Mafuriko mabaya sana kutokea huko Valenzi nchini Hispania. Mafuriko mabaya sana kutokea huko Valenzi nchini Hispania. 

Papa Francisko:tuombee watu wa Valencia na watu wengine wa Hispania wanaoteseka

Pamoja na salamu nyingi na miito ya Papa Francisko,Dominika tarehe 3 Novemba 2024,wazo lake limegeukia mji wa Hispania ulioharibiwa na dhoruba ya Dana.Ameomba waamini kuhamasisha msingi wa kiroho katika uso wa janga hili:"Nifanye nini kwa Valencia?Hata hivyo idadi ya wahanga imefikia vifo 210 na kuna hatari ya kuenea kwa maambukizi kutokana na kuziba kwa mifereji ya maji taka na ukosefu wa maji ya kunywa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 3 Novemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha watu wanateseka kutoka na dhoruba kali iliypiga huko Valencia nchini Hispania huku akihamaisha watu kujitoa kwa moyo katika kuhamasisha msaada wa hali na mali. Papa amesema “Na tunaendelea kuombea Valencia, na watu wengine wa Uhispania, ambao wanateseka sana katika siku hizi. Papa ameomba kujiuliza “ Je nifanye nini kwa watu wa Valencia? Tafadhali, ninaweza kutoa kitu? Fikirieni juu ya swali hili ...”Papa amehitimisha kwa kuwatakia “wote Dominika njema. Na tafadhali msisahau kuniombea. Kuwa na chakula cha mchana mwemma na kwaheri ya kukuona.

Maafa ni makubwa na waathirika ni wengi

Zaidi ya waru 210 wamekufa, lakini bado kuna wengi waliopotea. Matokeo ya   janga lililoikumba Valencia ulitolewa na  tarehe 2 Novemba 2024 na Waziri Mkuu Pedro Sanchez ambapo  bado yanabaki kuwa ya muda. Waziri Sanchez, katika hotuba yake, kisha alitangaza kuwasili kwa askari na mawakala wengine 10 elfu katika eneo lililoharibiwa na dhoruba  Dana. Kuna wanajeshi 5elfu, na ndio idadi kubwa zaidi ya vikosi vya jeshi kuwahi kufanywa wakati wa amani, Sanchez alibainisha zaidi. Kufikia sasa, watu 4,800 wameokolewa na watu 30,000 wamesaidiwa.

Mabishano dhidi ya rais wa mkoa

Wakati huo huo, mzozo uliendelea juu ya rais wa eneo hilo Carlos Mazón ambaye inadaiwa hakuwatahadharisha idadi ya watu, akikataa dharura hiyo ili, kulingana na vyanzo vya habari, asilazimike kushughulikia hitaji la msaada wa moja kwa moja. Kwa chaguo la kudumisha kiwango cha dharura cha 2 na kutoiinua hadi kiwango cha 3, ile ya maafa, licha ya idadi kubwa ya vifo, ilimaanisha kwamba Mazón hakuchukulia moja kwa moja amri ya shughuli, na hivyo kutekeleza jukumu lolote la kisheria linalowezekana.

Makadirio ya Chama cha Wafanyabiashara

Chama cha Wafanyabiashara cha Valencia kinakadiria kuwa karibu biashara 4,500 zimepata uharibifu, ambapo karibu 1,800 zinaweza kuharibiwa. Manispaa zilizoathiriwa zingekuwa mwenyeji wa zaidi ya 30% ya wakazi wote wa jimbo la Valencia. Na wakati huo huo, maelfu ya watu wanaendelea kufika katika maeneo yaliyoharibiwa kupeleka msaada wao, ni vijana kwa wazee, wajitolea ambao wamefika kutoka nchi nzima kwa njia zao za kufika sehemu zilizotengwa zaidi ambazo bado hazijafikiwa kwa msaada.

Uokoaji wa mwanamke

Hata hivyo, matumaini bado ni makubwa kwamba bado wataweza kuwapata watu wakiwa hai, uokoaji wa tarehe 2 Novemba  wa mwanamke ambaye alinaswa kwa siku tatu kwenye gari lililotelekezwa mwishoni mwa njia ya chini katika moja ya vituo vilivyoathiriwa zaidi na mafuriko iliwapa matumaini zaidi.

Papa baada ya Angelus 3 Novemba 2024
03 November 2024, 14:50