Papa:kusindikiza Italia kwenye njia ya umoja ili kushinda mateso
Na Angella Rwezaula–Vatican.
Mbele ya wajumbe elfu moja na maaskofu waliokusanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta jijini Roma, lile lile ambalo mnamo mwaka 1959 Papa Yohana XXIII alitangaza Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ndmi wamekusanyika katika kusanyiko la kwanza la kisinodi la Makanisa yote nchini Italia, ambao ulifunguliwa kuanzia tarehe 15 hadi 17 Novemba 2024 kwa kuongozwa na Kardinali Matteo Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia,(CEI) na ambaye alitoa utangulizi wa kikao cha ufunguzi kwa kusoma ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko ulioandaliwa kwa ajili ya hatua hii ya "awamu ya kinabii. Hii ni sehemu ya mwisho ya Njia ya Sinodi ya kitaifa ya miaka mitatu ambayo inajumuisha ulinganisho wa (maandishi yaliyokusanya matokeo yaliyopatikana hadi sasa na kupendekeza mipango mingine ya vitendo) na utayarishaji wa Zana ya Kazi, kwa kuzingatia mkutano wa pili uliopangwa, ten jijini Roma, kuanzia tarehe 31 Machi hadi tarehe 4 Aprili 2025.
Msiogope
Askofu wa Roma alikumbusha mkutano wa Mei uliopita ambapo ishara tatu zilitolewa: kuendelea kutembea, kuwa Kanisa pamoja na kuwa Kanisa lililo wazi. Kisha alisisitiza kuwa Muhtasari unaokusanywa na Makanisa mahalia ni ushuhuda wa uchangamfu unaooneshwa katika safari, katika kukuza kwa ujumla na kwa mtindo wa uwazi. Ni simulizi ambazo Roho Mtakatifu alitenda, akionesha vipimo vya kipaumbele vya kuanzisha upya baadhi ya michakato, kufanya uchaguzi wa ujasiri, kurudi kutangaza unabii wa Injili, kuwa wanafunzi wa kimisionari. Kwa njia hiyo aliwahimiza wasiogope kuinua matanga yao kwa upepo wa Roho!
Kufanya kazi kwa ajili ya uchaguzi na maamuzi ya kiinjili
Papa anarejea tabia ya nabii anayeishi kwa wakati na mtazamo wa imani unaoangazwa na Neno la Mungu na alikumbusha tena jukumu muhimu la Roho Mtakatifu ambaye anaweka nuru, kuelekeza na kufanya mazungumzo kuwa na matunda. Kwa hiyo ni suala la kutafsiri kile ambacho kimekusanywa katika miaka ya hivi karibuni katika uchaguzi na maamuzi ya kiinjili. Na hii inafanywa kwa unyenyekevu wa Roho, Papa aliwaeleza. Kutenda katika ngazi ya kisinodi Papa alifafanua kuwa “kunamaanisha kuyaweka Makanisa katika hali ya kuweza kutekeleza vyema ahadi yao kwa nchi kwa kuiga mtindo wa Yesu aliyejua kuelewa mateso na matarajio ya umati wa watu, nyenzo zao na mahitaji ya kiroho.” Papa aliiweka kazi yao chini ya baraka ya Maria na kuwaalika kwamba “Nawasihi sana Wachungaji mundelee kuisindikiza safari hii kwa ubaba na wema, kwa kuomba msaada wa Mungu kwa kile kitakachoamuliwa.” Kwa kuzingatia historia ya Mikutano ya kikanisa iliyowekwa alama ya njia ya Kanisa nchini Italia katika miongo kadhaa baada ya Mtaguso wa II wa Vatican, alisema kuwa “wataweza kuongoza jumuiya katika njia ya ushirika, ushiriki na utume,”Kama kauli mbiu ya Sinodi.