Tafuta

2024.11.07 Papa amekutana na washiriki wa hija iliyaoandaliwa na masisita Aaagostinani wa Mtakatifu Ildefonso, ya Talavera de la Reina (Hispania). 2024.11.07 Papa amekutana na washiriki wa hija iliyaoandaliwa na masisita Aaagostinani wa Mtakatifu Ildefonso, ya Talavera de la Reina (Hispania).  (Vatican Media)

Papa na kundi la wanahija wa kiagostiniani:tukumbuke watu wasio na kazi na makazi!

Baba Mtakatifu amekutana tarehe 7 Novemba 2024 na Masista wa kiagostiniani wa Talavera de la Reina,Hispania,wakiwa katika hija jijini Roma kuadhimisha miaka 450 ya Shirika.Papa amewaalika watawa na mapadre kuthamini neema nyingi wanazofurahia kama sehemu ya jumuiya."Mkristo aliyechoka,Padre aliyechoka,mtawa aliyechoka anasikitisha.Msiwe asidi."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Alhamisi tarehe 7 Novemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Kikundi cha wanahija kinachohusiana na Monasteri ya Agostisiani ya Talavera de la Reina, nchini Hispania ambacho kimefika kwa ajili ya hija katika kukumbuka miaka 450 ya kuanzisha Konventi ya Shirika hilo, maadhimisho waliyoadhimisha 2023. Papa amesema tangu kuanzishwa kwake, monasteri hiyo imechanganya maisha ya kutafakari na huduma ya elimu ya Kikristo, na wengi wao labda walikutana na watawa hao wakati wa siku zao za shule. Katika mwaka huu uliowekwa wakfu kwa ajili ya sala,  Papa amesema inaonekana kwake  kuwa ni mfano muhimu wa jinsi ya huduma yetu na utume wetu-mbali na kutuzuia kukutana na Bwana ambapo lazima utoke kwake.

Papa Francisko amekutana na watawa wa monasteri moja ya Kiagostiniani kutoka Hispania
Papa Francisko amekutana na watawa wa monasteri moja ya Kiagostiniani kutoka Hispania

Kwa maana hiyo Papa ametamani kuwapa Baraka zake watawa hao wa kiagostiniani na kutoa mwaliko sio tu wa kumuombea, kama anavyoomba kwa kila mtu, lakini pia kuwa "kielelezo cha maisha ya ndani," kwamba wawe "walimu katika sanaa,  sala, ili kutoka shuleni, kati ya maarifa yote ambayo wanaweza kusambaza kwa watoto, wawe na uwezo wa kuzungumza na Mungu uonekane wazi, uwezo wa kumsikiliza, kuhisi yuko katika kila dakika ya maisha na kukubali maongozi yake kwa unyenyekevu." Papa ameongeza: “Na tafadhali msipoteze furaha yenu, msipoteze hisia zenu za ucheshi,“ Papa amewashauri. Kwa kuongezea Papa amesema “Wakati Mkristo, hata zaidi mwanamke wa kitawa anapoteza hisia zake za ucheshi, anakuwa siki.  Na inasikitisha sana kuona Padre, au  mtawa anakuwa asidi.” Kwa njia hiyo amewaonya "Msiwe kama siki, wala asidi."

Kwa njia hiyo ameshauri kwamba daima wawe na tabasamu na ucheshi mzuri.  Papa amewaomba wasali vizuri sana kutoka kwa Mtakatifu Thomas More, kila siku ili kuomba hali ya ucheshi. Hata hivyo Papa aliwauliza kama wanamfahamu. Walijibu hapana na akawaomba watafuta na kusoma historia yake. Papa akiendelea alisema: “Utakatifu ni furaha daima, kutoka katika maneno mazuri ya ucheshi ya Mtakatifu Philip Neri hadi maonesho ya ucheshi mzuri zaidi wa tahadhari, ambao ni tabasamu." Muwe na tabasamu linalotoka moyoni, ambalo sio la uwongo, ambalo huwa limejaa kila wakati.”

Papa akutana na wanahija kutoaka Hispania
Papa akutana na wanahija kutoaka Hispania

Wao kwa kuwa wanatoka Hispania, Papa Francisko amekumbuka kuwa : “Siku hizi niko karibu sana na Hispania kutokana na mkasa wa Valencia. Jana, katika Katekesi , tuliweka Sanamu ya (Virgen de los Desamparados) yaani ya  Bikira Maria wa Maskini. Wanateseka sana huko. Na sasa inaonekana Barcelona nao wana matatizo, lakini kwa vile wanajua kidogo jinsi ya kukabiliana na tatizo, wanajaribu, kudhibiti.” Papa ameongeza:  “Na hii inaniongoza kuwapa  ushauri mwingine wa  "kuona mahitaji ya wengine kila wakati. Je mnajua kuna watu hawana kazi? Na mtu anapokwenda kulalamika kwa sababu ana kazi nyingi, afikirie wale ambao hawana kazi.” Papa ameongeza kusema: "Kuna watu hawawezi kulipa kodi na wanafukuzwa. Mtu anapoingia kwenye nyumba ya watawa, nyumba ya parokia, afikirie haya yote kwamba anayapata bure."  Papa ameongeza kwamba: "Wakati mtu anakaa katika nyumba yake ya parokia, katika nyumba ya watawa, na analindwa vyema siku za theluji na mvua, afikirie kwamba kuna watu wanaolala nje, bila chochote na hawana cha kujifunika."

Masisita Waagositiani wa Hispania wakutana na Papa
Masisita Waagositiani wa Hispania wakutana na Papa

Zaidi ya yote Papa Francisko amewasahuru kwamba "Lakini msipoteze hali yenu nzuri. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo alisema atawasomea sala ya Mtakatifu Thomas More,  ambapo amewashauri  wajifunze na kusali kila siku. Mtakatifu Thomas More anasema hivi: “Ee Bwana, nipe usagaji mzuri wa chakula na pia kitu cha kusagia. Nipe afya ya mwili, na ucheshi mzuri unaohitajika kuudumisha. Nipe, ee Bwana, roho mtakatifu, ambaye huhifadhi mema na usafi, ili niogope dhambi, lakini nije mbele yako na kupata  njia ya kurekebisha tena. Nipe roho ambayo haijui kuchoka.” Kwani Papa ameongeza kusema: 'Mkristo aliyechoka, Padre aliyechoka, mtawa aliyechoka anasikitisha,' akiendelea amesema roho “isiyojua kuchoka, kunung'unika, kulia na kuomboleza, na usiniruhusu nihangaike kupita kiasi" na  juu ya hilo, Papa ameongeza kuna kitu kinachoingilia sana kinachoitwa 'umimi.' Papa amendelea na sala: Nipe, ee Bwana, hali ya ucheshi, nipe neema ya kuelewa uchesi, ili nipate kujua furaha kidogo maishani na niweze kushiriki na wengine " na kwa hiyo "pia iwe hivyo,” Papa amehitimisha na kuwabariki.

Papa alikutana na wanahija kutoka Hispania
07 November 2024, 16:15