2024.11.25 Uwakilisho wa Jainist kimataifa. 2024.11.25 Uwakilisho wa Jainist kimataifa.  (Vatican Media)

Papa kwa Jainist:himizo la kujenga mshikamano na amani

Papa Fransisko akikutana na wajumbe wa kimataifa wa dini ya kale ya mashariki ametumaini kwamba mazungumzo ya kidini yanayoongezeka kila mara yanaweza kufanya kushirikiana kwa ajili ya kujumuisha, kutunza dunia, maskini na watu dhaifu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

BabaMtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican Jumatatu tarehe 25 Novemba 2024 na Uwakilishi wa Kimataifa wa  dini ya Kalie ya Mashariki. Katika hotuba yake Papa  amewakaribisha, hao wanatoka sehemu mbalimbali za dunia, katika mkutano ulioratibiwa na Taasisi ya Jainology ya London Uingereza. Kwa hiyo amefurahi kwamba ziara yao ni sehemu ya mazungumzo yanayokua kati ya Wajaini na Wakristo, ambayo yamekuwa yakifanyika kwa miongo kadhaa, yanayohamasishwa na Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini. Wakati wa mkutano wao wanajadiliana na baadhi ya washiriki wa Baraza la Kipapa kwa jinsi ya kushirikiana kwa maisha bora ya baadaye, wakigusa mada za utofauti na ujumuishaji. Baba Mtakatifu Francisko hata hivyo ametaka kuwambia “habari mbaya, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini Kardinali Ayuso (Guixot) yuko katika hali mbaya kiafya, anakaribia kufa.  Sala zenu zinahitajika kwa ajili yake.”

Papa akiendelea ameshukuru kwa kujitolea kwao kutafuta njia za pamoja za kutunza dunia, maskini na watu walio katika mazingira magumu zaidi katika jamii. Maeneo haya ya kutafakari na kuchukua hatua yamekuwa muhimu sana kwa nyakati zetu, na mipango inayohitajika lazima itekelezwe kwa umakini, kujitolea na kuwajibika kwa ushirikiano. Matatizo mengi yanayoikumba jamii siku hizi yanatokana na ubinafsi na kutojali, jambo ambalo linapelekea watu wengi kudharau utu na haki za wengine, hasa katika miktadha ya tamaduni nyingi. Kwa upande mmoja kuna makundi ambayo yanatawala na kuwatenga walio wachache, yakibaki viziwi kwa “kilio cha dunia na kilio cha maskini” (Laudato si’, 49). Kwa upande mwingine, wapo wanaolenga kujenga urafiki wa kijamii, mshikamano na amani ya kudumu. "Mambo matatu tunapaswa kuyazingatia kila wakati: urafiki wa kijamii, mshikamano na amani."

Kwa bahati mbaya, juhudi hizi za kujenga mara nyingi kuna vizingiti na kuzuiwa. Hata hivyo hatupaswi kuvunjika moyo, wala kuogopa kupanda tumaini kupitia mipango inayokuza hisia ya ubinadamu ndani yetu waamini na kwa kila mtu. Kujitolea huku kwa kudumu kunatokana na ukweli kwamba “Mungu aliumba wanadamu wote sawa katika haki, wajibu na utu, na akawaita kuishi pamoja kama kaka na dada” (Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Amani ya Dunia na Ushirikiano huko Abu Dhabi, 4 Februari 2019). “Hatupaswi kamwe kusahau udugu huu wa ulimwenguni pote.” Kila mtu mwenye mapenzi mema anaweza kueneza upendo, kujitolea kwa wale wanaohitaji huku akiheshimu tofauti. Ni mtindo huu ambao daima hutupa nguvu mpya ya kutunza kila mmoja na nyumba yetu ya kawaida. Mikutano ya kidini kama ile inayopangwa husaidia kuimarisha nia ya pamoja ya kufanya kazi pamoja ili kujenga ulimwengu bora. Ninawashukuru kwa ziara yenu na kwa kujitolea kwenu, na ninawatakia nyote mazungumzo yenye amani na matunda.

Papa na Jainist Kimataifa
25 November 2024, 16:51