Papa Fransisko:Tazama mimi hapa iwe tabia ya kidini mbele ya Mungu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 13 Novemba 2024, ameendeleza mzunguko wa katekesi kuhusu: “Roho Mtakatifu na Mchumba. Roho Mtakatifu kiongozi wa watu wa Mungu kukutana na Yesu Tumaini”, ambapo kwa kuongozwa na Barua ya l3 iliyoandikwa kwa Roho wa Mungu aliye hai: Maria na Roho Mtakatifu , somo lililosomwa ni kutoka (Mdo 1,12-14) ambapo “kulikuwa na Petro na Yohane, Yakobo na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda mwana wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu na kushikamana katika kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria mama yake Yesu, na ndugu zake.”
Baba Mtakatifu Francisko akianza alisema: “Miongoni mwa njia mbalimbali ambazo Roho Mtakatifu hutekeleza kazi yake ya utakatifu ndani ya Kanisa - Neno la Mungu, Sakramenti, sala - kuna moja ya kipekee ambayo ni ucha Mungu wa Maria. Katika mapokeo ya Kikatoliki kuna kauli mbiu au msemo huu: Leo wanataalimungu Wakatoliki wanaelekea kutoa maana mpya na sahihi zaidi kwa msemo wa kimapokeo “Ad Iesum per Mariam”, yaani, “kwa Yesu kupitia kwa Maria.” “Mama yetu anatuonesha Yesu Anatufungulia milango, daima! Mama ndiye mama anayetuongoza kwa mkono kuelekea kwa Yesu, Mama huelekeza kwa Yesu. Mpatanishi wa kweli na wa pekee kati yetu na Kristo, aliyeoneshwa hivyo na Yesu mwenyewe, ni Roho Mtakatifu. Maria ni mojawapo wa njia ambazo Roho Mtakatifu hutumia kutuleta kwa Yesu. Mtakatifu Paulo anafafanua jumuiya ya Kikristo kuwa ni “barua ya Kristo iliyoandikwa nasi, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, bali katika vibao vya mioyo ya wanadamu” (2Kor 3:3).
Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa “Maria, kama mfuasi wa kwanza na sura ya Kanisa, pia ni barua iliyoandikwa na Roho wa Mungu aliye hai. Kwa sababu hiyo, anaweza “kujulikana na kusomwa na watu wote” (2Kor 3:2), hata na wale wasiojua kusoma vitabu vya taalimungu, na wale “wadogo” ambao Yesu anawaambia kwamba siri za Ufalme zinafichuliwa, zimefichwa kwa wenye hekima (rej. Mt 11:25). Kwa kusema "mimi hapa" wakati Maria alikubali na kumwambia malaika: "Tazama, mapenzi ya Bwana yafanyike" na kukubali kuwa mama wa Yesu -, fiat – mimi hapa" kwa tangazo la malaika - Origen alitoa maoni ni kana kwamba Maria alimwambia Mungu: "Mimi hapa, mimi ni kibao cha kuandikwa: Mwandishi na aandike anachotaka, anifanyie atakalo Bwana wa wote." Wakati huo, ilikuwa ni desturi kuandika juu ya vidonge vya wax; leo huu tungesema kwamba Maria anajitolea kama ukurasa mtupu ambao Bwana anaweza kuandika chochote anachotaka,” Papa Francisko amesisitiza.
“Ndiyo ya Maria kwa Malaika - aliandika mfafanuzi mashuhuri - inawakilisha "kilele cha tabia zote za kidini mbele ya Mungu, kwa kuwa anaonesha, kwa njia ya juu kabisa, ya uwepo wa hali nzuri pamoja na utayari wa vitendo, utupu wa ndani kabisa unaoambatana na utimilifu mkubwa zaidi." Hapa, basi, ni jinsi gani Mama wa Mungu ni chombo cha Roho Mtakatifu katika kazi yake ya utakaso. Katikati ya mafuriko yasiyoisha ya maneno yaliyosemwa na kuandikwa juu ya Mungu, Kanisa na utakatifu ambao ni wachache sana, ikiwa wapo, wanaweza kusoma na kuelewa kikamilifu unapendekeza maneno mawili tu ambayo kila mtu, hata rahisi zaidi, anaweza kuyatamka, kwa kila tukio: "tazama Mimi hapa" na "fiat".
Maria ndiye aliyesema "ndiyo tazama mimi" kwa Bwana na kwa mfano wake na maombezi yake yanatusukuma kusema "ndiyo" yetu kwake pia, kila wakati tunajikuta tunakabiliwa na utii wa kutekeleza au mtihani wa kushinda. Katika kila zama za historia yake, lakini hasa wakati huu, Kanisa linajikuta katika hali ambayo jumuiya ya Kikristo ilikuwa wakati wa baada ya Kupaa kwa Yesu mbinguni. Papa Francisko amesisitiza kuwa “Ni lazima ahubiri Injili kwa watu wote, lakini anasubiri “uwezo utokao juu” uweze kufanya hivyo. Na tusisahau kwamba wakati huo, tunaposoma katika Matendo ya Mitume, wanafunzi walikuwa wamekusanyika karibu na "Maria, mama yake Yesu" (Mndo 1:14).”
Ni kweli kwamba pia kulikuwa na wanawake wengine pamoja naye kwenye ukumbi, lakini uwepo wake ni tofauti na wa kipekee kati ya wote. Kati yake na Roho Mtakatifu kuna kifungo cha pekee na kisichoweza kuharibika milele ambacho ni mtu halisi wa Kristo, "aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na Bikira Maria", tunaosali katika sala ya Nasadiki. Mwinjili Luka anaakisi kwa makusudi mawasiliano kati ya ujio wa Roho Mtakatifu juu ya Maria wakati wa Matamshi na kuja kwake kwa wanafunzi siku ya Pentekoste, akitumia baadhi ya maneno yanayofanana katika matukio yote mawili. Mtakatifu Fransis wa Assisi, katika moja ya sala zake, anamsalimia Bikira kuwa ni “binti na mjakazi wa Mfalme Mkuu Baba wa mbinguni, mama wa Bwana Mtakatifu Yesu Kristo, bibi arusi wa Roho Mtakatifu.”
Kwa njia hiyo Papa Francisko amerudia kukazia kwamba kuwa Binti wa Baba, Mama wa Mwana, Bibi arusi wa Roho Mtakatifu! Ni Uhusiano wa kipekee wa Maria na Utatu haungeweza kuoneshwa kwa maneno rahisi zaidi. Kama picha zote, hii moja ya "bibi-arusi wa Roho Mtakatifu" haipaswi kufanywa kuwa kamili, lakini ichukuliwe kwa kiasi cha ukweli uliomo, na ni ukweli mzuri sana. Yeye ni bibi-arusi, lakini yeye hata kabla ya hapo,ni mfuasi wa Roho Mtakatifu. MwanaMke na mwanafunzi. Tunajifunza kutoka kwake kuwa wanyenyekevu kwa maongozi ya Roho, hasa anapopendekeza kwamba “tuinuke upesi” na kwenda kumsaidia mtu anayetuhitaji, kama alivyofanya mara baada ya Malaika kumwacha (rej. Luka 1:39). Papa amehitimisha kwa kushukuru.