Tafuta

2024.11.25 Papa na Jumuiya ya Taasisi ya Yohane Paulo II kuhusu Taalimungu  na Sayansi ya  Familia na Ndoa 2024.11.25 Papa na Jumuiya ya Taasisi ya Yohane Paulo II kuhusu Taalimungu na Sayansi ya Familia na Ndoa  (Vatican Media)

Papa kwa Taasisi ya Kipapa ya Taalimungu ya Ndoa na Familia:Upendo ni mkuu katika familia

Baba Mtakatifu Francisko amekutanana maprofesa na wafanyakazi wa Taasisi ya Kipapa ya Taalimungu ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II.Katika hotuba yake Papa alivitaka vyuo vikuu vya Kikatoliki kutafiti jinsi gani tamaduni mbalimbali zinavyoona ndoa na kwamba Kanisa linataka kusindikizana na familia katika njia yao ya utakatifu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 25 Novemba 2024 Baba Mtakatifu Francisko alikutanana maprofesa na wafanyakazi wa Taasisi ya Kipapa ya Taalimungu ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II katika fursa ya Ufunguzi wa Mwaka wa masomo 2024/2025 ambapo katika  salamu na shukrani kwa Kansela Askofu Mkuu Vincenzo Paglia,Askofu Philippe Bordeyne, na pia makamu rais wa vitengo vya kimataifa, maprofesa, wanafunzi, wajumbe wa Mfuko wa Benedikito XVI na wafadhili. Kama wanavyojua katika hati ya mwisho ya Mkutano Mkuu XVI wa Sinodi inathibitisha kuwa familia ni mahali muafaka kwa ajili ya mafunzo na kufanya uzoefu msingi wa Kanisa la Kisinodi (35). Kwa leo hilo lazima ikuwa ndani mwake na utambuzi  wa kuwa  mafunzo na sio wapokeaji tu wa uchungaji wa familia, wawajibikaji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na jitihada za kijamii (64). Papa ameongeza kusema, ni kwa jinsi gani ndoa na familia ni za maamuzi kwa ajili ya Maisha ya watu: na daima Kanisa limekuwa likitunza, likisaidia na kuinjilisha.

Papa Francisko katika hilo pia amebainisha kwamba kwa bahati mbaya, kuna nchi ambazo mamlaka ya Umma hawaheshimu hadhi na uhuru ambao kila binadamu ana haki isiyoweza kubatilishwa kama mtoto wa Mungu. Mara nyingi kuna vizingiti na kulazimisha ambavyo huelemea hasa wanawake, na kuwalazimisha katika nafasi za utii. Hata hivyo, tangu mwanzo miongoni mwa wanafunzi wa Bwana walikuwepo wanawake pia na katika Yesu Kristo, anaandikia Mtakatifu Paulo, kuwa “hakuna mwanaume  wala mwanamke” (Gal 3,28). Hii ina maana ya kusema kuwa tofauti kati ya wote wawili ilifutwa, badala yake ni kwamba katika mpango wa wokovu hakuna ubaguzi kati ya mwanamume na mwanamke: wote wawili ni wa Kristo;  wao ni "wazao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ahadi(Gal 3,29).

Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba “Kwa njia ya Yesu sisi sote tumekombolewa na dhambi, huzuni, utupu wa ndani, upweke (Evangelii Gaudium,1) na Injili ya familia ni faraha ambayo inajaza moyo na Maisha kamili (Amoris Laetitia,200). Na Injili hii ambayo inasaidia wote, katika kila tamaduni, kutafuta daima kile ambacho ni cha binadamu na shauku ya wokovu iliyokita mizizi kwa kila mwanaume na kila mwanamke. Kwa namna ya pekee, Sakramenti ya Ndoa ni kama divai nzuri ambayo ilitolewa katika arusi ya Cana (Yh 2,1-2). Katika pendekezo hilo, Papa Francisko amesema “tunapaswa kukumbuka kuwa Jumuiya za kwanza za Kikristo iliendelea katika mfumo wa kinyumban, kwa kupanua vifundo vya familia kuwakaribisha waamini wapya, na walikuwa wakikusanyika majumbani. Kama nyumba iliyofunguliwa na kukaribisha, tangu mwanzo wa Kanisa, lilijikita ili vizuizi wa kiuchumi au kijamii visiweze kuzuia kuishi ufuasi wa Yesu. Kuingia katika Kanisa maana yake ni kuzundua udugu mpya daima uliosimikwa juu ya Ubatizo, ambao unakumbatia mgeni  hadi adui. Kwa kujikita katika utume,  hata Kanisa leo hii halifungi mlango wake ambao wanashiriki katika safari ya Imani, badala yake wanafungua mlango kwa wote wenye shida na umakini wa kichungaji wa huruma na kuwatia moyo(Amoris laetitia, 293).

"Mantiki ya ushirikiano wa kichungaji ni ufunguo wa ufuataji wa kichungaji" kwa wale "wanaoishi pamoja kwa kuahirisha kwa muda usiojulikana ahadi zao za ndoa" na kwa watu walioachana na walioolewa tena. “Wamebatizwa, ni kaka na dada, roho Mtakatifu anamimina kwao zawadi na karama kwa ajili ya wema wa wote (299): uwepo wao katika Kanisa unashuhuda utashi wa kudumu katika imani, licha ya majeraha ya uzoefu mchungu. Bila kubagua yeyote, Kanisa linahamasisha familia, iliyosimikwa juu ya Ndoa kwa kutoa mchango kila mahali na kila wakati ili kufanya kuwa thabiti muungano wa ndoa, katika familia ya upendo ambao ni mkubwa zaidi ya yote yaani upendo(89). Baba Mtakatifu amesema kwamba “Kiukweli “nguvu ya familia inakaa katika uwezo wake muhimu wa kupenda na kudumisha kupenda;” haijalishi jinsi gani familia inaweza kujeruhiwa, "inaweza kukua kuanzia  upendo (53).” Papa Francisko alisisitiza kuwa changamoto, matatizo na matumaini yanayogusa ndoa na familia ya leo ni sehemu ya uhusiano kati ya Kanisa na utamaduni, ambayo tayari Mtakatifu Paulo VI alitualika kuyazingatia, akisisitiza kwamba “mpasuko kati ya Injili na utamaduni ni mchezo wa kuigiza wa zama zetu(Evangelii nutiandi,20).

Mtakatifu Yohane Paulo II na Benedikito XVI waltafakari kwa kima mada ya Utamadunisho kwa kweka moto wa maswali ya Kiumaduni na wa Utandawazi. Kutoka katika uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo inategemea na uwezo wa kujikita kwa ukamilifu utume wa uinjilishaji ambao mkristo anajikita kila siku. Kwa pendekezo hilo, hasa Sinodi ya mwisho ilitajirisha utambuzi wa kikanisa kwa washiriki wote. Papa Francisko amesema kwamba, Taasisi ya Yohane Paul II ina haki ya ushirikiano maalum katika uwanja huu, kwa njia ya tafiti na utafiti unaokuza ujuzi muhimu wa mtazamo wa jamii na tamaduni mbalimbali kuelekea ndoa na familia.  Kwa hiyo, Papa Francisko amesema kwamba alitaka Taasisi pia ielekeze umakini wake «kwa maendeleo ya sayansi ya binadamu na utamaduni wa anthropolojia katika nyanja ya msingi sana kwa utamaduni wa maisha» (Barua ya Kitume Summa familiae cura, Dibaji).

Papa Francisko amesisitiza kwamba ni vyema ofisi za Taasisi zilizopo katika nchi mbalimbali duniani zifanye shughuli zao kwa mazungumzo na wanazuoni na taasisi za kitamaduni, hata kutoka maeneo mbalimbali, kama inavyofanyika tayari kwa Chuo Kikuu cha Roma Tre na Taasisi ya Taifa ya Saratani. Ni matumaini ya Papa kwamba “katika kila sehemu ya dunia, Taasisi itawasaidia wanandoa na familia katika utume wao, kuwasaidia wawe mawe hai ya Kanisa na mashuhuda wa uaminifu, huduma, uwazi wa maisha na ukarimu. Twende pamoja katika kumfuata Kristo! Mtindo huu wa sinodi ulingane na changamoto kubwa za siku hizi, mbele ya familia ambazo ni ishara ya kuzaa matunda na udugu unaosimikwa katika Injili.” Papa Francisko amewatakia mwanzo mwemwa wa mwaka wa masomo na wenye matunda.

 

 

 

25 November 2024, 16:58