Papa Francisko:sherehe za Kristo Mfalme:Kinachookoa Ulimwengu ni upendo wa bure!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 24 Novemba 2024 ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Kristo Mfalme, Sanjari na Maadhimisho ya Siku ya 39 ya Vijana Duniani kwa Ngazi za majaimbo yote, ameongoza Misa Takatifu Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Katika mahubiri yake, Baba Mtakatifu ameanza kusema Mwishoni mwa mwaka wa kiliturujia Kanisa linaadhimisha Sherehe ya Bwana Wetu Yesu Kristo Mfalme, Mfalme wa Ulimwengu. Anatualika tumtazame Yeye, tumtazame Bwana, asili na utimilifu wa kila kitu (rej Kol 1,16-17), ambaye "ufalme wake hautaangamizwa" (Dan 7:14). Ni tafakari inayoinua na kusisimua. Hata hivyo, tukitazama huku na huku, kile tunachokiona kinaonekana tofauti, na maswali ya kutatanisha yanaweza kutokea ndani mwetu. Vipi kuhusu vita, jeuri, mikasa ya kiikolojia? Na nini cha kufikiria juu ya shida ambazo nyinyi pia, wapendwa vijana, mnapaswa kukabiliana nazo, mkitazama siku zijazo: ukosefu wa usalama wa kazi, kutokuwa na uhakika wa kiuchumi na zaidi, migawanyiko na tofauti ambazo zinakabili jamii? Kwa nini haya yote yanatokea? Na tunaweza kufanya nini ili kuepuka kukandamizwa nayo? Kweli, haya ni maswali magumu, lakini ni maswali muhimu. Kwa sababu hiyo Papa Francsiko ameendelea, “ leo, tunapoadhimisha Siku ya Vijana Duniani katika Makanisa yote, ninapenda kutoa pendekezo hasa kwenu ninyi vijana, kwa kuzingatia Neno la Mungu, tutafakari mambo matatu, yanayoweza kutusaidia kuendelea kwa ujasiri katika safari yetu, kupitia changamoto tunazokutana nazo. Na vipengele hivi ni: tuhuma, maafikiano na ukweli(accuse, i consensi e la verità). Kwa hiyo Papa Francisko amependa kudadavua kimoja baada ya kingine.
Kwanza: tuhuma. Injili ya leo inatuonesha pamoja na Yesu katika nafasi ya mshitakiwa (rej. Yh 18:33-37). Yeye yuko - kama wanavyosema – ‘kizimbani’, kortini. Anayemhoji ni Pilato, mwakilishi wa Milki ya Roma, ambaye ndani yake tunaweza kuona akifananisha mamlaka zote ambazo katika historia huwakandamiza watu kwa nguvu za silaha. Pilato hapendezwi na Yesu. Lakini anajua kwamba watu wanamfuata, wakimchukulia kuwa kiongozi, bwana, Masiha, na Mwendesha Mashtaka hawezi kuruhusu mtu yeyote kuleta uharibifu na fujo katika "amani ya kijeshi" ya eneo lake. Kwa hiyo anawaridhisha maadui wenye nguvu wa nabii huyu asiyeweza kujitetea: anampeleka mahakamani na kutishia kumhukumu kifo. Naye, ambaye siku zote alihubiri haki, huruma na msamaha tu, haogopi, hajiruhusu kutishwa, wala haasi: Yesu anabaki mwaminifu kwa ukweli aliotangaza, mwaminifu hadi kufikia hatua ya kutoa maisha yake. Papa Francisko alisema: “wapendwa pengine wakati mwingine inaweza kukutokea hata ninyi mkawekwa "chini ya mashtaka" kwa kumfuata Yesu Shuleni, miongoni mwa marafiki, katika mazingira mnayotembelea mara kwa mara, kunaweza kuwa na wanaotaka kuwafanya mjisikie vibaya kwamba mmekosea kuwa waaminifu katika Injili na maadili yake, ili msipate kufanana, msijipinde kufanya kama wengine wafanyavyo.
Ninyi, hata hivyo, msiogope "hukumu", msijali: mapema au baadaye ukosoaji na mashtaka ya uwongo huanguka na maadili ya juu ambayo yanawaunga mkono yanafunuliwa kwa sababu wao ni wadanganyifu. “Wapendwa vijana, jihadharini msijiruhusu kulewa na udanganyifu. Tafadhali kuwa thabiti. Ukweli ni thabiti. Jihadharini na udanganyifu." Kinachobaki, kama Kristo anavyotufundisha, ni kitu kingine: ni kazi za upendo. Huo ndio unaobaki na unafanya maisha kuwa mazuri! Mengine haijalishi. Upendo wa kweli katika matendo. Kwa hiyo, Papa FRancisko amesisitiza “ninarudia: msiogope "hukumu" za ulimwengu. Endeleeni kupenda! "Lakini kupenda katika nuru ya Bwana, kutoa maisha ya mtu na kusaidia wengine."
Papa Fracisko amendelea na kipengele cha pili cha pili ambacho ni maafikiano au ridhaa. Yesu anasema: “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu” (Yh 18:36). Je, "Yesu na hii" inamaanisha nini? “Je, si ufalme wangu wa ulimwengu huu?” Kwa nini hafanyi chochote kuhakikisha mafanikio yake, kujifurahisha na wenye nguvu, kupata msaada kwa programu yake? Kwa nini asifanye hivyo? Je, anawezaje kufikiria kubadilisha mambo kama mtu "aliyeshindwa"? Kiukweli, Yesu anatenda hivyo kwa sababu anakataa mantiki yoyote ya uwezo (rej Mk10,42-45). Yesu yuko huru kutoka katika haya yote! Kwa hiyo amewaomba vijana hao kuwa hivyo na wao kwa sababu watafanya vyema kufuata mfano wake, kutojiruhusu kuambukizwa na tamaa - iliyoenea leo - tamaa ya kuonekana, kupitishwa na kusifiwa. Wale wanaojiruhusu kunaswa na marekebisho haya mwishowe wanaishia katika shida. Inahusu "kupiga kiwiko", kushindana, kujifanya, kuafikiana, kuuza maadili ya mtu ili kupata kibali kidogo na kuonekana. “Tafadhali kuwa makini kuhusu hili. Heshima yenu haiuzwi. Si ya kuuzwa! Kuweni makini.” Papa ameonya.
Lakini Mungu anawapenda jinsi mlivyo, si kama mnavyoonekana: mbele zake ndoto zenu safi ni za thamani zaidi kuliko mafanikio na umaarufu - na zina thamani zaidi - na uaminifu wa nia yenu ni wa thamani zaidi kuliko maafikiano. Msijiruhusu kudanganywa na wale ambao, kwa kuwashawishi kwa ahadi zisizo na maana, wanataka kuwanyonya tu kuwashawishi na kuwatumia kwa maslahi yao wenyewe. “Kuweni makini na unyonyaji. Kuweni wangalifu msije kuwa katika katika hali hii. Kuweni huru, lakini huru kulingana na heshima yenu." Msikubali kuwa "nyota ya siku", nyota kwenye mitandao ya kijamii au katika muktadha mwingine wowote! " Papa Francisko ametoa mfano mmoja kwamba anakumbuka "wakati mmoja, mwanamke kijana ambaye alitaka kuonekana - alikuwa mzuri - katika ardhi yangu. Na katika kwenda kwenye sherehe alijipodoa kabisa. Nilifikiri hivi: "Baada ya sherehe, ni nini kinachobaki?" na kwa hiyo Papa ameongeza kusema: “Msipodoe nafsi yenu, na mioyo yenu; bali muwe jinsi mlivyo: wakweli, wawazi. Msiwe "nyota ya siku" kwenye mitandao ya kijamii au muktadha mwingine wowote" Papa amekazia kusema tena hilo.
Anga ambalo wameitwa kuangaza ni kubwa zaidi: ni anga la upendo, ni anga ya Mungu, upendo usio na mwisho wa Baba ambao unaonekana katika mwanga mwingi mdogo: wote katika upendo wa uaminifu wa wanandoa, katika furaha isiyo na hatia ya watoto, katika shauku ya vijana, katika huduma ya wazee, katika ukarimu wa watu waliowekwa wakfu, katika upendo kwa maskini, katika uaminifu wa kazi. Kwa kusisitiza Papa amesema “Fikirieni mambo haya yatakayowafanya nyinyi vijana wote kuwa imara. Taa hizi ndogo: upendo mwaminifu wa wanandoa - jambo zuri -, furaha isiyo na hatia ya watoto - hii ni furaha nzuri! -; shauku ya vijana, kuwa na shauku ninyi nyote; utunzaji wa wazee. Swali: je mnajali wazee? Je, mtatembelea babu na bibi zenu? Ninyi ni wakarimu katika maisha yenu na mnafadhili kwa maskini katika uaminifu wa kazi zenu:? Hili ndilo anga la kweli, ambalo litang'aa kama nyota ulimwenguni (rej. Flp 2:15): na tafadhali msimsikilize mtu yeyote anayewadanganya na kuwaambia vinginevyo! Makubaliano hayaokoi dunia, wala hayatufanyi tuwe na furaha. Kinachookoa ulimwengu ni upendo wa bure. "Na upendo hauwezi kununuliwa, hauwezi kuuzwa: ni wa bure, ni mchango wa mtu mwenyewe.
Baba Mtakatifu akidadafua jambo la tatu ni ukweli. Kristo alikuja ulimwenguni “ili kushuhudia ukweli” ( Yh 18:37 ), na alifanya hivyo kwa kutufundisha kumpenda Mungu na ndugu zetu (rej Mt 22:34-40; 1 Yn 4:6-7 ). Ni pale kikweli tu, katika upendo, ambapo kuwepo kwetu kunapata mwanga na maana (rej 1 Yh 2:9-11). Vinginevyo tunabaki kuwa wafungwa wa uongo mkubwa. Na uongo mkuu ni upi? ule wa "umimi" wa kujitosheleza (rej Mwa 3:4-5), mzizi wa ukosefu wote wa haki na ukosefu wa furaha. "Mimi" ambayo inajielekeza yenyewe: Mimi, tu pamoja nami, daima "mimi" na sina uwezo wa kuangalia wengine, kuzungumza na wengine. Jihadharini na ugonjwa huu wa wa Umimi uliogeuka kuejielekeza binafasi. Kristo, ambaye ndiye njia, ukweli na uzima (Yh 14:6), akijivua kila kitu na kufa uchi msalabani kwa ajili ya wokovu wetu, anatufundisha kwamba ni katika upendo tu tunaweza kuishi, kukua na kusitawi katika maisha yetu ya hadhi kamili ( rej. Ef 4:15-16 ). Vinginevyo, kama Mwenyeheri Pier Giorgio Frassati alivyomwandikia rafiki - kijana kama ninyi - hauishi tena, lakini "unapita" (tazama Barua kwa Isidoro Bonini, 27 Februari 1925). Tunataka kuishi, si kupata riziki, na kwa hiyo tunajitahidi kushuhudia ukweli katika upendo, tukipendana kama Yesu alivyotufundisha (rej. Yh 15:12).
Baba Mtakatifu aliendelea kusisitiza kuwa, si kweli, kama wengine wanavyofikiri, kwamba matukio ya ulimwengu "yameponyoka" kutoka mikononi mwa Mungu. Maovu mengi yanayotutesa yametungwa na wanadamu. “Wale wanaoharibu watu, wafanyao vita, watakuwaje watakapojitokeza mbele za BWANA? “Kwa nini ulipigana vita hivyo? Kwa nini umeua?” Na watajibu nini? Hebu tufikirie hili. Kwetu sisi pia hatufanyi vita, hatuui, lakini nilifanya hivi, hivi, hivi,... Wakati Bwana atatuambia: “Lakini kwa nini ulifanya hivi? Kwa nini hukuwatendea haki katika hili? Kwa nini ulitumia fedha hizi kwa ubatili wako?” Bwana atatuuliza mambo haya pia. Bwana hutuacha huru, lakini hatuachi peke yetu: ingawa huturekebisha tunapoanguka, haachi kutupenda na, ikiwa tunataka, anatuinua tena, ili tuweze kurudi kwenye njia.
Vijana wa Korea wamepokea Msalaba
Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri aliendelea na kipengele kingne cha tukio la Siku ya vijana Ulimwengu ijayo na kwamba “Mwishoni mwa Ekaristi hii, vijana wa Kireno watakabidhi alama za Siku ya Vijana Duniani kwa Vijana wa Korea: Msalaba na Picha ya Maria Salus Populi Romani. Hii pia ni ishara: mwaliko, kwa sisi sote, kuishi na kuleta Injili katika kila sehemu ya dunia, bila kukoma na bila kukata tamaa, kuinuka baada ya kila anguko na bila kuacha kutumaini, kama Ujumbe wa hii. Siku hii inaongozwa na kauli mbiu:“Wale wanaomtumaini Bwana hutembea bila kuchoka” ( Isa 40:31). “Nyinyi vijana Wakorea mtapokea Msalaba, wa Bwana, Msalaba wa uzima, na ishara ya ushindi, lakini ambayo si peke yake. Mtapokea na mama yenu. Ni Maria ambaye daima anatusindikiza kuelekea kwa Yesu; ni Maria ambaye katika nyakati ngumu yuko karibu na Msalaba wetu ili kutusaidia, kwa sababu Yeye ni Mama, Yeye ni mama yetu. Mfikirie Maria.” Na tukazie mtazamo wetu kwa Yesu, Msalabani wake, na Maria, Mama yetu: hivyo, hata katika magumu, tutapata nguvu ya kusonga mbele, bila kuogopa shutuma, bila kuhitaji maelewano. “kwa heshima ya mtu, kwa uhakika wa kuokoka na kusindikizwa na mama yake, Maria, bila kufanya mapatano, bila kujitengenezea mambo ya kiroho. Utu wenu hauhitaji kutengenezwa. Tusonge mbele,” furaha kuwa kwa ajili ya kila mtu, kuwa katika upendo, na kuwa mashahidi wa ukweli. Na tafadhali, msipoteze furaha. Papa alihitimisha akishukuru kuwa Asante."
Maneno ya Papa kabla ya kukabidhiana msalaba kati ya Ureno na Korea Kusini
Baada ya Misa kabla ya kukabidi msalaba na ishara za Siku ya Vijana, Baba Mtakatifu Francisko aliwalekea Ujumbe kutoka Urena n aule wa Korea ya Kusini kwamba “Napenda kuwasalimu ninyi nyote, vijana mliopo hapa, na vijana kutoka pande zote za dunia, hasa ujumbe kutoka Ureno, ambako Siku ya Vijana Duniani ilifanyika mwaka jana,(2023) na ujumbe kutoka Korea Kusini, ambao utaandaa siku inayofuata huko Seoul mnamo 2027. Muda mfupi ujao vijana wa Kireno watakabidhi alama za WYD - Msalaba na Picha ya Maria Salus Populi Romani (Maria Afya ya Warumi),kwa Vijana wa Korea. Alama hizi zilikabidhiwa kwa vijana na Mtakatifu Yohane Paulo II ili kuzipeleka ulimwenguni kote. Na ninyi, Wakorea wapendwa, sasa ni zamu yenu! Kwa kuubeba Msalaba hadi Asia, mtatangaza upendo wa Kristo kwa kila mtu. Kuweni na ujasiri! Muwe na ujasiri wa kutoa ushuhuda kuhusu tumaini tunalohitajika zaidi leo huu kuliko wakati mwingine wowote. Mahali ambapo alama hizi zitapitia basi uhakika wa upendo usioshindika wa Mungu na udugu kati ya watu ukue. Na kwa waathiriwa wote vijana wa mizozo na vita, Msalaba wa Bwana na picha ya Mtakatifu Maria iwe msaada na faraja." Papa Francisko alihitimisha. Na tendo la kukabidhiana likafuata.