Papa kwa Rota Romana:lazima kutenda haki,upendo na ukweli
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Fransisko alikutana na washiriki wa kozi ya mafunzo ya Mahakama Kuu ya Rufaa ya Kipapa “Rota Romana”, Jumamosi tarehe 23 Novemba 2024 mjini Vatican ambapo katika hotuba yake amefurahi kukutana nao ambapo katika Kozi yao imeongozwa na mada ya Ministerium Iustitiae et Caritatis in Veritate, yaani Huduma ya Haki na Upendo katika Ukweli. Papa kwa hiyo amewasalimia wote na kuwashukuru wote hasa kwa walioshirikiana katika siku hizi za mafunzo na za tafakari. Mafunzo hayo yamekuwa fursa ya kuchunguza changamoto za kimahakama-kichungaji zinazohusu ndoa na familia. Haya ni muhimu sana. Huo ni uwanja mpana, lakini pia changamano na nyeti wa kitume, ambao unatakiwa kujitolea nguvu na ari, kwa lengo la kukuza Injili ya familia na maisha. “Upendo katika ukweli, ambao Yesu Kristo aliushuhudia kwa uhai wake wa duniani na zaidi ya yote, kwa kifo na ufufuko wake, ndio msukumo mkuu wa maendeleo ya kweli ya kila mtu na pia ya wanadamu wote. Upendo – “caritas” - ni nguvu isiyo ya kawaida, ambayo inasukuma watu kujitolea kwa ujasiri na ukarimu katika uwanja wa haki na amani. Ni nguvu ambayo asili yake ni Mungu, Upendo wa milele na Kweli kabisa.” Papa Francisko kwa kuongeza amesema: “Kwa maneno haya Papa Benedikto wa kumi na sita alifungua Waraka wake wa Caritas in veritate, (Upendo katika Ukweli) ambamo anawasilisha mafundisho ya kijamii ya Kanisa katika mtazamo wa uhusiano kati ya upendo na haki, na yote mawili na ukweli.
Ni maneno yanayotumika kwa nyanja nzima ya asasi za kiraia, lakini ambayo yanafaa kabisa wakati wa kuzingatia uhusiano kati ya waamini na kati yao na Wachungaji, ndani ya Watu wa Mungu. Kwa hiyo inafaa sana kuimarisha utume wa Mahakama kuu ya Rufaa ya Roma (Rota Romana) kama “ministerium iustitiae et caritatis in veritate” – “huduma ya haki na upendo katika ukweli”; na maelezo haya yanaweza kupanuliwa kwa mabaraza yote ya kikanisa ya ulimwengu, kwa hakika, yanakumbatia matendo yote ya kichungaji ya Kanisa, ambayo yamekuwa mada ya Mkutano huu. Moyo wa ujumbe ambao Papa alipenda kuwaachia ni kwamba wameitwa kupenda haki, upendo na ukweli, na kujitolea kila siku kuyatekeleza katika kazi yao kama wanasheria wa kanuni na katika kazi zote wanazozifanya kwa huduma ya waamini. Hata katika majukumu yao ya kisheria lazima wakumbuke kila wakati: watu lazima watendewe sio haki tu, ambayo ni muhimu, lakini pia na juu ya yote kwa upendo. Kamwe wasisahau kwamba yeyote anayewakaribia akiwaomba watumie ofisi yao ya kikanisa lazima wakutane na uso wa Mama yetu, Kanisa takatifu, anayewapenda watoto wake wote kwa huruma. Haki isiyo na huruma ambayo ni ya kugawanya tu bila kwenda zaidi ya hapo, yaani, bila huruma, lazima iepukwe, Papa Francisko amekazia. Katika Waraka wa Fratelli tutti, yaani Wote ni Ndugu, inachosema kinaweza kutumika kwa haki kwamba: “Watu wanaweza kukuza mitazamo fulani ambayo wanawasilisha kama maadili ya kimaadili: ujasiri, kiasi, bidii na fadhila zingine.”
Baba Mtakatifu katika hilo aliongeza kusema “Siwezi ‘kumpatia mwingine’ kile ambacho ni changu, bila kwanza kumpatia kile anachostahili kwa haki. Yeyote anayewapenda wengine kwa upedo, kwanza kabisa ni mwadilifu kwao.” Kwa hakika kwa sababu ukimpenda kila mwamini, unasitawisha usikivu wako wa kisheria, usioeleweka kama inavyofikiriwa mara nyingi kama utimilifu tu wa taratibu ambazo zinafaa, lakini kama utambuzi dhaifu wa kile kinachojumuisha haki ya kweli ya mtu katika Kanisa. Utu wake usio na kikomo lazima uwe wa mfano kuheshimiwa katika mahusiano ya ndani ya Kikanisa. Upendo haufuti haki, hahusiani na haki. Kwa jina la upendo, kile ambacho ni wajibu wa haki hakiwezi kupuuzwa. Kwa mfano, sheria za sasa za kesi za ndoa haziwezi kufasiriwa kama, katika utafutaji muhimu wa ukaribu na kasi, kwani kufanya hivyo zinamaanisha kudhoofisha mahitaji ya haki. Kwa upande wake, huruma haifuti haki, kinyume chake inatusukuma kuiishi kwa ustadi zaidi kama tunda la huruma mbele ya mateso ya wengine. Kwa hakika, “usanifu unaotegemeza maisha ya Kanisa ni huruma, hiyo ndiyo usanifu.” Kila kitu katika utendaji wake wa kichungaji kinapaswa kufumbatwa katika upole anaohutubia waamini; mitazamo mitatu ya Bwana, ambayo ni: Ukaribu, huruma na upole. Bwana yu karibu, amejaa huruma na ni mpole.
Baba Mtakatifu kwa washiriki hao wa kozi alisema kwamba "Kanisa linaweka imani kubwa kwao, kama waendeshaji wa haki na upendo katika ukweli. Hali ya kazi yao na iwe ya matumaini, ambayo ni katika Mwaka Mtakatifu ujao. Inawezekana kutona kwao Waraka ambao Papa aliandika katika Barua akisema: “Hebu sasa tujiruhusu kuvutiwa na matumaini na tuyaruhusu yaambukizwe kupitia sisi kwa wale wanaoyatamani. Maisha yetu yawambie wao kwamba: “Mtumaini Bwana, uwe hodari, moyo wako na uimarishwe na umtumaini Bwana” (Zab 27,14). Nguvu ya tumaini na ijae wakati wetu huu, tunapongojea kwa ujasiri kurudi kwa Bwana Yesu Kristo, ambaye sifa na utukufu zimwendee kwa karne zijazo.” Kwa ajili ya utume wao na kwa ajili ya utakaso wao ndani yake, kwa moyo mkunjufu Papa Francisko ametoa baraka kwao na wakati huo huo ameimba wasisahau tafadhali kusali kwa ajili yake.