Ushiriki wa Jumuiya ya Watanzania katika Katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 13 Novemba 2024. Ushiriki wa Jumuiya ya Watanzania katika Katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 13 Novemba 2024. 

Jumuiya ya Watanzania,Roma:Papa awatakia furaha na amani ya Bwana wetu Yesu Kristo!

Katika salamu zake Baba Mtakatifu kwa mahujaji na wageni wote wanaozungumza Kiingereza walioshiriki katika katekesi yake aliwasalimu"hasa vikundi kutoka Uingereza,ndonesia,Japan,Korea,Uholanzi,Ufilipino na Marekani na kwa namna ya pekee,salamu kwa mapadre,watawa na waseminari kutoka Tanzania,ambao wamekuja Roma kwa ajili ya masomo yao.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya katekesi yake, akiwasalimia mahujaji  na waamini kutoka pande za dunia kwa upande wa lugha ya kiingereza, Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 13 Novemba 2024 alisema “Ninawasalimu mahujaji na wageni wote wanaozungumza Kiingereza wanaoshiriki katika katekesi ya leo, hasa vikundi kutoka Uingereza, Indonesia, Japan, Korea, Uholanzi, Ufilipino, na Marekani.

Jumuiya ya Watanzania washiriki katekesi ya Papa Francisko
Jumuiya ya Watanzania washiriki katekesi ya Papa Francisko

Salamu kwa Jumuiya ya Watanzania Roma

Papa Francisko akiendelea alisema: "Kwa namna ya pekee, ninawasalimu mapadre, waliowekwa wakfu na waseminari kutoka Tanzania, ambao wamekuja Roma kwa ajili ya masomo yao. Juu yenu nyote, na juu ya familia zenu, ninawatakia furaha na amani ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu awabariki!”

Jumuiya ya watanzania Roma washiriki Katekesi ya Papa Francisko
Jumuiya ya watanzania Roma washiriki Katekesi ya Papa Francisko

Hata hivyo mara baada ya katekesi ya Papa Francisko, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Italia kwa upande wa Mapadre, Watawa na waseminari, Padre Joseph Herman Luwela alifika katika vyombo vyetu ya Radio Vatican. Katika mahojiano naye kuhusiana na tukio hili  Padre Luwela alisema:  “Kwa upande wa jumuiya ya Watanzania waishio Italia ilikuwa ni furaha na fursa ya kipekee kushiriki katekesi ya Baba Mtakatifu na kupokea baraka za kitume, kwani Baba Mtakatifu alikazia juu ya furaha ya Injili ikirejea 'Ndiyo au (Fiat)' ya Bikira Maria, Mama wa Mungu kwa kukubali kuwa Mama wa Mungu na mfuasi wa kwanza wa Kristo, kwamba daima tuwe tayari kuitikia Mwito wa Mungu kwa ajili ya utume."

Ushiriki wa Jumuiya ya Watanzania katika katekesi ya Papa
Ushiriki wa Jumuiya ya Watanzania katika katekesi ya Papa

Padre Luwela aidha alieleza kuwa "Papa Francisko kisha aliwaaga mahujaji kwa kuwahimiza kuombea "amani na upatanisho kwa zile nchi zenye mapigano na vita kwani amani ni tunu adimu na inahitajika sana sana na kila mtu" hivyo ni vema kuilinda wakati wote, kisha alitoa baraka za kitume kwa mahujaji wote na kusali sala ya Baba Yetu kwa Lugha ya Kanisa, yaani kilatini pamoja na mahujaji wote kisha kuwabariki na kuwaaga. Kwa upande wake akifafanua hisia za walioshiriki alisema "Hakika kwa jumuiya ya Watanzania Italia walikuwa wenye bashasha na furaha kwa kushiriki tukio hilo la katekesi linaloongozwa na Kharifa wa Kristo na mchungaji Mkuu wa Kanisa la Ulimwengu."

Jumuiya ya watanzania Roma washiriki katekesi ya Papa
Jumuiya ya watanzania Roma washiriki katekesi ya Papa

Ikumbukwe, Jumuiya ya Watanzania wakatoliki nchini Italia, kwa upande wa Umoja unaojumuisha Mapadre, Masista, Mabruda na mafrateli (wa mashirika) na waseminari ambao wako nchini Italia kwa ajili ya masomo na wengine katika utume mbalimbali walikutana pamoja katika Chuo cha Kipapa cha Mtakatifu Paulo jijini Roma, Jumamosi tarehe 9 Novemba 2024, kama sehemu ya matukio mbali mbali ya kawaida ya mwaka hasa awali ya yote misa kwa nia ya kumshukuru Mungu kwa mwaka uliopita na kuanza mwaka mpya wa masomo masomo 2024/2025. Misa pia ilikuwa kuwaombea ndugu zetu marehemu hasa wale wa wanajumuiya wenzetu waliokufa mwaka huu na marehemu wote katika mwezi huu wa Novemba wa kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.


Papa ametoa salamu na kuomba tuombee amani

 

 

13 November 2024, 17:34