Tafuta

 Papa na Patriaki wa Ashuru  Mar Awa III alipomtembelea.tarehe 9 Novemba 2024anatarajiwa kurudi tena. Papa na Patriaki wa Ashuru Mar Awa III alipomtembelea.tarehe 9 Novemba 2024anatarajiwa kurudi tena.  (ANSA)

Papa na Patriaki Mar Awa III wa Ashuru wataadhimisha kumbukumbu ya miaka 30 ya Azimio la Pamoja!

tarehe 9 Novemba 2024 Patriaki wa Kanisa la Wakatoliki wa Ashuru ya Mashariki atamtembelea Papa Francisko mjini Vatican kwa ajili ya kumbukumbu ya hati ya kiekumene.Na kumbukizi ya miaka 40 ya ziara ya kwanza ya Roma ya Patriaki wa Ashuru kwa Mtakatifu Yohane Paulo II.

Vatican News

Ilikuwa mnamo tarehe 11 Novemba 1994 wakati  Mtakatifu Yohane Paulo II  na Patriaki wa Kikatoliki wa wakati huo wa Kanisa la Ashuru la Mashariki, Patriaki Mar Dinkha IV, walipotia saini Azimio la pamoja la Kikristo ambalo liliidhinisha, kama tunavyosoma katika kifungu hicho, "hatua ya msingi kwenye njia ya  kuelekea ushirika kamili” kati ya jumuiya za Kikatoliki na za Mashariki.

Sherehe ya kumbukumbu

Miaka 30 baada ya tukio hilo, tarehe 9 Novemba 2024, Baba Mtakatifu, Francisko na Patriaki wa Wakatoliki wa Ashuru Mar Awa III wanatarajiwa kuwa pamoja mjini Vatican kwa ajili ya maadhimisho ya mwaka huu, ambayo pia yanahusishwa na maadhimisho ya awamu ya pili ya miaka 40 tangu ziara ya kwanza ya  jijini Roma ya Patriaki wa Ashuru - yaani, Mar Dinkha IV yuleyule ambaye pamoja na Papa Yohane Paulo II  alikuwa ameanzisha kazi ya Tume ya Pamoja ya Majadiliano ya Kitaalimungu  kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Ashuru la Mashariki. Na watakuwa baadhi ya wajumbe wa Tume mchanganyiko ambao watasindikiza ziara ya Baba wa Taifa Mar Awa III kwa  Papa Francisko, Jumamosi tarehe 9 Novemba 2024  , kama ilivyoelezwa na barua kutoka Baraza la Kipapa la kuhamasisha wa Umoja wa Kikiristo, ambalo linasisitiza kwamba kazi ya Tume imeanza hivi karibuni ya awamu mpya ya majadiliano juu ya liturujia katika maisha ya Kanisa".

Azimio la 1994

"Bila kujali tofauti za Kikristo ambazo zimekuwepo - tunasoma katika kifungu cha Azimio la '94 - leo tunakiri kwa umoja imani ile ile katika Mwana wa Mungu aliyefanyika mwanadamu ili sisi, kwa neema yake, tupate kuwa watoto wa Mungu." Aidha taarifa inabainisha kuwa "Imani na kuaminiana ambayo tayari ipo kati ya Makanisa yetu  inatuidhinisha kuanzia sasa na kuendelea kufikiria jinsi inavyowezekana kushuhudia ujumbe wa kiinjili kwa pamoja na kushirikiana katika hali fulani za kichungaji, ikiwa ni pamoja kwa namna maalumu " katika uwanja wa katekesi na mafunzo ya mapadre wa siku zijazo," kinahitimisha kifungu  cha taarifa hiyo kutoka Baraza usika.

08 November 2024, 14:53