Papa Francisko:tuombee Valencia na Hispania ambao wanateseka na mafuriko

Kabla ya kuanza Katekesi yake Nobemba 2024 Papa Francisko ameweka maua mbele ya picha ya "Virgen de los Desamparados",mtakatifu msimamizi wa jiji la Hispania lililoharibiwa na dhoruba ya Dana.Na mwisho wa Katekesi hiyo ametoa wito mpya wa amani na kumbukumbu bado raia 153 waliouawa kwa risasi barabarani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 6 Novemba 2024 kabla ya Katekesi yake akiwageukia waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu Francisko amesema “Nilitaka kumsalimu Virgen de los Desamparados, Bikira Maria  anaye watunza maskini ambaye ni Msimamizi wa mji wa Valencia, ambao unateseka sana, na pia sehemu nyingine za Hispania, lakini zaidi ya yote huko Valencia, ambayo ni sehemu  ya maji na inateseka. Nilitaka awe hapa, mtakatifu msimamizi wa Valencia. Picha hii ambayo Watu wa Valencia wenyewe walinipatia. Leo hii, kwa namna ya pekee, tunaiombee Valencia na maeneo mengine ya Hispania ambayo yanasumbuliwa na maji.”

Sanamu ya Bikira Maria wa Valencia
Sanamu ya Bikira Maria wa Valencia

Baba Mtakatifu Francisko katika salamu zake mbali mbali hata kwa lugha ya kiitaliano amewakaribisha  mahujaji wote, kwa namna ya pekee washiriki wa kozi iliyohamasishwa na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu, (Santa Croce), waseminari wa Jimbo kuu la Mtakatifu Marko Argentano-Scalea, hija ya Watawa wa Mitume Wadogo wa Ukombozi, kikundi cha sala cha Mondragone, wanariadha wa mbio za marathoni wa Pordenone.

Picha ya makundi
Picha ya makundi

Hatimaye, mawazo yangu yaliwaendea vijana, wagonjwa, wazee na wanandoa wapya. Papa amewahimiza kila mtu kuishi maisha yake ya kila siku kwa uaminifu wa Injili, akiungwa mkono na imani na matumaini.

Papa akisalimiana na wanandoa wapya
Papa akisalimiana na wanandoa wapya

Tusisahau Ukraine,Gaza na Israel

Na tuombe amani. Tusisahau Ukraine inayoteswa, ambayo inateseka sana; tusisahau Gaza na Israel. Juzi raia 153 waliokuwa wakitembea barabarani walipigwa risasi na bunduki. Inasikitisha sana. “ Papa amesema kwa huzuni kweli. “Tusisahau Myanmar. Na tusisahau Valencia au Hispania. Kwa sababu hii, kama nilivyosema, leo Virgen de los Desamparados, Madonna de Desamparados, ambaye ni mtakatifu msimamizi wa Valencia, awaongoze. Kwa njia hiyo Papa amewaaalika wote kusali Salamu Maria kwa  kwa ajili ya Valencia…. Na tunawombea kwa Bwana ili waishi kwa matumaini daima. Papa  ametoa baraka zake kwa wote.

Baada ya katekesi ya Papa
06 November 2024, 11:19