Tumebelee kuombea Ukraine,Nchi za Mashariki na kwingineko duniani. Tumebelee kuombea Ukraine,Nchi za Mashariki na kwingineko duniani.  (ANSA)

Papa Francisko:vita vipigwe marufuku,tuombee nchi zenye vita!

Mwishoni mwa Sala ya Malaika wa Bwana Papa alirudia kuzindua upya wito wa kunyamazisha silaha,kutoa nafasi ya mazungumzo na kushughulikia masuala na sheria na mazungumzo,amesisitiza juu ya Kifungu cha 11 cha Katiba ya Italia na pia alielekeza wazo kwa nchi ya Ukraine,Mashariki ya Kati,Myanmar na Sudan Kusini na kuwaomba kusali kwa ajili ya wakazi wa Valencia nchini Hispania waliokumbwa na kimbunga kikali.

Na Angella Rwezaula - vatican

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 3 Novemba 2024,  akiwageukia waamini na mahujaji wengi sana waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu Franciko alianza na salamu kwamba: “Ninawasalimu ninyi nyote, Warumi na mahujaji kutoka Italia na nchi zingine!

Papa amesalimia kundi la wakarmeli
Papa amesalimia kundi la wakarmeli

Amewasalimu Masista Wamisionari Wakarmeli wa Roho Mtakatifu, wanaoadhimisha miaka ishirini na mitano ya udugu wao wa kilimwengu; Amewasalimu waamini wa Venezia, Pontassieve, Barberino ya Mugello, Empoli na Palermo, na wa Mtakatifu  Maria wa Fornaci huko Roma; pamoja na vijana wa Catanzaro wakiwa na waelimishaji wa parokia zao. Amewasalimu wachangiaji damu wa Coccaglio (Brescia).

Chama cha Wachangia damu kutoka Brescia, Italia
Chama cha Wachangia damu kutoka Brescia, Italia

Papa aidha amewasalimu kikundi cha Dharura ya Kusini mwa Roma kilichojitolea kukumbuka Kifungu cha 11 cha Katiba ya Italia, kinachosema: “Italia inakataa vita kama chombo cha kosa dhidi ya uhuru wa watu wengine na kama njia ya kusuluhisha mizozo ya kimataifa". Papa ameomba “Kumbuka makala hii. Endeleeni mbele!”Na kanuni hii inaweza kutekelezwe duniani kote: vita vipigwe marufuku na masuala yashughulikiwe kupitia sheria na mazungumzo. Silaha zinyamazishwe na kutoa nafasi kwa mazungumzo.” Amesema Papa Papa akiendelea Papa amesema “Tunawaombea wanaoteswa Ukraine, Palestina, Israel, Myanmar, Sudan Kusini.

Papa baada ya Angelus
03 November 2024, 14:27