Papa:Katika Msalaba wa Kristo kuna upendo wote wa Mungu&huruma yake kuu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 14 Novemba 2024, amekutana na Washiriki wa Kongamano lililoandaliwa na Baraza la kipapa la Kuwatangaza Watakatifu kuanzia tarehe 11-13 Novemba, katika Chuo Kikuu cha Baba wa Kanisa Agostino, Jijini Roma. Katika hotuba yake amemsalimia KardinaliMarcello Semeraro pamoja na Wakuu wengine wa Vatican, Viongozi, Washauri, na wote walioshiriki Kongamano kuhusu kaulimbiu ya kifo cha imani na utoaji wa maisha. Baba Mtakatifu alisema “Ilikuwa na kama Neno lake la kuongoza lile la Yesu katika Injili ya Yohane: “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yh 15:13). Kwa njia hiyo akiongeza alisema: “Na kumtangaza mfiadini kuwa mwenyeheri huhitaji muujiza. Kuuawa kwa imani kunatosha ... Akiendelea alisema “Na huku kutoa maisha kwa ajili ya marafiki zake ni Neno ambalo daima hutia faraja na matumaini. Kwa hakika, katika jioni ya Karamu kuu ya Mwisho Bwana alizungumza juu ya zawadi yake mwenyewe ambayo ingekamilika msalabani.
Kwa hiyo Papa amesisitiza kuwa “Upendo pekee ndio unaoweza kueleza msalaba: upendo mkubwa sana unaochukua kila dhambi na kuisamehe, unaingia katika mateso yetu na kutupatia nguvu ya kuubeba, pia unaingia katika kifo ili kukishinda na kutuokoa. Katika Msalaba wa Kristo kuna upendo wote wa Mungu, kuna huruma yake kuu. Kuwa watakatifu hakuhitaji tu juhudi za kibinadamu au kujitolea kibinafsi kwa dsadaka na kujikana. Kwanza kabisa ni lazima tujiruhusu sisi wenyewe kubadilishwa na nguvu ya upendo wa Mungu, ambao ni mkuu kuliko sisi na kutufanya tuwe na uwezo wa kupenda hata zaidi ya kile tulichofikiri tunaweza kufanya. Si kwa bahati kwamba Vatican II, kuhusu wito wa utakatifu wa ulimwengu mzima, inazungumza juu ya "utimilifu wa maisha ya Kikristo" na "ukamilifu wa upendo", wenye uwezo wa kukuza "katika jamii ya kidunia yenyewe kiwango cha maisha cha kibinadamu" (rej.Lumen gentium, 40).
Huduma ya Kanisa yenye thamani
Mtazamo huu pia unaakisi kazi yao kwa ajili ya mambo ya watakatifu, huduma ya thamani ambayo Kanisa hutoa, ili ishara ya utakatifu ulioishi na wa sasa usishindwe kamwe. Wakati wa Mkutano walitafakari juu ya aina mbili za utakatifu uliotangazwa kuwa mtakatifu: ule wa kifo cha kishahidi na ule wa kutoa maisha. Tangu nyakati za kale, waamini katika Yesu wamewaheshimu sana wale ambao walilipa kibinafsi, maisha yao wenyewe, kwa upendo wao kwa Kristo na Kanisa. Walifanya makaburi yao kuwa mahali pa ibada na sala. Walikuwa pamoja, siku ya kuzaliwa kwao mbinguni, ili kuimarisha vifungo vya udugu ambao katika Kristo Mfufuka unavuka mipaka ya kifo, hata kama ni damu na uchungu. Katika mfiadini tunapata sifa za mfuasi mkamilifu, aliyemwiga Kristo kwa kujikana mwenyewe na kuchukua msalaba wake na, akibadilishwa kwa upendo wake, alionesha kila mtu uwezo wa kuokoa wa Msalaba wake.
Baba Mtakatifu Francisko alisema kuwa ninaijiwa akilini nq "Kuuawa kishahidi, huko Libya wa Kiorthodox waliokufa wakisema: "Yesu". "Lakini hao walikuwa Waorthodox!" Walikuwa Wakristo. Wao ni wafiadini na Kanisa linawaheshimu kama wafiadini wenyewe... Pamoja na kifo cha imani kuna usawa. Vile vile ilitokea Uganda kwa wafiadini wa Kianglikani. Wao ni wafiadini! Na Kanisa linawachukua kama wafia imani.” Katika muktadha mchakato wa kuwatangaza watakatifu, hisia ya pamoja ya Kanisa imefafanua mambo matatu ya msingi ya kifodini ambayo daima yanabaki kuwa halali. Mfiadini ni Mkristo ambaye - kwanza - ili asiikane imani yake, akijua anapatwa na kifo cha kikatili na cha mapema. “Hata Mkristo ambaye hajabatizwa, ambaye ni Mkristo moyoni, anamkiri Yesu Kristo kwa Ubatizo wa damu.”
Mara nyingi ukristo unateswa
Pili: mauaji hayo yanafanywa na mtesaji, yanayosukumwa na chuki dhidi ya imani au wema mwingine unaohusishwa nayo; na tatu: mwathirika anapata mtazamo usiotarajiwa wa upendo, uvumilivu, upole, kwa kuiga Yesu aliyesulubiwa. Ni mabadiliko gani, katika enzi tofauti, sio dhana ya kifo cha kishahidi, lakini njia madhubuti ambazo, katika muktadha maalum wa kihistoria, hufanyika. Hata leo, katika sehemu nyingi za ulimwengu, kuna wafiadini wengi wanaotoa maisha yao kwa ajili ya Kristo. Mara nyingi Ukristo unateswa kwa sababu, ukisukumwa na imani yake kwa Mungu, unatetea haki, ukweli, amani na utu wa watu. Hii ina maana, kwa wale wanaosoma matukio mbalimbali ya kifo cha kishahidi, kwamba - kama Papa Pio XII alivyofundisha - "wakati fulani uhakika wa maadili hautokani isipokuwa na wingi wa dalili na ushahidi ambao, ukichukuliwa mmoja mmoja, hauna uwezo wa kuthibitisha uhakika wa kweli; na zikijumlishwa tu haziruhusu shaka yoyote ifaayo kutokea kwa mtu mwenye maamuzi sahihi” (Hotuba kwa Mahakama ya kitume ya Roma, 1 Oktoba 1942). Ni maelewano ya maarifa.
Mashahidi wa imani katika mtazamo wa mwaka Mtakatifu
Baba Mtakatifu amesema kuwa Katika Hati ya kutangaza Jubilei ijayo, alifafanua kuhusu wafiadini kuwa ushuhuda wa matumaini wenye kusadikisha zaidi. Hii ndiyo sababu, ndani ya Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu Papa alitaka kuanzisha Tume ya Wafiadini Wapya - Mashahidi wa Imani, kwa mtazamo wa Mwaka Mtakatifu ambao unatarajiwa na kwamba tofauti na mjadala wa sababu za kifodini, ungekusanya kumbukumbu za wale ambao, hata ndani ya madhehebu mengine ya Kikristo, waliweza kuacha maisha yao ili wasimsaliti Bwana. Na kuna wengi, wengi wa madhehebu mengine ambao ni wafiadini. Uzoefu wa sababu za watakatifu na ulinganisho unaoendelea na uzoefu halisi wa waamini uliniongoza, tarehe 11 Julai 2017, kutia sahihi ya motu proprio "Maiorem hac dilectionem", ambayo Papa amesema “nilikusudia kueleza akili ya kawaida ya Watu wa Mungu waaminifu kuhusu ushuhuda wa utakatifu wa wale ambao, wakihuishwa na upendo wa Kristo, walijitolea maisha yao kwa hiari, wakikubali kifo fulani na cha muda mfupi.”
Uhusiano kati ya kutoa uhani na kifodini
Kwa kuwa lilikuwa ni suala la kufafanua njia mpya ya Mchakato wa kutangazwa kuwa mwenyeheri na kutangazwa kuwa mtakatifu, Papa amebainisha alivyogundua kwamba ilibidi kuwe na uhusiano kati ya kutoa uhai na kifodini. Kwamba Mtumishi wa Mungu alikuwa ametumia wema wa Kikristo angalau kwa kiwango cha kawaida na kwamba, hasa baada ya kifo chake, alizungukwa na sifa ya utakatifu na umaarufu na ishara. Kinachotofautisha utoaji wa uzima, ambamo sura ya mtesaji inakosekana, ni kuwepo kwa hali ya nje, inayoweza kupimwa kimaadili, ambamo mfuasi wa Kristo amejiweka huru na ambayo inaongoza kwenye kifo. Hata katika ushuhuda wa ajabu wa aina hii ya utakatifu, uzuri wa maisha ya Kikristo unang'aa, ambao unajua jinsi ya kujitoa kama zawadi bila kipimo, kama Yesu msalabani. Kwa kuhitimisha, Papa Fancisko aliwashukuru na kuwatia moyo ili waendeleze kazi yao kwa ajili ya watakatifu kwa shauku, na kwa ukarimu. Amewakabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria na mashahidi wote wa Kristo, ambao majina yao katika kitabu cha uzima. Aliwabariki kutoka ndani ya moyo wake na tafadhali aliomba wamwombee.