2024.10.27 SMisa ya hitimisho la Sinodi ya Maaskofu Oktoba 2024. 2024.10.27 SMisa ya hitimisho la Sinodi ya Maaskofu Oktoba 2024.  (Vatican Media)

Papa na Sinodi ya Maaskofu:Hati ya mwisho ya Sinodi ni sehemu ya Majisterio

Papa Francisko alichapisha barua ya kuambatanisha na Hati ya Mwisho ya Sinodi ya Maaskofu.Ndani mwake anakabidhi Waraka kwa Kanisa na kutoa wito kwa utekelezaji wa ubunifu na kujitolea upya kwa ushirika,ushiriki na utume

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameandika barua  yake inayoambatana na Hati ya Mwisho ya Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, maandishi ambayo yanachukua matokeo ya Sinodi ya Maaskofu wa Sinodi ya miaka miwili ambayo Baba Mtakatifu Francisko aliitaka kuanzia mwezi Oktoba 2021 na kuhitimishwa mnamo Oktoba 2024. Katika maandishi yanayoambatana na Hati hiyo, Papa Francisko anaandika kwamba tangu kuanzishwa  kwake,  njia ya Sinodi imekuwa na sifa ya uwazi kwa sauti ya Roho Mtakatifu. Roho hii imeongoza Kanisa katika mabara, lugha, na tamaduni. "Safari hii," Papa Francisko anaandika, kuwa imeliruhusu Kanisa kusoma uzoefu wake mwenyewe na kutambua hatua za kuishi ushirika, kutambua ushiriki, na kuendeleza utume uliokabidhiwa kwake na Kristo."

Safari ya Kisinodi ilianzia katika ngazi mahalia

Papa anaeleza jinsi ambavyo safari hii ya sinodi ilianza hasa katika ngazi mahalia  ikipitia awamu za kitaifa na bara. Kwa kuwa Mkutano Mkuu  ulihitimishwa, Baba Mtakatifu Francisko anakabidhi Hati ya Mwisho na yaliyomo ndani ya Makanisa mahalia, ambayo anayaalika kutekeleza yaliyomo katika Hati hiyo kwa utambuzi, ubunifu, na heshima kwa mazingira yao ya kipekee. Kisha Papa Francisko anafafanua zaidi kwamba “Hati hiyo kama sehemu ya Magisterium ya kawaida ya Mrithi wa Petro na anaomba  kwamba asili yake ya mamlaka iheshimiwe hivyo.” Na kwamba “Inawakilisha namna ya kutekeleza mafundisho ya kweli ya Askofu wa Roma, huku, akiongeza kuwa kuwa ina mambo ya mambo mapya lakini inaendana na yale aliyofafanua mnamo tarehe 17  Oktoba  2015, “niliposema kuwa sinodi ndio tafsiri sahihi,  mfumo wa kuelewa huduma ya uongozi.” Hata hivyo, anafafanua kuwa “ Hati si ya kawaida kabisa bali ni wito wa kutafakari unaotumika kwa njia tofauti katika kila muktadha.”

Mkutano Mkuu wa Sinodi hauishii na Sinodi;mwanzo wa utekelezaji katika makanisa

Pia anabainisha kwamba hitimisho la Mkutano Mkuu wa Kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu siyo mwisho wa mchakato wa sinodi. Badala yake, linaashiria mwanzo wa awamu ya utekelezaji, na Makanisa mahalia na makundi yao sasa yameitwa kutekeleza, katika miktadha tofauti, maelekezo ya kimamlaka yaliyo katika Hati kwa njia ya utambuzi na michakato ya kufanya maamuzi iliyotabiriwa na sheria ya kanuni na Hati yenyewe. Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo anaendelea kuikabidhi Sekretarieti kuu ya Sinodi na Mabaraza ya Kipapa la Curia Romana jukumu la kusindikiza  Makanisa mahalia yanapofanya kazi ya kutekeleza vyema dira ya Sinodi.

Kwa waamini:safari ya Sinodi inahitaji maneno na matendo

Maaskofu, pia, watatoa taarifa juu ya chaguzi zilizofanywa katika Kanisa lao la mahalia kuhusu ishara zake katika Hati ya Mwisho, matatizo yaliyopatikana, na matunda yaliyopatikana, na wanaitwa kuripoti maendeleo wakati wa ziara zao za kitume (ad limina), wakishirikisha  changamoto na matunda ya juhudi zao. Papa aidha anawahimiza maaskofu kukaribia awamu hii kwa ujasiri, ubunifu, na unyenyekevu, akisisitiza  kwamba itachukua muda kushughulikia masuala fulani ambayo yanahitaji maridhiano katika Kanisa la kimataifa. Akitoa maelezo yake kwa karibu zaidi  Baba Mtakatifu anawakumbusha waamini wote kwamba safari ya sinodi inahitaji maneno ya pamoja ili yaambatane na matendo, na ni matumaini yake kwamba Roho Mtakatifu, kama maelewano ya Kanisa, ataendelea kupyaisha na pyaishwa kwa kuongozwa ili kufika kwenye  ushirika kamili na Kristo.

Barua ya Papa kusindikiza hati ya mwisho wa Sinodi
26 November 2024, 15:13