2024.11.16 Papa amekutana na Ujumbe wa Baraza la Kitaifa la Vijana nchini Italia. 2024.11.16 Papa amekutana na Ujumbe wa Baraza la Kitaifa la Vijana nchini Italia.  (Vatican Media)

Papa kwa vijana wote:kuota ndoto na kutazama upeo bila kukata tamaa!

Katika hotuba kwa wajumbe wa Baraza la Vijana la Kitaifa,Novemba 16,Papa Francisko aliwaalika vizazi vipya kuwa mashuhuda wa tumaini lisilokatisha tamaa bila kuathiriwa na tamaa na mashaka.Kutoka katika migogoro migumu,tunaweza kutoka humo pamoja kwa kutazama upeo kulika mchanga wa uadui.“Kusonga mbele katika huduma,kutafuta,kulinda na kutoa sauti kwa wasio nayo na matumaini.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 16 Novemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Baraza la Vijana Kitaifa nchini Italia. Katika hotuba yake alianza kumsalimia Rais na wote na kuwa na furaha kukutana nao katika hafla ya maadhimisho ya miaka ishirini ya Baraza hilo kwamba “ ni hatua muhimu ambayo inakuwa fursa ya kuendelea kujihusisha kwa ujasiri, kabla ya vijana kukata tamaa.” Matumaini hayakatishi tamaa! Papa aliomba wasikilize hilo kwa makini kwamba “matumaini hayakatishi tamaa. Kamwe.” Kwa maneno haya  Papa alisema alivyoakisi Jubilei ya Kawaida ya 2025. Papa ameeleza alivyofurahishwa kusoma kwenye “Tafiti yenu ya Kanuni yenu ya  Nne ya Kujiamini” kwamba tumaini ni mtazamo wa ndani ambamo vijana Waitaliani wanajitambua zaidi leo hii. Mara nyingi tunakutana na watu ambao wamevunjika moyo kwa sababu wanatazamia wakati ujao kwa mashaka na kutokuwa na matumaini.” Kukata tamaa. Kwa hiyo ni muhimu kujua kwamba vijana wa Italia wanajua jinsi ya kuwa mafundi wa matumaini kwa sababu wana uwezo wa kuota. Tafadhali msipoteze uwezo wa kuota: wakati kijana anapoteza uwezo huu, sisemi anakuwa mzee, hapana, kwa sababu wazee huota. Bali wanakuwa mstaafu wa Maisha.”Ni mbaya sana."

Vijana msiwe wastaafu wa maisha

Papa Francisko alisema kuwa "Tafadhali, vijana, msiwe wastaafu wa maisha, na msijiruhusu kuibiwa na matumaini! Kamwe! Matumaini kamwe hayakatishi tamaa!” Papa alisisitiza sana. Katika mazungumzo na taasisi, nyinyi ni chombo cha mashauriano kilichoitwa kuwakilisha ulimwengu wa vijana katika ngazi ya ndani, kitaifa na Ulaya. Na kwa kusudi hili lazima kukuza ushiriki hai wa vijana, kuunda "mtandao" kati ya vyama vingi vinavyochochewa na maadili kama vile mshikamano na ushirikishwaji. Kutengeneza mtandao, lakini pia kufanya kelele. Ni muhimu sana. Katika kazi hiyo -ya mitandao na kufanya kelele”, Papa amewaalika kuwa sauti ya kila mtu, hasa wale ambao hawana sauti. Na leo hii kuna watu wengi hawana sauti, wengi wametengwa, si tu kijamii, kutokana na matatizo ya umaskini, ukosefu wa elimu, udikteta wa madawa ya kulevya ... lakini pia wale ambao hawajui jinsi ya kuota. Mtandao wa kuota, na wasipoteze uwezo huo wa kuota Ndoto. Papa Francisko aidha alisema “Kama tujuavyo - pia kutoka katika habari za hivi karibuni -kuna changamoto nyingi zinazowahusu: heshima ya kazi, familia, elimu, kujitolea kwa raia, utunzaji wa uumbaji na teknolojia mpya. Kuongezeka kwa vitendo vya unyanyasaji na kujidhuru, hadi kitendo cha kupindukia zaidi cha kujiua, ni ishara za usumbufu wa wasiwasi na ngumu.”

Baraza la vijana Kitaifa Italia
Baraza la vijana Kitaifa Italia

Papa alisema wanajua kwamba, ulimwenguni pote, kujiua kwa vijana si yote yanayochapishwa, yamefichwa. Ni mabadiliko ya enzi, hatua moja hadi ukomavu lakini sio tu ya kiutamaduni bali pia ya kianthropolojia. Ndiyo maana njia ya elimu inayohusisha kila mtu ni muhimu. Ninaweza kusema kwamba tunahitaji “kijiji cha elimu ambapo, katika utofauti, tunashiriki ahadi ya kuzalisha mtandao wa mahusiano ya kibinadamu na ya wazi. Tunahitaji mapatano, muungano, kati ya wale wanaotaka kumweka mtu katikati na, wakati huo huo, wako tayari kuwekeza nguvu mpya katika mafunzo ya wale ambao watakuwa kwenye huduma ya jamii. Mnaitwa kuwa mashahidi wa uzuri na upya wa maisha. Kuna uzuri unaopita zaidi ya mwonekano: ni ule wa kila mwanamume na kila mwanamke anayeishi wito wao wa kibinafsi kwa upendo, katika huduma ya kujitolea kwa jamii, katika kazi ya ukarimu kwa furaha ya familia, kwa kujitolea bure kukuza urafiki wa kijamii. Kugundua, kuonesha na kuangazia uzuri huu kunamaanisha kuweka misingi ya mshikamano wa kijamii na utamaduni wa kukutana. Utumishi wao na  nia kwa ukweli na uhuru, kwa haki na amani, kwa familia na siasa ni mchango bora na muhimu zaidi unaweza kutoa kwa taasisi kwa ajili ya ujenzi wa jamii mpya.

Papa alikutana na Baraza la  vijana kitaifa Italia
Papa alikutana na Baraza la vijana kitaifa Italia

 “Na hii haifanywi kwa mawazo, inafanywa kwa uwezo wa kibinadamu, uwezo wetu wote, bila kusahau ukali wa maisha. Haya ni mambo mawili ambayo Papa Francisko amwaachia maswali: baadhi yao wameolewa, wamezaa watoto  je na wanajua kucheza na watoto? Je, wana uwezo wa kupoteza muda kucheza na watoto wao au wajukuu zao? Je, wana uwezo wa hili? Uwezo huu wa kucheza Na kisha, swali lingine: una uwezo wa kubembeleza mtu mzee? Kucheza na watoto na kubembeleza wazee. Na leo katika tamaduni zetu watoto wanaachwa wakue peke yao, bila huruma, na wazee wanapelekwa kwenye nyumba za kustaafu, na kufia huko ... Tunapaswa kubadilika: kucheza na watoto na kubembeleza wazee. Na hii itahakikisha kwamba ujana wenu  unazaa matunda. Msisahau hili: watoto na wazee.”

Hatimaye, Papa Francisko ameomba aruhusiwe kuwapa  jambo muhimu zaidi, “ukweli huo ambao kwa Mkristo haupaswi kunyamazishwa kamwe. Ni tangazo ambalo linahusu kila mtu, mdogo kwa mzee, na kwamba tunahitaji kusikia tena kila wakati: “Mungu awakupenda, mnajua”? Kristo anakuokoa na Anaishi”! Na ikiwa Anaishi, basi tumaini sio bure. Uovu, tamaa, mashaka hayatakuwa na neno la mwisho. Na vijana wengi huanguka katika mashaka haya, pia yanaungwa mkono na madawa ya kulevya. Mwanzoni mwa kuwa Mkristo hakuna uamuzi wa kimaadili au wazo kuu, lakini kuna kukutana na Mtu, kukutana na Yesu, ambaye anatoa maisha  ya upeo mpya. Tumaini, hali ya akili ambalo vijana wa Italia wanajitambua zaidi leo hi, ina jina na uso kwa ajili yetu Wakristo: uso wa Bwana, uso wa Yesu. Kwa kukabiliwa na changamoto na ugumu mnaoweza kukutana nao katika kazi zenu msiogope! Msiogope kupitia migogoro pia. “Migogoro hutufanya kukua. Lakini Msisahau kwamba migogoro ni kama njia ngumu ya kupitia: huwezi kutoka nje ya njia ngumu peke yako, unatoka pamoja na mtu mwingine anayekusaidia.

Mfano wa kuigwa wa Giorgio Frassati

Papa amefafanua kwamba kwanza unapotaka kutokea katika njia hiyo ngumu kupitia  juu lazima uwaruhusu wengine wakusaidie. Na kila wakati kutazama juu ili maisha yasiwe ya safari nguvu isiyopitika  ambayo inaua vijana. Kuzeekea katika njia hiyo ngumu ni kuzeeka kwa maadili ya juu juu. Inasikitisha kuona kijana wa kiume au wa kike wakiishi maisha yao kijuujuu.” Inasikitisha sana ... Katika maisha yenu hata kushinda migogoro - kunahitaji uvumilivu ili kuwabadilisha kuwa na uwezo wa kusikiliza, kutambua wengine, kukua kwa pande zote. Kujaribu kushinda mizozo ni ishara kwamba tumelenga juu zaidi, juu zaidi kuliko masilahi yetu maalum, kutoka kwenye mchanga wa haraka wa uadui wa kijamii. Kusonga mbele katika huduma yao: kutafuta, kulinda na kuleta sauti na matumaini ya vijana wa Italia kwenye mipangilio ya taasisi ili kushiriki pamoja katika manufaa ya wote. Papa Francisko amewakabidhi  kwa Mwenyeheri Pier Giorgio Frassati. Na kuwauliza kama wanamfahamu? Nilikuwa nimesikia kumhusu nikiwa mtoto, kwa sababu baba yangu alikuwa mshiriki wa Chama Katoliki cha Matendo ya vijana. Yeye ni kijana kama wao , ambaye ameshuhudia kwa maisha yake furaha ya Injili. Kwa hiyo Papa amewashauri wamfahamu  na kuiga mshikamano wake, ujasiri wake na furaha yake. Amewatakia safari njema kwa kila mtu na kazi nzuri! Amewashukuru kwa  ziara yao. Hatimaye amewabariki kwa moyo wote na kuwaomba tafadhali wasali kwa ajili yake.

Papa na vijana Italia
16 November 2024, 14:32