Papa:Marekebisho ya mfumo wa Mfuko wa Pensheni na usimamizi wa sasa yanahitajika
Vatican News
Hatua za haraka za kimuundo, ambazo haziwezi kuahirishwa tena katika Mfuko wa Pensheni, ili kufikia uendelevu na kuhakikisha utoaji wa pensheni kwa vizazi vijavyo, ni jambo ambalo kwa sasa haliwezi kudhamini katika muda wa kati. Mfumo wa sasa unazalisha upungufu mkubwa.” Baada ya barua ya Septemba 16 kwa Makardinali wote kushirikiana kwa ajili ya utekelezaji wa kina zaidi wa mageuzi ya kiuchumi ili kufikia lengo la upungufu sifuri, Baba Mtakatifu Francisko alituma barua mpya kuomba juhudi zaidi na hata kuomba kufanya sadaka, katika wakati huu wa kuomba marekebisho ya Mfuko wa Pensheni. Hata hivyo tayari mnamo mwezi Machi 2024, Papa Francisko, kwa barua ya mkono binafasi ya Motu Proprio, alikuwa amerekebisha Kanuni na, hata kabla ya hapo, mnamo 2015 alikuwa amefanya marekebisho ya kina ya Kitaasisi.
Katika barua aliyoiandikwa kwa Baraza la Makardinali, wenyeviti wa Mabaraza ya Kipapa na wakuu wa Taasisi za Curia Romana pamoja na Taasisi zinazofungamana na Makao makuu ya Vatican anaomba usimamizi bora wa muundo huu ambao umekuwa mada ya "wasiwasi" tangu kuanzishwa kwake (hili lilikuwa jina la Motu Proprio iliyoianzisha mwaka 1992) ya Mapapa waliotangulia na kitovu cha mageuzi ya kiuchumi. Kile ambacho katika barua iliyotajwa hapo juu ya Septemba, Papa Bergoglio aliandika, kilikuwa mojawapo ya mada kuu za Mikutano kabla ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wake.
Kardinali Farrell ndiye msimamizi pekee mfuko wa hazina
Zaidi ya hayo, katika barua hiyo hiyo - iliyotiwa saini tarehe 19 Novemba 2’24 lakini iliyotolewa tarehe 21 Novemba 2024 , Papa alitangaza uamuzi wa kumteua Kardinali Kevin Farrell - ambaye kwa sasa pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, , camerlengo Kanisa Takatifu la Roma, rais wa Tume ya Mambo Yaliyohifadhiwa na Kamati ya Uwekezaji - kama mkurugenzi pekee wa Mfuko wa hazina ya Pensheni. Chaguo, hilo kwa maelezo ya Papa, ambayo kwa wakati huu yanawakilisha "hatua muhimu ya kukabiliana na changamoto ambazo mfumo wetu wa usalama wa hazina unapaswa kukabiliana nao katika siku zijazo".
Sio maamuzi rahisi na kujitolea
Katika waraka huo, Papa Francisko anakumbusha kwamba kipindi cha sasa kinajulikana na "matatizo makubwa na magumu ambayo yanaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hayatashughulikiwa mara moja." Kwa hivyo, hatua za haraka zinahitajika ambazo zinahusisha "maamuzi si rahisi ambayo yatahitaji usikivu fulani, ukarimu na nia ya kujitolea kutoka kwa kila mtu"
Uchunguzi na uchambuzi
Baada ya muda tayari kumekuwa na watu ambao wamechunguza jambo hili na "wamehuishwa kwa uwajibikaji na wasiwasi ili kuhakikisha mfano wa usalama wa hazina wa haki kwa ajili ya jumuiya katika huduma ya Vatican na Mji mzima wa Vaican na kutimiza wajibu wa kimaadili wa kutoa mafao ya heshima kwa wale walio na haki nayo, sambamba na rasilimali za kiuchumi zilizopo", anasisitiza Papa. Kwa kusudi hilo. tafiti mbalimbali zimefanyika ambayo iliibuka kuwa "usimamizi wa sasa wa pensheni, kwa kuzingatia mali zilizopo, hutoa upungufu mkubwa." Uchambuzi wa kina zaidi, uliofanywa na wataalam wa kujitegemea, unaonesha ukweli mwingine, ambao ni "kukosekana kwa usawa kwa Hazina, ambayo ukubwa wake unaelekea kupanuka kwa muda bila kukosekana usawa". Kwa maneno mengine, Papa Francisko anasisitiza kuwa "ina maana kwamba mfumo wa sasa hauwezi kuhakikisha utimilifu wa wajibu wa pensheni kwa vizazi vijavyo katika muda wa kati".
Usawa kati ya vizazi
Kwa hiyo Papa Francisko anaomba "hatua za haraka za kimuundo", bila kuahirishwa, ili kufikia uendelevu wa Mfuko wa Pensheni "katika muktadha wa jumla wa rasilimali ndogo zinazopatikana za shirika zima". Sambamba na hilo, "kifuniko kifaacho cha hazina hifadhi kwa wafanyakazi wa sasa na wa baadaye kinahitajika haraka, kwa nia ya haki na usawa kati ya vizazi tofauti".
Mabadiliko mapya na yasiyoepukika
"Licha ya kuthamini mchango uliotolewa kwa uangalifu na wale ambao wameshughulikia suala hili dhaifu katika miaka ya hivi karibuni, sasa ninaamini kuwa ni muhimu kupitia hatua hii mpya, ya msingi kwa utulivu na ustawi wa hazina yetu, kwa haraka na umoja wa maono ili hatua zinazohitajika zifanyike mara moja." Francisko katika hitimisho la barua hiyo anaomba kila mtu ushirikiano maalum katika kuwezesha njia hii "mpya na isiyoepukika" ya mabadiliko.