2024.11.08 Papa alitembelea Pompei  21-03-2015 na kusali mbele ya picha ya Mama wa Rozari. 2024.11.08 Papa alitembelea Pompei 21-03-2015 na kusali mbele ya picha ya Mama wa Rozari. 

Papa:Sala ya Rozari ni chombo rahisi ili kusaidia Unjilishaji wa Kanisa leo hii!

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa Msimamizi wa Madhabahu ya Bikira Maria wa Rozari huko Pompei katika fursa ya kuadhimisha mwaka wa Jubilei ya kumbukumbu ya miaka 150 ya kuwasili kwa Picha ya Bikira ambayo Bartolo Longo alitaka iwafikie watu wa Pompei na kueneza ibada ya Mama wa Mbinguni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 10 Novemba 2024 ametoa wito wa kugundua upya uwezo wa kusali Rozari ya kuinjilisha Kanisa, katika barua yake ya aliyomtumia Msimamizi wa Madhabahu ya Bikira Maria huko Pompei, Askofu Mkuu Thomas Kaputo katika kuadhimisha miaka 150 tangu picha ya Mama Yetu wa Rozari ulipowasili katika Madhabahu ya Pompei nchini  Italia. Rozari, ni chombo rahisi kinachoweza kufikiwa na kila mtu, kinaweza kuunga mkono uinjilishaji mpya ambao Kanisa linaitwa kufanya leo. Jumuiya ya kikanisa huko Pompei inajiandaa kusherehekea Mwaka wa Jubilei kwa mipango mbalimbali ya kichungaji, katika kumbukizi hii ya miaka 150 ya kuwasili kwa Picha ya  kuheshimiwa, ya Mama Yetu wa Rozari. Kwa njia hiyo katika ujumbe wa Baba Mtakatifu anabainisha kwamba anaungana kiroho na wale wote watakaoadhimisha tukio hili muhimu na atakuwa nao  katika kumbukumbu ya sala katika madhabahu ya  Maria wa Pompei, ili kupata faraja na matumaini katika uso mtamu wa Mama wa Mbinguni.

Jubilei ya 2025 na 1700

Papa aisisitiza kuwa kipindi cha kumbukizi ya  uchoraji wa Mama Yetu wa Pompeii kifanane na Mwaka wa Jubilei inaoyokaribia, kwa kuzingatia Yesu tumaini letu, na maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nikea, ambayo ilitiliwa mkazo maalum Juu ya Fumbo la Mungu kuwa Binadamu katika Kristo kwa nuru ya  Utatu. Papa anandika kuwa “Ni ajabu kugundua tena Rozari katika mtazamo huu, kuingiza mafumbo ya maisha ya Mwokozi, kuyatafakari kwa mtazamo wa Maria. Rozari, kama chombo rahisi kufikiwa na kila mtu, inaweza kusaidia uinjilishaji mpya ambao Kanisa linaitwa leo kufanya.” Papa alisisitiza jinsi ilivyo muhimu kugundua tena uzuri wa Rozari ndani ya familia na nyumba. “Sio tu kwamba maombi haya yanasaidia katika kujenga amani, bali pia Papa alisisitiza jinsi ilivyo muhimu “kupendekeza kwa vijana ili wasiweze kuiona kama inayorudiwa na kuchukiza, lakini kama tendo la upendo ambalo halichoshi kujimwaga yenyewe.”

Kujitolea upya kupitia mipango ya kihistoria

Zaidi ya hayo, Rozari, pia ni chanzo cha faraja kwa wagonjwa na wanaoteseka, Papa alisema "mnyororo mtamu unaotufunga sisi kwa Mungu, lakini pia mnyororo wa upendo ambao unakuwa wa kukumbatiwa kwa walio wadogo na waliotengwa, kama  Bartolo Longo alivyoona hasa katika watoto yatima na watoto wa wafungwa." Kwa kuzingatia hili, Papa aliwahimiza wale wanaoadhimisha kumbukumbu hiyo kuendelea na kujitolea upya, kupitia mipango mingi ya Madhabahu hiyo, historia kuu ya upendo ambayo alianzisha.

Urithi wa Mwenyeheri Bartolo Longo

Ni urithi mzuri zaidi wa kiroho, Papa Francisko alisisitiza, na ambao Mwanzilishi Mwenyeheri Bartolo Longo aliacha nyuma.  Baba Mtakatifu Francisko aliendelea kuandika kuwa, anasali kwamba Bwana, kupitia ujumbe wa Mama Yetu wa Pompei, aendelee kuzungumza na wanadamu wa leo wanaohitaji kugundua upya njia ya maelewano na udugu. Pia alionesha matumaini yake kwamba watu wengi wanafanya ibada kwake waliotawanyika ulimwenguni pote watashikamana sikuzote kwa uaminifu zaidi na Bwana, wakitoa ushuhuda wa ukaribu kwa kaka na dada zao, hasa walio na uhitaji zaidi.

Pabarua ya Papa kwa fursa ya maadhimisho huko Pompei
10 November 2024, 15:45