Papa kwa washiriki wa Mkutano wa kanisa la Kambini:Kukarabati ukosefu wa usawa katika jamii
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatatu tarehe 4 Novemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa “Mkutano wa III wa Kanisa Hospitali kambini”( III Encuentro de Iglesias Hospital de Campaña). Katika hotuba yake kwa lugha ya Kihispania amewakaribisha na furaha ya kuwapokea. Amewapatia neno ambalo liwasaidia kutafakari kati yao katika Kanisa kwa ajili ya kusaidia walio maskini zaidi na walio pembezoni. Amewashukuru uwepo wao hapo. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo amependa kushirikishana nao mantiki tatu ambazo alizitaja hivi karibuni: kutangaza Kristo, kusawazisha ukosefu wa haki katika kiungo cha kijamii na kupanda matumaini. Wao kwa kusaidiwa na neema ya Roho Mtakatifu, wanajibidisha ili Makanisa yaweze kuwa Hospitali kambini, kwa kupeleka mbele misingi hiyo mitatu.
Kwanza kabisa, Papa amewatia moyo wao ambao wanatoa ushuhuda wa kukaribisha kuelekea ndugu kwa ishara zaidi ambazo kwa maneno, wanaendelea kuona kila mmoja wao, mwathirika, uso wa Kristo. Ktika hilo wanatangaza Kristo ambaye anatembea daima nao, kwa sababu ni Yeye ambaye akiwa wa kwanza alijifanya maskini kwa kuvua yote (Fil 2,6-11). Mantiki ya pili na kukarabati ukosefu wa usawa. Papa Francisko amesema kwamba kwa utume wao wanashutumu kwa jamii kuhusu ukosefu wa usawa kati ya tajiri na maskini, wakati mwingine mkubwa sana, sio kile ambacho Mungu anataka kwa wanadamu na, kwa haki, ukosefu huu wa usawa lazima utatuliwe. Hii tunahitaji kuanzisha upya mfumo wa kijamii wa kurekebisha ukosefu wa usawa; hakuna anayeweza kubaki na kutojali mateso ya wengine(Mw 4,9).
Na hatimaye, mantiki ya tatu lazima kupanda tumaini. Kila mtu ambaye wanamkaribisha, kwa sababu hana nyumba, kwa sababu ni mkimbizi, kwa sababu ni sehemu ya familia katika hali ya mazingira magumu, kwa sababu ni mwathirika wa vita au kwa sababu nyingine yoyote inayomfanya atengwe na jamii. Ikiwa ndugu zetu hawa mara nyingi huhisi wamekandamizwa wanapokabiliwa na mandhari ambayo inaweza kuonekana kama "njia kipofu," Papa amesema wakumbushe wao kuwa tumaini la kikiristo ni kubwa zaidi ya hali yoyote, kwa sababu ina msingi wake katika Mungu(Mt 19, 26).
Baba Mtakatifu Francisko amependa kuwaeleza wote kwamba katika kazi ambayo wanajikita nayo katika Kanisa, “msiache kamwe kugundua kuwa kumsaidia mwathirika daima ni baraka, kwa sababu katika yeye ni Ufame wa Mungu (Mt 5,3). Kila mara tunapokuwa na fursa ya kuwakaribisha wao, na kuwatolea wao msaada wetu, ni fursa kwetu ya kugusa, mwili wa Kriso kwa sababu kupeleka Injili siyo jambo la kufikirika na ambalo linapunguzwa mafundisho ya kanisa, bali ni uthibitisho huo, katika ahadi ya Kikristo na wahitaji zaidi; hapo ndipo uinjilishaji wa kweli ulipo. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kwa ushuhuda wao wa maisha ya kikristo. Amewaomba wandeleea kuonesha tumaini, huruma na upendo kwa wato wengine ili kwa kuamini ukweli huu, wanaweza kuungana kwa ajili ya kushirikiana katika huduma ya maskini zaidi. Yesu aweze kuwabariki na Bikira Maria awalinde na tafadhali wasisahahu kumuombea.