Tafuta

2024.11.15  Papa akutana na Wajumbe wa Shirikisho la Kitaifa la Ufundi na Biashara Ndogo na za Kati nchini Italia. 2024.11.15 Papa akutana na Wajumbe wa Shirikisho la Kitaifa la Ufundi na Biashara Ndogo na za Kati nchini Italia.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Tunaishi nyakati za vita na vurugu.Kuipamba dunia ni kujenga amani!

Baba Mtakatiru akikutana na wawakilishi wa biashara ndogo na za kati nchini Italia aliwahimiza kujiweka katika huduma kwa manufaa ya wote akikumbusha kwamba wakati wa vita na vurugu kuna hatari ya kupoteza imani katika uwezo wa wanadamu.Kwa kutazama shughuli zao zinatufariji na kutoa matumaini.Ametoa onyo dhidi ya utengenezaji wa silaha zinazoua.

Na Agella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 15 Novemba 2024 amekutana na wawakilishi wa Shirikisisho la Kitaifa la Ufundi na Biashara Ndogo na za Kati, ambapo amewakaribisha na kuwasalimi kuanzia kwa  Rais na wanachama wote wa chama hicho  cha wafanya biashara, kilichoenea nchini Italia. Papa amesema anapenda sana ufundi kwa sababu unaonesha thamani ya kazi ya binadamu vizuri. Tunapounda kwa mikono yetu, wakati huo huo tunainua kichwa na miguu yetu: kufanya daima ni matunda ya mawazo na harakati kuelekea wengine. Ufundi ni sifa kwa ubunifu; kiukweli, fundi lazima awe na uwezo wa kuona umbo fulani katika jambo lisilo na maana ambalo wengine hawawezi kutambua. Na hii inawafanya wao kuwa washiriki katika kazi ya uumbaji ya Mungu na kwamba  “Tunahitaji talanta yao ili kutoa maana kwa shughuli za binadamu na kuiweka katika huduma ya mipango  inayokuza manufaa ya wote.”

Hofu na uvivu ya kutozalisha talanta nyingine

Papa amerudia  katika kifungu maarufu cha Injili cha  mfano wa talanta (rej. Mt 25:14-30). Bwana aliwapa watumishi watatu talanta ili kuzitumia. Aliyepokea tano alionekana kuwa na uwezo na kupata tano zaidi. Aliyepokea mbili alifanya vivyo hivyo na kupata mbili zaidi. Wote wawili walisifiwa na bwana sawa. Kwa njia hiyo Papa alisema kuwa “ Sio wingi unaohesabika, bali kujitolea, na kinachozingatiwa ni kili cha kujitolea kufanya zawadi zilizopokelewa ili kuzaa matunda.  Na ndicho hasa  kile kinachokosekana kutoka katika mtumishi wa tatu, ambaye alificha talanta yake chini ya ardhi kwa hofu na uvivu. Aliachana na ujanja kwa sababu hakukuza uhusiano wa uaminifu wa bwana wake wa kuelekea maisha, na kwa wengine. Kwa hiyo alikosa Uhusiano wa uaminifu na wengine.

Tunachopokea au kupata zi matokeo ya uwezo wetu

Mfano huu ni wimbo wa kumwamini Mungu, na mwaliko wa "ushirikiano" wenye afya na chanya. Katika hilo, Papa ameomba ruhusa kusema neno tena la "ushirikiano" na Mungu, ambaye hutufanya washiriki katika mali yake na anazingazitia, kuhusu wajibu wetu. Ukitaka kukua kimaisha unahitaji kuachana na woga na kuwa na imani.” Wakati fulani, hasa matatizo yanapoongezeka, tunajaribiwa kufikiri kwamba Bwana ni msuluhishi au mtawala asiyechoka badala ya Yule anayetutia moyo kuchukua uhai mikononi mwetu wenyewe. Lakini Injili daima inatualika tuwe na mtazamo wa imani; tusifikiri kwamba kile tunachopata ni matokeo ya uwezo wetu tu au sifa zetu.” “Pia ni matunda ya historia ya kila mmoja wetu, ni matunda ya watu wengi waliotufundisha kusonga mbele kimaisha tukianzia kwa wazazi wetu.

Tuishi kama washiriki wa Mpango mkuu wa Mungu

Papa amesisitiza kuwa tufikiri kwamba “Kazi tunayofanya ni matokeo ya historia, ambayo imetufanya kuwa na uwezo wa kufanya hivi." Kwa hiyo wao  pia, ikiwa wana shauku juu ya kazi yao, na ikiwa wakati mwingine wanalalamika kwa usahihi kwa sababu hawatambuliki vya kutosha, ni kwa sababu wanafahamu thamani ya kile ambacho Mungu ameweka mikononi mwao, si kwa ajili yao tu bali kwa kila mtu. Sote tunapaswa kuweka kando woga unaolemaza na kuharibu ubunifu. Tunaweza pia kufanya hivi kwa jinsi tunavyoishi kazi yetu ya kila siku, tukihisi kama sisi ni washiriki katika mpango mkuu wa Mungu, wenye uwezo wa kutushangaza kwa zawadi zake.

Vitega uchumi vinavyoua haipendezi

Nyuma ya utajiri wetu hakuna ujuzi tu, bali pia Mpaji ambaye anatuchukua kwa mkono na kutuongoza. Ufundi waweza kueleza haya yote vizuri, ikiwa unaambatana siku baada ya siku na ufahamu kwamba Mungu hatutupi kamwe, kwamba sisi ni kazi bora za mikononi mwake, na kwa sababu hiyo tunaweza kuumba kazi za asili. Pia amependa kupongeza kazi yao kwa sababu inapamba ulimwengu. Tunaishi nyakati za vita na vurugu... Kila mahali habari ziko hivi, na inaonekana kutufanya tupoteze imani katika uwezo wa wanadamu, tukitazama shughuli zao hutufariji na kutupa tumaini. Kuipamba dunia ni kujenga amani. "Mwanauchumi aliniambia kuwa vitega uchumi vinavyozalisha mapato mengi zaidi leo, nchini Italia, ni viwanda vya kutengeneza silaha... Hii haipendezi dunia, ni mbaya. Ukitaka kupata zaidi lazima uwekeze kuua. Hebu tufikirie hili. Msisahau – ninarudia kusema  tena – kuipamba dunia ni kujenga amani.”

Uharibifu ni kuongeza uadui kwa Mungu

Katika Waraka wa Fratelli Tutti (Wote ni Ndugu, imefafanua wajenzi wa amani kama mafundishi wenye uwezo wa kuanzisha mchakato wa kurudisha na wa kukutana na ugwiji na shauku (225). Na wakati huo huo ugwiji na shauku ambayo wanayo waitumie kutekekeza kazi nyingi zenye hatma ya kutajirisha Ulimwengu. Na Mungu huwaita wote wanawake na wanawaume kufanya kazi kwa namna ya ufundi, kama Yeye na kufanya kazi katika mpango huo wa amani alio nayo. Kwa njia hiyo Yeye ugawanya kwa wingi talanta zake, ili ziweze kuwekwa katika huduma za maisha na zisiishie kuwa tasa za vifo na uharibifu, kama vita ifanyavyo  kwa kuongeza uadui kwa Mungu. Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kwa kile ambacho wanatarajia kutekeleza kupitia kazi yao; amewashukuru hata kwa jitihada za kijamii; hata hiyo ni kazi ambayo inahitaji uvumilivu, inahitaji pia mpangilio. Mtakatifu Yosefu fundi seremala awahuishe daima kuishi kazi kwa ubunifu na ari. Kwa moyo wote Papa amewabariki na familia zao. Amewaomba tafadhali wasisahau kusali kwa ajili yake.

15 November 2024, 12:14