2024.11.25  Uwakilishi wa Amani duniani. 2024.11.25 Uwakilishi wa Amani duniani.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa vijana wa Amani duniani:huduma,kujihusisha na matumaini!

Hali ya sasa inafanya uhamasishaji wa amani kuwa muhimu zaidi na hasa vijana kutoka asili na dini tofauti. Hii ni ishara tosha kwamba shauku ya amani imekita mizizi ndani ya moyo wa mwanadamu na kwamba ina uwezo wa kuleta umoja katika utofauti.Ni maneno ya Papa kwa wawakilishi wa vijana, walioandaliwa na Baraza la Amani Ulimwenguni aliokutana nao tarehe 25 Novemba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 25 Novemba 2024, amekutana na wawakilishi wa vijana, walioandaliwa na Baraza la Amani Ulimwenguni. Katika salamu zake, amefurahi kupata fursa ya kukutana nao, wakati wa ziara yao jijini Roma na amewasifu kwa kujitolea kwao kwa ajili ya kazi ya amani katika Nchi Takatifu, nchi ambayo imeshuhudia vurugu na mateso mengi kwa karne nyingi. “Kwa bahati mbaya, siku zetu sio tofauti, na kwa zaidi ya mwaka mawingu meusi ya migogoro yamekuja tena kukumba eneo la ulimwengu unaoita nyumbani. Ni mbaya…” Papa Francisko amesema kuwa “Hali ya sasa inafanya uhamasishaji wa amani kuwa muhimu zaidi na amefurahi kuona kwamba ujumbe wao unaundwa na vijana kutoka asili na dini tofauti. Hii ni ishara tosha kwamba shauku ya amani imekita mizizi ndani ya moyo wa mwanadamu na kwamba ina uwezo wa kuleta umoja katika utofauti. Sisi sote tunajua, hata hivyo kazi yao si rahisi. Kwa sababu hiyo alipenda  kupendekeza mambo matatu mafupi kwa ajili yao.

La kwanza ni kwamba tunahitaji vijana kutekeleza huduma hii muhimu, kwa sababu wana aina fulani ya mawazo, shauku na matumaini, ambayo yanatukumbusha sote kwamba ulimwengu bora unawezekana, kwamba amani inawezekana. Hasa, vijana wanaweza kuwasaidia wengine kugundua vipengele muhimu vinavyofungua njia ya amani: msamaha na nia ya kuacha chuki na majeraha ya zamani. "Vijana ni wabunifu, lakini ni mbaya tunapokutana na vijana "wenye itikadi", ambao itikadi zinachukua nafasi ya mawazo, na nia ya kutenda mema." Papa amelalamika. “Daima tunapaswa kukumbuka na kujifunza kutokana na historia, kushikamana kwa njia inayofaa ili kudhibiti majeraha na ubaguzi wa siku za nyuma ambao hauwezi kamwe kusababisha amani ya kweli na ya kudumu. Kiukweli, mawimbi ya migogoro na mgawanyiko yanaendelea tu.

Jambo la pili ni kujihusisha kila wakati katika mazungumzo, kwani ndio nyenzo kuu tuliyo nayo. “Kukaribia, kujieleza, kusikiliza kila mmoja, kutazama kila mmoja, kufahamiana, kujaribu kuelewana, kutafuta alama za mawasiliano, yote haya yanafupishwa katika kitenzi“mazungumzo.” Mazungumzo ndio njia pekee ya amani.” Kukutana wao kwa wao  Vijana wanaweza kuwa mafundi wakubwa wa amani kwa njia ya mazungumzo.  Jambo la tatu ni kutopoteza matumaini. Matumaini kamwe  hayakatishi tamaa. Msikate tamaa. Ni rahisi sana kuvunjika moyo tunapoona madhara mabaya ya vita, athari mbaya za chuki, bila kusahau umaskini, njaa, ubaguzi na mambo mengine mbalimbali yanayotishia matarajio ya amani. Ukweli huu ni matokeo ya vita.

“Hii inaweza kutufanya tufikiri kwamba kujitolea kwetu kwa mazungumzo ni bure kwa sababu hutoa matokeo machache madhubuti. Labda pia utakosolewa kwa kuzingatia hitaji la mazungumzo ili kuendeleza mambo ya amani. Katika nyakati hizo, kumbuka kwamba jambo lolote linalostahili kufanywa si rahisi kamwe. Inahitaji kujitolea na inahitaji utayari wa kurejea kazini kila siku, haswa wakati mambo hayaendi vile tungependa, Papa alisisitiza. “Endeleeni kuwa na tumaini hai, enyi vijana wapendwa, sikuzote mkikumbuka kwamba sisi sote ni sehemu ya familia moja ya kibinadamu. Sisi sote ni kaka na dada na juhudi za kukuza upatanisho, maelewano na amani daima zitastahili wakati na juhudi zetu. Na, bila shaka, kamwe msipoteze hisia zenu za ucheshi: furaha hiyo ya afya ... Hii ni muhimu sana,” aidha  Msipoteze uwezo huo wa furaha unaowasaidia kuona mambo bora zaidi.  Ninawashukuru kwa ziara yenu na ninawahakikishia maombi yangu kwa kujitolea kwenu  kwa amani katika Nchi Takatifu. Ninawabariki ninyi nyote na ninawaomba, tafadhali, mnikumbuke katika maombi yenu.”

Papa na vijana wa amani duniani
25 November 2024, 16:40