Papa:Katika Jubilei 2025 kutakuwa na Mkutano kuhusu haki za watoto mjini Vatican!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 20 Novemba 2024, wakati wa salamu zake kwa mahujaji wa lugha ya kiitaliano, Baba Mtakatifu alikuwa na mengi ya kueleza. Awali ya yote Papa alisema kuwa: “ Katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Watoto na Vijana inayoadhimishwa leo(20 Novemba 2024), ninapenda kutangaza kwamba tarehe 3 Februari 2025 kutakuwa na Mkutano wa Dunia wa Haki za Mtoto utakaofanyika hapa Vatican, kwa kuongoza na mada: Tuwapende na kuwalinda ", kwa ushiriki wa wataalam, na mashuhuri kutoka nchi tofauti. Itakuwa fursa ya kutambua njia mpya za kusaidia na kulinda mamilioni ya watoto ambao bado hawana haki wanaoishi katika mazingira hatarishi, wananyonywa na kunyanyaswa na wanapata matokeo makubwa ya vita.” Baba Mtakatifu Francisko akiendelea alisema: “Kuna kundi la watoto wanaoandaa Siku hii, asante kwa wote mnaofanya hivyo. Na inaweza kuonekana kwamba kuna ujasiri ambao ..., wote wanakuja ah, kila mtu anakuja, eh! Watoto ndivyo walivyo, mmoja akianza halafu wanakuja wote! Hebu tuwasalimie watoto! Wanataka kukushukuru hapo juu... Asante kwenu!”
Wenyeheri Carlo Acutis na Piergiorgio Frassati
“Ninataka kusema kwamba mwaka ujao katika Siku ya Watoto na Barubaru, nitamtangaza Mwenyeheri Carlo Acutis,kuwa Mtakatifu, kwamba Siku ya Vijana, mwaka ujao, nitamtangaza Mwenyeheri Giorgio Frassati kuwa Mtakatifu.”
Siku 1000 za vita Ukraine
Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza kuwa “Jana iliadhimishwa siku elfu moja tangu uvamizi wa Ukraine, kumbukumbu ya kutisha kwa waathiriwa na uharibifu uliosababisha. Lakini wakati huo huo maafa ya aibu kwa wanadamu wote. Hata hivyo, hii lazima isituzuie kubaki pamoja na watu wa Ukraine wanaoteswa, kuanzia na kuomba amani na kufanya kazi ili silaha zitoe nafasi ya mazungumzo na migogoro ya kukutana. Juzi nilipokea barua kutoka kwa mvulana wa chuo kikuu cha Ukraine na inasema hivi: “Baba, Jumatano utakapokumbuka nchi yangu na kupata fursa ya kuongea na ulimwengu mzima katika siku ya elfu moja ya vita hivi vya kutisha, inakusihi, usiseme tu juu ya mateso yetu, lakini pia ushuhudie imani yetu: hata ikiwa si kamilifu, thamani yake haipunguki, inachora maumivu ya picha ya Kristo Mfufuka. Kumekuwa na vifo vingi sana katika maisha yangu siku hizi. Kuishi katika jiji ambalo kombora linaua na kujeruhi makumi ya raia, kushuhudia machozi mengi ni ngumu. Ninatamani kutoroka, ninatamani kurudi kuwa mtoto wa kukumbatiwa na mama yangu, ninatamani sana kukaa kimya na upendo lakini namshukuru Mungu kwani kupitia maumivu haya, ninajifunza kupenda zaidi. Huzuni sio tu njia ya hasira na kukata tamaa; ikiwa ni msingi wa imani yeye ni mwalimu mzuri wa upendo. Baba, ikiwa maumivu yanaumiza inamaanisha kuwa unapenda, kwa hivyo unapozungumza juu ya uchungu wetu, unapokumbuka siku elfu za mateso, unakumbuka pia siku elfu za upendo kwa sababu upendo tu, imani na tumaini hutoa maana ya kweli kwa majeraha .”Ndivyo aliandika kijana huyu wa Chuo kikuu cha Kiukraine, Papa Francisko alisema.
Akiendelea Papa alisema: “Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Hasa, ninawasalimu washiriki katika mkutano wa kimataifa uliohamaishwa na Familia ya Augustiniani, Mfuko wa Muziki na Sanaa Takatifu waliojitolea wa Ushuhudua wa watu wa kujitolea wa Italia.” Ninawakaribisha kwa uchangamfu wanafunzi wa Shule ya Poli ya Velletri, ambao wamepata uthibitisho na ninawatia moyo katika safari yao ya imani katika huduma ya jumuiya. Asante kwa ushuhuda wenu.” Hatimaye, mawazo yake Papa Francisko yamewaendea vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa wapya. Domika ijayo, (24 Novemba 2024) wakati wa kuhitimisha kipindi cha Mwaka wa kawaida, tutasherehekea ukuu wa Kristo, mfalme wa Ulimwengu. Ninawaalika kila mtu kutambua uwepo wa Bwana katika maisha yake, ili kushiriki katika ujenzi wa Ufalme wake wa upendo na amani.
Siku ya Sala kwa Watawa wa Ndani
Papa Francisko hakuishia hapo bali alisema "Kesho yaani (tarehe 21 Novemba 2024) ni kumbukumbu ya kiliturujia ya kuwekwa Hekaluni, Bikira Maria, sanjari na Siku ya Sala ya Mashirik ya Kitawa ya ndani (Pro Orantibus)." Baba Mtakatifu Francisko aliwakumbuka watawa wa Ndani walioitwa na Bwana kwa maisha ya kutafakari, na kwamba “tunawahakikishia ukaribu wetu. Nyumba za watawa zilizofungwa zisikose msaada unaohitajika wa kiroho na kimwili kutoka kwa jumuiya ya kikanisa. Baraka yangu kwenu nyote!”