Papa na Wanachama wa "Chama cha Utafiti wa Wakristo Waliofichwa" (Japan) Papa na Wanachama wa "Chama cha Utafiti wa Wakristo Waliofichwa" (Japan)  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa watafiti wa Kijapan:hata leo hii wengi wanakufa kwa jina la Yesu

Papa akikutana na wanachama wa Chama cha utafiti wa wakristo waliofichwa(Japan),waliofika Roma kwa ajili ya kuhiji,alikazia ahadi ya kulinda maneo ya Kikristo yaliyofichwa huko Nagasaki kuwa ni ushuhuda hai kwa uaminifu wa wengi ambao wamepitisha hazina ya imani kama urithi.Wazo la Papa kwa wanaoteseka katika hali za unyanyasaji na ukandamizwaji kwamba ni matunda machungu ya vita na mateso.Watu wa Japan ni watu waungwana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 30 Novemba 2024, amekuwa na furaha ya kukaribisha ujumbe wa  Wanachama wa "Chama cha Utafiti wa Wakristo Waliofichwa"kutoka Japan waliofika mjini Roma kwa ajili ya hija yao. Hawa walianza tafiti za kutafuta Maeneo ya Siri ya Kikristo huko Nagasaki na wako katika Orodha ya Urithi wa Dunia kwa mwaka 2018. Papa ameshukuru sana jitihada zao za kuhifadhi maeneo hayo kama ushuhuda wa thamani wa urithi mkubwa,  lakini ni sura iliyofichwa katika historia ya Kanisa la ulimwengu wote na ile ya watu wao watukufu.

Papa amependa kusisitiza kuwa, Wajapan ni watu waungwana. Ni matumaini ya Papa  kwamba utambuzi wa umuhimu wa maeneo hayo, pamoja na kuhakikisha uhifadhi wao wa kutosha, utakuwa pia ushuhuda hai wa uaminifu wa Wakristo wengi wa Japan, ambao wamepitisha hazina ya thamani ya imani kama urithi, kutoka katika kizazi kwa kizazi. Katika hiyo Papa Francisko aidha amesema: “Na nitakuwa na furaha ya kuunda Kardinali mwingine wa Kijapan mnamo 7 Desemba  2024.

Inafaa kwamba mkutano huo umefanyika katika fursa ya mkesha wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mtakatifu Francis Xavier, mmisionari mkuu ambaye aliota kwamba kuhubiriwa kwa Injili kutazaa mavuno mengi ya roho katika nchi yao ya asili. Kama warithi wa ndoto hiyo, Papa ameomba kazi yao ya elimu na uhifadhi ifanye sura hii mashuhuri katika historia ya uinjilishaji kujulikana na kuthaminiwa zaidi. Ziara ya kutembelea sehemu hizo za kihistoria ziwatumiwe kwa wafuasi wa Kristo, katika Japan ya leo, "kumbukumbu na moto ulio hai wa roho ya kila utume katika nchi hiyo, na uwezo wa kuendelea kupyaisha na kufanya bidii ya kueneza Injili(Salamu kwa tukio la 'heshima kwa mashahidi watakatifu, Nagasaki, 24 Novemba 2019).

Papa amesisitiza kuwa tunapofikiria ushujaa wa wamisionari wa kwanza, ujasiri wa wafia imani wa Japan na ustahimilivu wa jumuiya ndogo lakini yenye imani ya Kikatoliki ya nchi yenu, hatuwezi kukosa kuwafikiria ndugu zetu Wakristo ambao katika siku zetu wanateswa na kuangaika  hata kufa kwa jina la Yesu? Kwa hiyo Papa ameomba kuungana naye katika kuwaombea, na wale wanaoteseka kutokana na matunda machungu ya vita, vurugu, chuki na dhuluma. Tutegemee maombezi ya Mama Yetu, Mama wa Kanisa, na tuombe kwa bidii zaidi kwa ajili ya ujio wa Ufalme wa Kristo, Ufalme wa upatanisho wa ulimwengu wote, haki na amani.  Papa amewapa baraka zake kwa upendo na kuwahakikishia maombi yake.  Na tafadhali, wamwombee.

Hotuba ya Papa kwa Ujumbe kutoka Japan
30 November 2024, 10:54