Papa kwa Wakatoliki wa Estonia:kuendekeza furaha ya kimisionari katika siku zijazo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amemkumbuka Askofu Mkuu Mjesuit Profittlich,mwathirika wa mateso ya kisovieti kuwa nguvu zake za roho katika kukaa karibu na kundi, hadi kumwaga damu, alipanda mbegu ambazo bado zinazaa matunda hadi leo. Amebainisha hayo katika Barua yake aliyoitumwa kwa kwa Askofu Philippe Jourdan wa Tallinn, kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Usimamizi wa Kitume nchini Estonia. Katika barua hiyo Papa anaanza kuwa “Nikiwa na kumbukumbu nzuri za Ziara yangu ya Kitume katika nchi yenu kwa mwaka 2018, ninatuma salamu za dhati, pamoja na hakikisho la ukaribu wangu wa kiroho, kwako na jumuiya yote ya Kikatoliki katika hafla ya kuadhimisha miaka mia moja tangu kuundwa kwa usimamizi wa Kitume wa Estonia, iliyoinuliwa hivi karibuni hadi ngazi ya Jimbo.” Papa amendika.”
Umuhimu wa historia
Papa Francisko anasisitiza kwamba: “Hatua hii muhimu katika historia yao inayoadhimisha karne moja ya uaminifu thabiti kwa imani ya Kikatoliki, ambayo imewezesha Kanisa hilo dogo lakini lililo hai kuwa chanzo cha huruma na lishe ya kiroho kwa wanaume na wanawake wengi nchini kote. Wakati huo huo, maadhimisho haya yanaadhimisha tumaini lisiloyumbayumba na imani kwa Bwana kupitia miongo ya mateso, kazi na ukandamizaji. Kuhusiana na hili, mnapotafakari miaka hii mia moja iliyopita,” Papa anaungana nao katika kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mfano wa imani uliotolewa na wazee wao wa zamani waliokuwa jasiri na wastahimilivu ambao walikuwa muhimu katika kulea na kudumisha jumuiya ya Kikatoliki nchini Estonia.” Kwa namna ya pekee, Papa Francisko amemfikiria “Mtumishi wa Mungu Askofu Mkuu Eduard Profittlich, ambaye ushuhuda wake kwa Kristo na ujasiri wa kukaa karibu na kundi lake, hata kumwaga damu yake, alipanda mbegu ambazo hata leo zinazaa matunda.”
Urithi wa kwa vijana
Ushuhuda wake na uwe daima chanzo cha msukumo kwao na kukukumbusha kwamba hata mimea ndogo sana, ishara ndogo sana na sadaka ya chini kabisa inaweza kukua zaidi ya mwanzo wao mdogo na kutoa mavuno mengi (taz.32). “Zaidi ya hayo, nina hakika kwamba urithi huu wa ajabu wa imani na mapendo unaoidhinisha nao utawatia moyo kizazi cha sasa cha mapadre, watawa na waamini walei kuendelea kukua katika ufuasi wa kimisionari wenye furaha wanapotazamia siku zijazo. Kwa hakika, karne hii ya sasa iwe fursa ya kufanywa upya kiroho katika nchi yao, na kuwasha hisia mpya ya bidii ya uinjilishaji, hasa miongoni mwa vijana. Kwa njia hiyo, wataweza kwa ufanisi zaidi kutangaza ujumbe wa Mungu wa upendo, huruma, na upatanisho, na hivyo, kuleta nuru ya Yesu na nguvu ya ukombozi ya Injili kwa wanaume na wanawake wengi wa siku hizi ambao hata hawaamini katika Mungu.”
Umoja wa kidugu na maelewano
Baba Mtakatifu “Vilevile ni matumaini yangu kwamba, Wakatoliki wa Estonia wanapojitahidi kujenga jamii inayosimikwa katika amani, haki, mshikamano na utu wa kila binadamu, watafanya kazi zaidi pamoja na wanaume na wanawake wa madhehebu mengine ya Kikristo katika kutoa ushuhuda kwa umoja. kwa ahadi za Mungu. Hili ni muhimu hasa katika muktadha wa vita vya leo barani Ulaya, ambavyo ni chanzo cha wasiwasi mkubwa na kwa masikitiko makubwa yanaangazia nyakati za giza za miaka ya nyuma.” Hata hivyo, Roho Mtakatifu anaweza kukuongoza kuwa ishara fasaha ya kuendelea kutumainia maongozi ya Mungu na kuwaongoza Wakristo wa Kiestonia, pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kunyoosha mkono wa urafiki kwa wakimbizi na walio hatarini zaidi kati ya kaka na dada zetu. Kristo Mfalme wa Amani awabariki kwa zawadi zake za uvumilivu, umoja wa kidugu na maelewano. Kwa hisia hizi, ni maombi yangu ya dhati kwamba neema ya Mungu iwasindikize, mapadre watawa, na waamini walei wa Kanisa la Estonia, wanapoanza sura inayofuata ya safari yao iliyojaa imani, tumaini na upendo. “Nikiwakabidhi ninyi nyote kwa maombezi ya Mtakatifu Victor na ulinzi wa upendo wa Maria, Mama wa Kanisa, ninawapa kwa furaha Baraka yangu kama ahadi ya neema nyingi za mbinguni.”