Tafuta

Barua ya Papa Francisko kuhusu kupyaishwa kwa somo la historia ya Kanisa imechapishwa. Barua ya Papa Francisko kuhusu kupyaishwa kwa somo la historia ya Kanisa imechapishwa. 

Papa Francisko:kusoma historia na kumbukumbu za siku zilizopita ili kujenga mustakabali wa kidugu

Barua ya Papa kuhusu kupyaishwa somo la historia ya Kanisa ili kuwasaidia mapadre:“kutafsiri vyema ukweli wa kijamii.”Papa anaomba kuwa waangalifu kwa wale wanaopendekeza kupuuza yaliyopita.Hivi ndivyo itikadi za rangi tofauti zinavyofanya kazi,huharibu kila kitu ambacho ni tofauti.Ninaonya msilazimishwe kuganda na upuuzi bali kujibu vizuizi vya kupooza,kiutamadun,utafiti,maarifa na kushirikisha.

Vatican News

Historia ya Kanisa inapaswa kupendwa na kujifunza kama mama, kama ilivyo. Historia hii, ambayo mara nyingi inaendeshwa na majina ya matatizo, lazima ielezwe bila kusahau, kuacha au kurahisisha, ili isijitoe katika ushawishi wa itikadi za rangi tofauti zenye uwezo wa kuharibu kila kitu ambacho ni tofauti. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 21 Novemba 2024  amechapisha barua kuhusu upyaishaji wa somo la historia ya Kanisa ili kuwasaidia mapadre kutafsiri vyema ukweli wa kijamii hasa kwa kuzingatia mafunzo ya mapadre wapya na mawakala wa kichungaji. Matumaini ya Papa ni kwamba, “kupitia utafiti huu kwa sababu ni utafiti na si kuzungumza au muhtasari kwenye mtandao, kwamba tunaweza kufikia chaguo la ujasiri na la nguvu ambalo, lililochochewa na utafiti, ujuzi na kushirikiana, kujibu vizuizi vya kupooza vya matumizi kupita kiasi ya kiutamaduni.”

Kumwilisha uhusiano na vizazi vilivyopita

Huku akitambua umakini ambao mapadre hujitolea katika masomo ya historia ya Kanisa, Papa Fransisko alianza kwa kutoa mwaliko wa  “ukuzaji wa usikivu halisi wa kihistoria kwa wanafunzi vijana wa Taalimungu. Hiyo ni kuzoeana wazi na mwelekeo wa kihistoria wa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuwajua kwa hakika wao ni akina nani na wanakusudia kuwa nani kesho bila kulea dhamana inayowaunganisha na vizazi vilivyowatangulia,” anaandika.

Wajibu wa kimaadili, kushirikiana na mshikamano

Utafiti, katika maono ya Papa, hunaweka “hai mwali wa dhamiri ya pamoja, ikijitenga na kumbukumbu za mtu binafsi zinazohusishwa na maslahi ya mtu mwenyewe au hisia za mtu, bila uhusiano wa kweli na jumuiya ya kibinadamu na ya kikanisa ambayo tunajikuta tunaishi. Kwa hivyo inawezekana kusuka uhusiano na ukweli ambao unahitaji uwajibikaji wa kimaadili, kushirikiana na mshikamano.”

Kanisa, mama wa kupendwa kama Yeye

Papa Francisko katika barua hiyo anamnukuu mtaalimungu  Mfaransa ambaye alisema kwamba uchunguzi wa historia “unatulinda dhidi ya imani ya kidini yaani, kutoka katika maono ya kimalaika sana"ya Kanisa ambayo yanapuuza madoa na mikunjo yake. Na Kanisa, kama mama, lazima lipendwe kama yeye, vinginevyo hatulipendi kabisa, au tunapenda roho ya mawazo yetu. Hujifunza kutokana na makosa yake na kujitambua hata katika nyakati zake za giza, kuponya majeraha yake na yale ya ulimwengu lnamoishi.”

Itikadi zinazoharibu walio tofauti

Waraka wa kitume wa baada ya Sinodi  wa Christus vivit, yaani Kristo anaiishi, Papa Francisko anaandika kuwa tayari ulikuwa na mwaliko wa “kuwa waangalifu na wale wanaopendekeza kupuuza yaliyopita na "kutothamini uzoefu wa wazee.” Mtu huyo anahitaji wewe kuwa mtupu, kung'olewa, kutoamini kila kitu, ili uweze kuamini ahadi zake tu na kutii mipango yake. Hivi ndivyo itikadi za rangi tofauti zinavyofanya kazi, ambazo huharibu (au kutengeneza) kila kitu ambacho ni tofauti na kwa njia hii wanaweza kutawala bila upinzani.”

Hatari ya kumbukumbu uangafu inahitajika

Ufunguo wa kusoma sasa ni mafunzo na tathimini, ambayo inakataa kukaa kwenye kuoanisha. Mtazamo huo,  Papa anabainisha kuwa, “ni wa dharura ili kukabiliana na kufutwa kwa siku za nyuma na historia au masimulizi ya kihistoria yenye upendeleo. Tatizo huwa kubwa zaidi ikiwa tutafikiria kuhusu historia zilizotungwa kwa uangalifu na kwa siri ambazo hutumikia kujenga kumbukumbu za dharura, kumbukumbu za utambulisho na kumbukumbu za kutengwa.”

Hukumu hiyo ilikabidhiwa kwa mitandao ya kijamii pekee

Hata hivyo, utafiti wa ukweli, wa zamani au wa sasa, haupaswi kubadilika kwa kurahisisha ujinga na hatari. Ikiwa hukumu ya wakati wa kutisha na watu wa giza sana inakabidhiwa kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au kwa ajili ya maslahi ya kisiasa tu, kila mara tunakabiliwa na msukumo usio na mantiki wa hasira au hisia. Mwishowe, kama wanavyosema, kitu kisicho na muktadha hutumika kama kisingizio.”

Unaweza kusoma Barua ya Papa Francisko kwa kubonyeza hapa:LEGGI IL TESTO INTEGRALE DELLA LETTERA DI PAPA FRANCESCO

Historia ya Kanisa, kati ya ukweli na tatizo na  majina

Papa Francisko anataja mashauri ya Yesu, kama yalivyosimuliwa katika Injili ya Mathayo, "inayoundwa na historia ya kweli, ambapo kuna baadhi ya majina ambayo ni shida kusema kidogo". Kadhalika, Kanisa halipuuzi ukweli kwamba, miongoni mwa washiriki wake, makasisi na walei, “hakukuwa na upungufu wa wale ambao hawakuwa waaminifu kwa Roho wa Mungu. Kwa chochote ambacho historia ya hukumu inatoa juu ya kasoro hizi, lazima tuzifahamu na kuzipiga marufuku kwa nguvu, ili katika kueneza Injili kusidhurike.

Kumbukumbu isonge  mbele

Papa Francisko kadhalika anahimiza tusiwaalike watu kusahau. Matukio kama vile Shoah,(Kimbari) milipuko ya mabomu ya atomiki huko Hiroshima na Nagasaki, na mapigo mengine mengi yanatufanya tuone aibu kuwa wanadamu. Kumbukumbu za kukumbukwa bila kugandishwa, bila kuangukia katika jaribu la kufukuza na muda mwingi umepita na tunahitaji kutama mbele. Hapana, kwa ajili ya Mungu! Bila kumbukumbu hatusogei mbele kamwe, hatuwezi kukua bila kumbukumbu safi na nzuri.

Shauku na ushiriki katika kusoma

Utafiti wa historia ya Kanisa, Papa zaidi anabainisha  haupaswi kuwekewa kikomo kwa mtazamo wa mpangilio wa matukio tu au kwa upunguzaji wa jumla usio na uwezo wa mazungumzo na ukweli ulio hai.” Papa Francisko pia anasisitiza umuhimu wa kuwaelimisha wanafunzi kutafuta kwa usahihi vyanzo, kubadilisha kujifunza kuwa "shauku na ushiriki. Ni muhimu kutoa ushahidi kwa wale ambao hawajaweza kutoa sauti zao"katika historia. Miongoni mwa haya, Papa anatualika kudhihirisha uzoefu wa kifo cha kishahidi. Hasa ambapo Kanisa halijashinda machoni pa ulimwengu ni pale ambapo limefikia uzuri wake mkuu.

Kazi kubwa

Papa Francisko kwa kuhitimisha anaandika kwamba:  Tunazungumza juu ya kusoma, sio juu ya kuzungumza, juu ya usomaji wa juu juu, juu ya kukata na kubandika muhtasari kutoka katika  Mtandao. Ni muhimu kuuliza maswali yenye lengo la kupata maana ya maisha bila kurudi kwenye yasiyo muhimu. Hili ndilo jukumu lenu kuu: kujibu vizuizi vya kupooza vya utumiaji wa kiutamaduni kwa chaguo thabiti na kali, kwa utafiti, maarifa na kushirikisha.

Barua ya Papa kusoma historia ya Kanisa
21 November 2024, 12:32