Tafuta

Papa Francisko. Papa Francisko.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:Washairi wapendwa tusaidie kuota ndoto

Tunachapisha barua aliyoandika Papa Francisko katika kitabu:“Antolojia ya shairi la kidini"kilichoandikwa na Davide Brullo,Antonio Spadaro na Nicola Crocetti,ambacho kitakuwa katika duka la vitabu Jumanne 12 Novemba 2024.Katika barua hiyo Papa anabainisha kuwa:Kiukweli ushairi hauzungumzii ukweli kuanzia kanuni za kufikirika bali kusikiliza ukweli wenyewe:kazi upendo,kifo na mambo ya maisha.

Papa Francisko

Washairi wapendwa, ninajua mna njaa ya maana, na kwa sababu hiyo pia mnatafakari jinsi imani inavyohoji maisha. “Maana” hii haiwezi kupunguzwa kwa dhana, hapana. Ni maana ya jumla ambayo inachukua mashairi, ishara na hisia. Maana ya kweli sio ile ya kamusi: hiyo ndiyo maana ya neno, na neno ni chombo cha kila kitu kilicho ndani yetu. Nimewapenda washairi na waandishi wengi maishani mwangu, ambao kati yao ninamkumbuka sana Dante, Dostoevsky na wengine. Pia sina budi kuwashukuru wanafunzi wangu katika (Colegio de la Inmaculada Concepción)-Chuo cha Moyo safi  huko Mtakatifu Fe, ambao nilishirikishana nao usomaji wangu nilipokuwa mdogo na kufundisha fasihi. Maneno ya waandishi yalinisaidia kujielewa, ulimwengu, watu wangu; lakini pia kuimarisha moyo wa mwanadamu, maisha yangu binafsi ya imani, na hata kazi yangu ya uchungaji, hata sasa katika huduma hii.

Kwa hiyo, neno la fasihi ni kama mwiba ndani ya moyo unaokuchochea kutafakari na kukuweka kwenye njia. Ushairi umefunguliwa, unakutupa mahali pengine. Kwa kuzingatia uzoefu huu wa kibinafsi, leo ningependa kushiriki nanyi baadhi ya mambo ya kuzingatia kuhusu umuhimu wa huduma yenu. Ningependa kueleza ya kwanza kama hii: nyinyi ni macho yanayotazama na kuota. Ninyi sio tu kuangalia, lakini pia ndoto. Mtu ambaye amepoteza uwezo wa kuota hukosa mashairi, na maisha bila mashairi hayafanyi kazi. Sisi wanadamu tunatamani ulimwengu mpya ambao pengine hatutauona kikamilifu kwa macho yetu, hata hivyo tunautamani, tunautafuta, tunauota. Mwandishi wa Amerika ya Kusini alisema kwamba tuna macho mawili: moja la mwili na lingine la kioo. La  mwili, tunatazama kile tunachokiona, na la kioo tunatazama kile tunachoota. Masikini tukiacha kuota, masikini sisi! Msanii ni mtu anayetazama kwa macho yake na wakati huo huo huota, anaona kwa undani zaidi, anatabiri, anatangaza njia tofauti ya kuona na kuelewa mambo yaliyo mbele ya macho yetu. Kwa kweli, ushairi hauzungumzii ukweli kuanzia kanuni za kufikirika, bali kwa kusikiliza ukweli wenyewe: kazi, upendo, kifo, na mambo yote madogo madogo yanayojaza maisha. Kwa kumnukuu Paul Claudel anaandika: “Yesu  ni jicho la kusikiliza.”

Sanaa ni dawa dhidi ya mawazo ya kuhesabu na usawa; ni changamoto kwa mawazo yetu, kwa njia yetu ya kuona na kuelewa mambo. Na kwa maana hii Injili yenyewe ni changamoto ya kisanaa. Inayo malipo hayo ya “mapinduzi,” ambayo mnayajua vizuri, na ninatoa shukrani kwa fikra zenu kwa neno linalopinga, kupiga simu, kupiga kelele. Kanisa pia linahitaji fikra zenu, kwa sababu linahitaji kupinga, kuita na kupiga kelele. Hata hivyo, ningependa kusema jambo la pili: ninyi pia ni sauti ya wasiwasi wa kibinadamu. Mara nyingi wasiwasi huzikwa ndani ya moyo mnajua vizuri kwamba msukumo wa kisanii haufariji tu, bali pia unasumbua, kwa sababu unaonesha ukweli mzuri wa maisha na wale wa kutisha. Sanaa ni uwanja wenye rutuba ambamo “upinzani maarufu  wa ukweli - kama Romano Guardini alivyowaita - huoneshwa, ambao kila wakati unahitaji lugha ya ubunifu na isiyo ngumu, yenye uwezo wa kuwasilisha ujumbe na maono yenye nguvu. Kwa mfano, hebu tufikirie wakati Dostoevsky katika andiko la Ndugu Karamazov, anaelezea mtoto mdogo, mwana wa mtumishi, ambaye halirusha jiwe na kugonga mguu wa mbwa mmoja wa bwana wake. Kisha mmiliki aliagiza mbwa wote kumshambulia mtoto huyo. Alikimbia na kujaribu kujiokoa kutokana na hasira ya kundi hilo, lakini aliishia kupasuliwa vipande vipande chini ya mtazamo wa kuridhika wa jenerali na mtazamo mahangaiko ya mama yake. Sehemu hii ina nguvu kubwa ya kisanii na kisiasa: inazungumza juu ya ukweli wa jana na leo, juu ya vita, migogoro ya kijamii, na ubinafsi wetu. 

Kwa kutaja kifungu kimoja tu cha kishairi kinachotupatia changamoto. Na sirejei ukosoaji wa kijamii katika wimbo huo tu. Ninazungumza juu ya mvutano wa roho, ugumu wa maamuzi, na hali inayopingana ya uwepo. Kuna mambo katika maisha ambayo, wakati mwingine, hatuwezi hata kuelewa au ambayo hatuwezi kupata maneno sahihi: hii ni ardhi yenu yenye rutuba, uwanja wenu wa hatua. Na hapa ndipo pia mahali ambapo mtu hupitia uzoefu wa Mungu kila wakati huwezi kuuchukua, unausikia na unakwenda zaidi; daima hufurika, uzoefu wa Mungu, kama beseni ambapo maji humwagika daima na baada ya muda, hujaa na maji hufurika. Hili ndilo ningependa kuwaomba leo pia: kwenda zaidi ya mipaka iliyofungwa na iliyoainishwa, kuwa wabunifu, bila kudhibiti wasiwasi wenu na wa wanadamu. Ninaogopa mchakato huu wa kufungwa kwa sababu unaondoa ubunifu, unaondoa ushairi. Kwa neno la ushairi, kukusanya shauku zisizo na utulivu ambazo huishi ndani ya moyo wa mwanadamu, ili zisipoe na zisitoke.

Kazi hii inamruhusu Roho kutenda, kuunda maelewano ndani ya mivutano na migongano ya maisha ya mwanadamu, kuweka moto wa shauku  nzuri na kuchangia ukuaji wa uzuri katika aina zake zote, uzuri ambao unaoneshwa kwa usahihi kupitia utajiri wa sanaa. Hii ni kazi yenu kama washairi: kutoa uhai, kutoa mwili, kutoa maneno kwa kila kitu ambacho wanadamu hupata, kuhisi, kuota, kuteseka, kuunda maelewano na uzuri. Ni kazi ambayo inaweza pia kutusaidia kumwelewa Mungu vyema kama “mshairi” mkuu wa wanadamu. Je, watawakosoa? Sawa, kubeba mzigo mkubwa wa ukosoaji, huku pia mkijaribu kujifunza kutokana  na ukosoaji. Lakini bado msiache kuwa wa asili, wabunifu. Msipoteze maajabu ya kuwa hai. Kwa hiyo: macho ambayo huota, sauti za wasiwasi wa kibinadamu; na kwa hivyo ninyi pia mna jukumu kubwa. Na ni nini? Hili ni jambo la tatu ambalo ningependa kuwaambia: ninyi ni miongoni mwa wale wanaounda mawazo yetu. Kazi yenu  ina matokeo juu ya mawazo ya kiroho ya watu wa wakati wetu. Na leo tunahitaji fikra ya lugha mpya, ya historia na picha zenye nguvu. Mimi pia ninahisi, ninakiri, hitaji la washairi wenye uwezo wa kupaza sauti ujumbe wa kiinjili kwa ulimwengu, kutufanya tumuone Yesu, kutufanya tumguse, kutufanya tujisikie karibu naye mara moja, kumtoa kwetu kama uhalisi ulio hai, na kufanya tufahamu uzuri wa ahadi yake.

Kazi yenu inaweza kutusaidia kuponya mawazo yetu kutoka katika kila kitu kinachoficha uso wake au, mbaya zaidi, kutoka kwa kila kitu kinachotaka kuidhibiti. Kutunza uso wa Kristo, kuuweka kwenye fremu na kuutundika ukutani, kunamaanisha kuharibu sanamu yake. Ahadi yake badala yake inasaidia mawazo yetu: inatusaidia kufikiria maisha yetu, historia yetu na maisha yetu ya baadaye kwa njia mpya. Na hapa ninarudi kukumbuka kazi nyingine bora ya Dostoevsky, ndogo lakini ambayo ina mambo haya yote ndani: Kumbukumbu kutoka chini ya ardhi. Mle ndani kuna ukuu wote wa ubinadamu na maumivu yote ya wanadamu, taabu zote pamoja. Hii ndiyo njia. Washairi wapendwa, asante kwa huduma yenu. Endelea kuota, kuwa na wasiwasi, kufikiria maneno na maono ambayo hutusaidia kuelewa fumbo la maisha ya mwanadamu na kuelekeza jamii zetu kuelekea uzuri na udugu wa Ulimwengu wote. Tusaidie kufungua fikira zetu ili ziweze kupita mipaka finyu ya nafsi, na kufungua ukweli kwa ujumla, katika wingi wa sura zake: hivyo zitapatikana kujifungua kwa fumbo takatifu la Mungu, kwenda bila kuchoka, kwa ubunifu na ujasiri!

Barua ya Papa kwa watunzi wa mashairi
10 November 2024, 16:23