Tafuta

2024.11.16 Papa Francisko amekutana na Waseminari wa Majimbo ya  Pamplona, Tudela, Mtakatifu  Sebastian, Redemptoris Mater kutoka Hispania. 2024.11.16 Papa Francisko amekutana na Waseminari wa Majimbo ya Pamplona, Tudela, Mtakatifu Sebastian, Redemptoris Mater kutoka Hispania.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa waseminari:Shukeni kwenye magereza ya kukata tamaa ya maisha!

Katika hotuba yake kwa mapadre watarajiwa kutoka Hispania waliokutana na Papa Francisko katika Ukumbi wa Mikutano tarehe 16 Novemba 2024 aliwashauri kuepuka madaraka ya mali na kusifiwa.Pia ushauri kuwa na ujasiri,bila ubinafsi na bila kuchoka katika kuleta huruma ya Mungu,bila kutofautisha kati ya watu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ingieni katika magereza, sio tu magereza ya serikali, ili kuwapa waliofungwa humo mafuta ya faraja na divai ya matumaini, bali  pia katika magereza ambayo inawafunga wanaume na wanawake katika jamii yetu kama vile : itikadi, maadili; wale walionyanyaswa, waliokatishwa tamaa, ujinga na kumsahau Mwenyezi Mungu. Haya yanapatikana katika Hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na wanaseminari kutoka majimbo ya Kihispania ya Pamplona, Tudela, Mtakatifu Sebastián na Redemptoris Mater, Jumamosi tarehe 16 Novemba 2024 katika Ukumbi wa  Mikutano mjini Vatican. Kwa njia hiyo akiwakaribisha karibu mapadre 40 na pamoja na watarajiwa kutoka Peninsula ya Iberia, Papa Francisko alikumbuka jinsi  ambavyo seminari ni mahali pa kujifunza umuhimu wa ukombozi na kuwa picha  hai ya Yesu, Mkombozi mwenye jina kuu.

Papa na waseminari kutoka Hispania
Papa na waseminari kutoka Hispania

Katika hotuba yake mara kadhaa Papa aliwahimiza kuwatembelea walio gerezani na kushiriki katika huduma hiyo. Alikumbuka jinsi ambavyo tangu alipokuwa Askofu, siku ya Alhamisi Kuu alitembelea Gereza na kuosha miguu ya wafungwa kwa sababu kama wao ndio wanaotuhitaji sana tuoshe miguu yao." Papa alikumbuka kipindi kimoja alipokuwa akiosha miguu ya mwanamke katika gereza la wafungwa  wanawake, na alipokuwa akikaribia kwenda kwa mtu mwingine, huyo alimshika mkono na kumwambia sikioni, “Baba, nimemuua mwanangu.” Papa alisisitiza hili ni janga la ndani linaloathiri dhamiri za wale wanaoishi gerezani. Na kuongeza:  “mtakapokuwa makuhani, nendeni kwenye magereza, ni kipaumbele na pia mtahisi swali linalojitokeza ndani yenu ‘kwa nini wao na sio mimi?’

Akirejea magereza  ambayo si ya kimwili tu bali zaidi ya yote kiakili, kihisia na kiroho ambamo mtu anaweza kujikuta amefungwa, Papa Francisko alirudia kusema kwamba “mtu hupokea upako wa kikuhani kwa usahihi kuwaweka huru wafungwa, wale ambao wamefungwa bila kutambua kwa mambo mengi: utamaduni, jamii, maovu na dhambi zilizofichwa.” Papa alikumbusha tena kutafakari kwa ajili ya maandalizi ya makuhani wa baadaye katika Injili ya Luka ambayo alisema: “inatutia moyo tusiwe na hofu ya kukabiliana na majaribu ya huduma ya ibada ya miungu ambapo sisi tumo katikati, kwa kutafuta madaraka ya mali au kusifiwa” badala yake Papa ametoa wito kwamba “Tuwe na unyenyekevu kwa Roho ili kupitia jangwa hili tupate kukutana na Mungu na kujiondoa wenyewe katika mambo mengi ambayo yanatuelemea.”

Papa na waseminari kutoka majimbo 5 ya Hispania
Papa na waseminari kutoka majimbo 5 ya Hispania

Tena, Papa alisema "kama Yesu alipokwenda Nazareti, akijua kwamba machoni pa ulimwengu hakuwa zaidi ya mwana wa Yosefu, mmoja kama sisi, Papa Francisko alihimiza kuwa “kamwe tusisahau mizizi hii, ya kuwa wana wa watu.” Alisema kwamba katika utume wetu hatuwezi kufanya tofauti za upendeleo kati ya watu, hata zaidi ikiwa ni wageni au hata maadui kwa sababu machoni pa Mungu sisi sote ni watoto,” aliongeza kwamba” tunapomtazama kaka au dada yetu, tunatambua tabia ya kupokea neema ambayo Bwana hutoa.” Tukikumbuka kifungu kingine cha Injili, ambapo Bwana anahuzunika kwa ajili ya ugumu wa mioyo ya watu wa wakati wake ambao hawakuelewi ombi la Yesu la kumfungua mwanamke aliyekuwa amefungwa na pepo mchafu kwa miaka mingi: Papa ameonesha waseminari kwamba: “Ninyi, waseminari, siku zote muwe na  moyo tayari wa kubariki, kuweka huru na kuwa wajasiri, wasio na ubinafsi na wasiochoka katika kutoa huruma ya  Mungu.”

Hotuba ya Papa kwa waseminari wa Hispania
16 November 2024, 17:26