2024.11.11 Papa amekutana na Uwakilishi wa wamafundi na washirika wa Kiwanda cha Mtakatifu Petro. 2024.11.11 Papa amekutana na Uwakilishi wa wamafundi na washirika wa Kiwanda cha Mtakatifu Petro.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa na mafundi na washirika wa kiwanda cha Mtakatifu Petro:Wambie waungamishi wasamehe!

Papa akikutana na mafundi na washirika wa kiwanda cha Mtakatifu Petro,Novemba 11,alisema:“tukumbuke kwamba kiini cha asili cha Basilika ni Kaburi la Petro, mfuasi ambaye Bwana Yesu alimchagua kuwa wa kwanza kati ya Mitume,akimkabidhi funguo za Ufalme wa mbinguni.Kwa hiyo amekazia mada tatu:"kussali sala,mtazamo wa imani na mguso wa mahujaji.Hebu hisia hizi za kimwili na za kiroho, ziamuru kwa akili mipango ya kutekelezwa."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu FranciskoJumatatu tarehe 11 Novemba 2024 amekutana na mafundi wataalamu na washirika wa kiwanda cha Mtakatifu Petro. “Ninawasalimu kwa shukrani, kwa sababu ziara yenu inathibitisha bidii mnayotumia kuzindua mipango  mipya na ushirikiano kwa manufaa ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.” Alisimulia Papa Francisko  siku moja alivyokwenda kuona wanachofanya na kuwa ni vizuri sana. “Nyumba hii ya sala kwa watu wote (taz. Isa 56:7; Mt 21:13) ilikabidhiwa kwetu na wale waliotutangulia katika imani na katika huduma ya kitume. Kwa hiyo ni zawadi na kazi ya kuitunza, katika hali ya kiroho na kimwili, hata kupitia teknolojia za hivi karibuni.”

Zana hizi hasa changamoto ubunifu wetu na wajibu wetu. Kiukweli, matumizi sahihi na yenye kujenga ya uwezo ambao hakika ni muhimu, lakini usio na utata, unategemea sisi. Wakati mwingine hutokea kwamba chombo kinapuuza madhumuni ambayo yanapaswa kutumika: ni kana kwamba sura inakuwa muhimu zaidi kuliko uchoraji. Kwa hiyo “ni muhimu kutawala teknolojia, kukumbuka kwamba bidhaa zake ni nzuri tu ikiwa  zinafanya kazi vizuri, lakini juu ya yote wakati zinatusaidia kukua. Hili ndilo kusudi,” Papa alisisitiza. Kanuni hii ni halali zaidi kwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kwa maingiliano mbalimbali yanayohitajika, ili kwa wageni wote wapate mahali pa kuishi kwa imani na historia, nyumba ya ukarimu, hekalu la kukutana na Mungu na ndugu ambao kuja Roma kutoka duniani kote. Kila mtu, lazima ajisikie kukaribishwa katika nyumba hii kuu: wale walio na imani na wale wanaotafuta imani; wale wanaokuja kutafakari uzuri mwingi wa kisanii wa Roma na wale wanaotaka kufafanua kanuni zake za kiutamaduni.”

Tukumbuke kiini cha Basilika ni Kaburi la Petro

Kwa njia jiyo Papa Francisko amesisitiza “tukumbuke kwamba kiini cha asili cha Basilika ni Kaburi la Petro, mfuasi ambaye Bwana Yesu alimchagua kuwa wa kwanza kati ya Mitume, akimkabidhi funguo za Ufalme wa mbinguni (rej. Mt 16:18).  Hili linadhihirishwa na maandishi makubwa ya Kigiriki na Kilatini yanayoambatana na waamini kutoka juu hadi kwenye madhabahu ya Kiti.” Na “Kazi zilizopangwa lazima ziwe na madhumuni sawa: kusindikizana  na wanaume na wanawake wa leo hii; kuunga mkono safari yao kama wanafunzi, kwa kufuata mfano wa Simoni Petro.” Papa Francisko akiendelea alibanisha hasa kuwaachia vigezo vitatu vya kuongoza kazi yao ambavyo ni: “kusali sala, mtazamo wa imani, na mguso wa mahujaji.” Hebu hisia hizi, za kimwili na za kiroho, ziamuru kwa akili mipango ya kutekelezwa,” Papa alikazia.  

Kusali sala, mtazamo wa imani na mguso wa mahujaji

Kwanza kabisa, kusali sala: “Ninahimiza kujitolea kwa Kiwanda na washiriki wake katika kupitishwa kwa teknolojia zinazohimiza sio tu ushiriki wa mwingiliano wa watu, lakini juu ya yote ufahamu wao wa mahali patakatifu, ambayo ni nafasi ya kutafakari.” Pili, Papa Francisko alisema “mtazamo wa imani, kutumia zana za kisasa kwa mtindo wa kimisionari, usio wa kitalii, bila kutafuta mvuto wa athari maalum, lakini badala yake kuwekeza katika njia mpya za kuiambia imani ya Kanisa na tamaduni ambayo imeunda.” Na Hatimaye, ya tatu ni mguso wa Hija: ambapo Papa alisema “kwa karne nyingi, sanaa za uchongaji, picha na usanifu zimewekwa kwa huduma ya watu wa Mungu kwa kutumia teknolojia bora zaidi za wakati huo. Watangulizi wetu walifanya ajabu! Kila mradi mpya lazima uwe katika mwendelezo na nia ile ile ya kichungaji.”

Kusamehe daima 

Papa alieleza kuwa kuna kazi nyingine ya kisanii ambayo pia inaendeshwa katika Basilika, ambayo imejificha yaani kuungamisha. “Tafadhali waungamishi wawepo daima kwa ajili ya kuungamisha. Watu wanakwenda, wanasikia chochote, hata wale wasio wakatoliki wanakaribia ili kuomba baraka… Pamoja na namna hiyo ya kisanii na nzuri, kuna hata sanaa ya mawasiliano binafsi. Tafadhali wambie waungamishi, wasamehe yote! Kila kitu husamehewa. Bwana anataka hili na siyo kufanya hotuba. “Wewe unapaswa…”Hapana hakuna cha unapaswa.”… Ninakusamehe na uende mbele za Bwana. Semehe na siyo kuhubiri; unaweza kusema neno, lakini kusamehe na ili pasiwepo anayekwenda nje bila baraka.” Papa Francisko akikazia juu ya msamaha amefafanua kuwa “ Hata wale wasio kuwa wakristo, wananiambia waungamishi kuwa mara nyingi ni waislamu au wa dini nyingine, wanakaribia kuomba baraka. Muwapatia baraka daima wote na wale ambao wanataka kuungama wasemaheni wote.” Papa amehitimisha kwa kuwashukuru kufika kwao na kwa moyo amewabariki na kazi zao. Amewaomba tafadhali wasali kwa ajili yake.

Papa akutana na wataalamu wa kiwanda cha Mtakatifu Petro

 

11 November 2024, 15:41