Papa Francisko:Hatuwezi kuendelea katika mwelekeo huu tukiongozwa na ufanisi bila maono!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Fransisko Jumanne tarehe 5 Novemba 2024 amekutana na Jumuiya ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana katika maadhimisho ya Ufunguzi wa Mwaka wa Kitaaluma ( Dies Academicus). Mapema mwaka huu, Chuo Kikuu hiki cha Kipapa cha Gregorian na taasisi mashuhuri inayoendeshwa na Wajesuit iliyoanzishwa na Mtakatifu Ignatius katika karne ya 16 , iliunganishwa na taasisi za Kipapa za Kibiblia na ya Mashariki. Kwa njia hiyo katika mkutano huo ulikuwa na taasisi hizo mpya zilizounganishwa, ambapo Baba Mtakatifu ametoa lectio magistralis yaani mafundisho lakini marefu sana kwa, wafanyakazi na wanafunzi wote.
Katika hotuba yake, Papa alitafakari juu ya ishara ambayo mara moja ilining'inia kwenye mlango wa nyumba ya Wajesuit katikati ya karne ya 16 jijini Roma taasisi ambayo siku moja ingekuwa Chuo cha Kirumi na, baadaye, Chuo Kikuu cha Gregoriana. Ishara hiyo, Papa alisema, ilisomeka: "Shule ya sarufi, ubinadamu, na mafundisho ya Kikristo. Je, tunaweza kujifunza nini leo hii, Papa aliuliza, kutokana na ishara hiyo rahisi? Fundisho la kwanza, alipendekeza, linatokana na mchanganyiko wa masomo ambayo Wajesuit walitoa, wakichanganya sayansi ya kidini na wanadamu. Leo, alipendekeza, huu unatazamwa kama mwaliko wa kufanya sayansi ya kidini kuwa ya kibinadamu, kuwasha na kuhuisha tena cheche za neema katika kile ambacho ni mwanadamu.
Fundisho la pili, la Baba Mtakatifu alisema, linaweza kutolewa kutokana na ukweli kwamba masomo yalitolewa bure (kwa Kiitaliano ‘gratis’). Ni utovu huo, , ambao “unatufungua kwa mshangao wa Mungu … Papa Francisko pia alisisitiza umuhimu wa unyenyekevu katika elimu ya Kikatoliki. Kwa muda mrefu sana, sayansi takatifu ilidharau kila mtu mwingine, na mawazo ya sisi dhidi ya wengine, mbinu, ambayo ilisababisha makosa mengi," Papa alisema. Kwa sasa, aliongeza kuwa "ni wakati wa walimu katika Kanisa kuwa wanyenyekevu, kukiri kwamba hatujui kila kitu ..." Huu ni ulimwengu mgumu na utafiti unahitaji mchango wa kila mtu," Papa alisema. Kinachohitajika, Papa alihimiza, ni vyuo vikuu vyenye "tabaka chache, meza nyingi zaidi bega kwa bega - kila mtu ni mwombaji wa maarifa, huku akigusa majeraha ya historia.
Akitafakari juu ya muunganisho wa hivi karibuni wa taasisi nyingnie kwa Gregoriana, Papa alisema ametoa kibali chake kwa matumaini kwamba haitakuwa kesi ya "marekebisho ya kiutawala tu", bali liwe tukio la "kufafanua upya utume huo. Kuhusiana na hilo , Papa aliwaonya wafanyakazi wa chuo kikuu dhidi ya kujiwekea kikomo kwa "muunganisho, kusimamishwa na kufungwa" bila maono mapana ya kinachotokea ulimwenguni na Kanisa. Je, umejiuliza,” Papa alihoji, unakwenda wapi na kwa nini unafanya mambo unayofanya? Lazima ujue unakokwenda, na usipoteze upeo wa upeo.
Mwisho Baba Mtakatifu alitoa zawadi kwa wanachuo waliojipambanua na ubora wa mafunzo katika Chuo kikuu cha Kipapa cha Gregoriana.
Kama kawaida ya baba Mtakatifu, hasingeweza kutokutana na wanashirika wenzake ambao ndiyo wanajikita kupeleka mbele chuo Kikuu hiki kikubwa, kwa njia hiyo kabla ya kuondoka chuoni alikutana na Wajesuit.