Papa Francisko:ujuzi duni na kutotumia kanuni za usalama huhatarisha usalama barabarani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 25 Novemba 2024 amekutana na wawakilishi wa Shirikisho la Wanapikipiki nchini Italia na kuanza na salamu kwa Rais wao na Shirikisho zima. Kama shirikisho la michezo wana jukumu la kusimamia na kudhibiti pikipiki katika eneo la kitaifa na kuiwakilisha katika kiwango cha kimataifa. Katika kukuza na kulinda shughuli hizi Papa amewahimiza kujitolea kuongeza uelewa wa kuzingatia sheria na Kanuni za Usalama Barabarani.
Kueneza elimu ya usalama barabarani, ambayo pia hutolewa na Sheria zao kupitia kuandaa kozi zitakazofanyika shuleni wanazithamini. Kwa njia hiyo, inatoa fursa ya kuwafanya watoto wafikirie, ambao wanapenda kuwa mabingwa wa pikipiki lakini mara nyingi hawajui hatari. Kiukweli, kuna waathiriwa, wengi wa ajali za barabarani, na vijana wapo wengi! Mara nyingi, ujuzi duni au kushindwa kutumia kanuni za usalama huhatarisha usalama sio wa dereva tu, bali hata pia kwa wengine. Kwa sababu hiyo, wakati uliowekwa kwa mipango ya elimu kwa maana hii ni uwekezaji katika neema ya maisha.
Papa Francisko amewashukuru kwa kile wanachofanya kusaidia na kuelimisha kwa njia hizi! Amewatakia kila la kheri katika shughuli yao na amewabariki wote kutoka ndani ya moyo wake. Pia, amewaomba wamwombee, maana anahitaji maombi, kwa nini? Kwa sababu kazi yake ina kasi sana na Pikipiki yake tayari ni ya zamani na haifanyi kazi vizuri, Papa Francisko alisema kwa matani.