Tafuta

2024.11.21 Mkutano wa Kimisionari wa Marekani (CAM6) huko Puerto Rico. 2024.11.21 Mkutano wa Kimisionari wa Marekani (CAM6) huko Puerto Rico.  (CAM6)

Papa kwa wamisionari:Msingi wa utume ni kukutana na kuguswa upendo wa Yesu

Mfano wa maajabu ni sala ya wamisionari wengi ambao kwa maneno na matendo,wameitangaza.Yesu alikuwa mmisionari,nabii mwenye uwezo katika tendo na neno mbele za Mungu na watu wote.Ni katika ujumbe Papa Francisko alioulekeza kwa Kardinali Enrique Porras Cardozo, nkwa washiriki wa Kongamano la VI la Wamisionari wa Marekani kuanzia 19-24 Novemba 2024.

Na Angella Rwezaula -Vatican

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Franciskoalioulekeza tarehe 21 Novemba 2024 kwa Kardinali Baltazar Enrique Porras Cardozo na kaka na dada washiriki wa Kongamo linaloendelea huko Puerto Riko kuanzia tarehe 19 hadi 24 Novemba 2024  kwamba wao wanayo furaha ya kushiriki katika Kongamano hilo la sita la Wamisionari wa Marekani, hasa katika mwaka ambao Papa mwenyewe alitaka kuutolea kwa ajili ya maombi, kama maandalizi ya Jubilei ya 2025. Na wao wamejitayarisha kwa ajili ya tukio hili kwa maombi ambayo alipenda kutoa  kwa ajili ya tukio hilo. “Ni sala inayoelekezwa kwa Utatu Mtakatifu, kwanza kabisa tukimtambua Baba kuwa ni Mungu wa huruma ambaye, kwa Mwanae Yesu Kristo, ametufunulia “Habari Njema” ili kumsihi amimine, kwa njia ya Roho Mtakatifu Upendo wake na kufanya upya uso wa dunia. Huu ndio msingi wa utume: kujitambua sisi wenyewe kama watoto, kuguswa na huruma ya Mungu.  Msingi wa utume ni uzoefu wa Mungu, kukutana kwa upendo na Yesu, ambaye anafunua "Habari Njema", na anatuonesha Baba.

Kardinali Baltazar Porras
Kardinali Baltazar Porras

Papa anasisitiza kwamba "Mfano wa maajabu haya ni sala ya wamisionari wengi ambao, kwa maneno na matendo, wameitangaza. Yesu alikuwa mmisionari, “nabii mwenye uwezo katika tendo na neno mbele za Mungu na watu wote” (Lk 24:19). Maneno yaliyotamkwa mbele za Mungu, Baba yake, katika sala ya kina  iliyotangulia kila tendo lake. Kazi zilizofanywa mbele za Baba yake katika maisha ya kujitolea kabisa kwa mapenzi yake, ili hivyo kuweza kutoa ushahidi wa upendo mkuu zaidi kwa watu wake. Huu ndio ujumbe ambao wamisionari wameendelea kutafsiri katika kila zama, kila mahali, katika kila lugha. “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Mt 5:16).

Baba Mtakatifu anabainisha kuwa huu ndio wito wa mtu aliyebatizwa ambayo sala inahusu: kumwona Mungu, kumwona duniani, katika ndugu zake, kuwa na macho "ya Kristo" na, pamoja nao, yaani macho ya huruma, ya kukaribisha na ya upole. Kama vile wimbo mzuri wa Liturujia ya masifu unavyosema: "Nilikuona, naam, nilipokuwa mtoto na kubatizwa kwa maji, na, nikiwa nimesafishwa na dhambi za kale, bila pazia, niliweza kukuona". Mwonekano unaopitisha furaha inayofurika kutoka moyoni mwetu. Furaha ya wanafunzi baada ya kukutana na Aliyefufuka, ambayo haiwezi kuzuilika na kuwasukuma kuanza. Roho Mtakatifu hufanya ajabu hii ndani yetu na kuweka ndani yetu maneno ya kumwambia Mungu (rej. Rm 8:14) na kwa wanadamu (rej. Mt 10:19). Kwa hiyo, tangu mapambazuko ya Kanisa, pamoja na Maria, wanafunzi katika semina, katika kusanyiko, jambo la kwanza walilofanya ni kumwomba Roho."

Mama Maria
Mama Maria

Papa wa Roma anafafanua kuwa kupitia nguvu yake ya uzima tunaweza kusambaza ujumbe katika lugha yoyote, ndiyo, kwa sababu Kanisa huzungumza yote, lakini, zaidi ya yote, kwa sababu daima huzungumza kwa lugha moja. Ni lugha ya upendo, inayoeleweka kwa watu wote, kwa kuwa ni sehemu ya asili yao, ile ya kuwa sura ya Mungu. Kwa njia hii, furaha ya Roho haiishii kwao, bali inapanuka, inawasiliana, ikitualika kutembea pamoja, kama Watu waaminifu wa Mungu, katika sinodi na kusikilizana. Tunapomsikiliza Mungu na ndugu zetu, tunaweza kuona jinsi nyakati nyingine mfano wake unavyoonekana kuwa umefifia kwa macho yetu yaliyochoka na inaonekana kwamba hatuna nguvu za kutembea. Hatupaswi kuacha maombi yetu, tukimwomba Baba bila kukoma amimine Upendo wake,  na Roho wake wa uzima, ili aufanye upya uso wa dunia hii uliojeruhiwa kwa udhalimu wetu na mateso tuliyosababisha.

Kongamano la Vi (CAM6) la Kimisionari Marekani
Kongamano la Vi (CAM6) la Kimisionari Marekani

Baba Mtakatifu anaandika kuwa "Bikira Maria Mtakatifu zaidi, Binti wa Mungu Baba, Mama wa Mungu Mwana na Bibi-arusi wa Roho Mtakatifu, anajionesha kama sanduku la Agano, na Hema la kwanza ambaye, kwa kumkaribisha Yesu, alianza safari yake, kwa ajili ya  huduma. Yeye ni kielelezo cha uinjilishaji ili kumtoa Kristo kwa wanadamu wote; kwa sababu katika maombi “aliyaweka hayo yote moyoni mwake” (Lk 2:51), kwa sababu katika kusanyiko la waamini anaomba zawadi ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya Kanisa. Tukiiga kielelezo chake cha kujitolea na kuungwa mkono na utunzaji wake wa uzazi na utunzaji, lazima sikuzote tuwe wanafunzi wake wamisionari hadi miisho ya dunia. Baba Mtakatifu amesema "Awalinde na Yesu awabariki daima,"amehitimisha.

Papa kwa CAM6
21 November 2024, 17:31