaomba na anakuja. Juu ya Mlima Karmeli, manabii wa uongo wa Baali, mkumbuke kifungu hiki kutoka katika Biblia   walichochewa kuomba moto kutoka mbinguni juu ya dhabihu yao, lakini hakuna kilichotokea, kwa sababu walikuwa waabuduo sanamu: waliabudu mungu ambaye hayupo; Eliya alianza kuomba na moto ukashuka na kuteketeza maangamizi (taz 1 Wafalme 18:20-38). Kanisa kwa uaminifu linafuata mfano huu: daima midomoni mwake linasihi kwamba “Njoo! Njoo! kila wakati linapogeuka kwa Roho Mtakatifu, linasema “Njoo” kila mara,  linamgeukia Roho Mtakatifu kwa neno hilo. Na linafanya zaidi ya yote katika Misa ili ashuke kama umande na kutakasa mkate na divai kwa ajili ya dhabihu ya Ekaristi.

Papa Francisko katika katekesi
Papa Francisko katika katekesi

Papa kwa kukazia zaidi amesema “Lakini pia kuna kipengele kingine, ambacho ni muhimu zaidi na cha kutia moyo kwetu: Roho Mtakatifu ndiye anayetupa maombi ya kweli. Mtakatifu Paulo anasema hivi: “Roho - ((anasema Mtakatifu Paulo)) - huja kwa msaada wa udhaifu wetu; kiukweli, mara nyingi hatujui kuomba inavyopasa, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa; na yeye aichunguzaye mioyo anajua mapenzi ya Roho, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama makusudi ya Mungu” (Rm 8:26-27). Kwa njia hiyo “Ni kweli, hatujui kuomba, hatujui. Tunapaswa kujifunza kila siku, sababu ya udhaifu huu wa maombi yetu ilioneshwa zamani kwa neno moja, lililotumiwa kwa njia tatu tofauti: kama kivumishi, kama nomino na kama kielezi,” Papa amekazia.

“Ni rahisi kukumbuka, hata kwa wale ambao hawajui Kilatini, na ni muhimu kukumbuka, kwa sababu ina mkataba mzima peke yake, mambo haya matatu. Sisi wanadamu tulisema kuwa,” mali, mala, male petimus” ambayo ina maana: kuwa mbaya (mali), tunaomba mambo yasiyofaa (mala) na kwa njia mbaya (petmus) Yesu anasema: “Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo mengine mtapewa” (Mt 6:33); badala yake tunatafuta kwanza ziada yote, yaani, masilahi yetu - mara nyingi na tunasahau kabisa kuomba ufalme wa Mungu, tunamwomba Bwana kwa Ufalme na kila kitu huja pamoja naye. Roho Mtakatifu anakuja, ndiyo, ili kuokoa udhaifu wetu, lakini bado anafanya jambo muhimu sana: anatuhakikishia kwamba sisi ni watoto wa Mungu na kuweka midomo yetu kilio: “Baba!” (Rm 8:15; Gal 4.6). Hatuwezi kusema “Abba “-“Baba, Hatuwezi kusema “Baba” bila nguvu za Roho Mtakatifu.

Papa Francisko katika Katekesi 6 Novemba
Papa Francisko katika Katekesi 6 Novemba

Maombi ya Kikristo siyo ya mwanadamu anayezungumza na Mungu kutoka upande mmoja wa simu na upande mwingine, hapana, ni Mungu anayeomba ndani yetu! Tunaomba kwa Mungu kupitia kwa Mungu. Kuomba ni kujiweka ndani ya Mungu na Mungu aingie ndani yetu,” Papa amesisitiza. Ni katika maombi hasa ambapo Roho Mtakatifu anajidhihirisha kama “Paraclete”, yaani mtetezi wetu. Yeye hatushitaki mbele za Baba, bali anatutetea. Ndiyo, anatutetea, anatusadikisha ukweli kwamba sisi ni wenye dhambi (rej. Yh 16:8), lakini anafanya hivyo ili tuweze kufurahia furaha ya huruma ya Baba, na si kutuangamiza kwa hisia tasa za hatia. Hata mioyo yetu inapotushutumu kwa jambo fulani, anatukumbusha kwamba “Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu” (1 Yh 3:20).

“Mungu ni mkuu kuliko dhambi zetu. Sisi sote ni wenye dhambi, lakini tunafikiri: labda baadhi yenu - sijui - ambao wanaogopa sana mambo waliyofanya, wanaoogopa kukemewa na Mungu, wanaoogopa mambo mengi na hawawezi kupata amani.” Papa aliendelea: “Jiweke katika maombi, mwite Roho Mtakatifu, naye atawafundisha jinsi ya kuomba msamaha. Na mnajua nini? Mungu hajui sarufi nyingi na tunapoomba msamaha, haturuhusu kumaliza! “Kwa sababu  hapo, haturuhusu kumaliza neno msamaha. Anatusamehe kwanza, anatusamehe daima, huwa karibu nasi ili atusamehe, kabla hatujamaliza kusema neno la msamaha. Tunasema “Kwa…” na Baba hutusamehe daima.”

Papa Francisko katika katekesi
Papa Francisko katika katekesi

Roho Mtakatifu hutuombea ((kwa ajili yetu, lakini)) na pia hutufundisha kufanya maombezi, kwa upande wake, kwa ajili ya ndugu zetu - “yeye hutuombea na kutufundisha kuwaombea wengine -; maombi ya maombezi anatufundisha kwamba: mwombeeni mtu huyu, mwombeeni huyo mgonjwa, aliye gerezani, mwombeeni..., mwombee mama mkwe pia, ee! Na siku zote omba na daima.” Maombi haya yanampendeza Mungu hasa kwa sababu ndiyo ya bure na yasiyopendezwa zaidi. Wakati kila mtu anaomba kwa ajili ya kila mtu, hutokea Papa alibainisha kwamba Mtakatifu Ambrose alisema hivi - kwamba kila mtu anapomba kwa ajili ya kila mtu; maombi hayo huongezeka. Hivyo na Sala iko hivyo.”

Hapa kuna kazi ya thamani na ya lazima katika Kanisa, hasa wakati huu wa maandalizi kwa ajili ya Jubilei: kuungana na Mfariji (Paraclete) ambaye anatuombea sisi sote ((watakatifu)) kulingana na mipango ya Mungu. “Lakini msiombe kama kasuku, tafadhali!Msiseme “Blah, blah, bla…” La! Kusema “Bwana”, bali iseme kutoka moyoni. “Nisaidie Bwana”, “Nakupenda Bwana.”Na unapoomba Baba Yetu, omba “Baba, Wewe ni Baba yangu.” Omba kwa moyo wako na sio midomo yako, usifanye kama kasuku.” Papa ameonya ((Kamwe kama katika nyakati hizi “Roho na Bibi-arusi walilia pamoja kwa Yesu: Njoo!” (rej. Ufu 22:17)) “Roho na atusaidie katika maombi, ambayo tunayahitaji sana. Asante. Papa Francisko amehitimisha.

Katekesi ya Papa
06 November 2024, 11:02