Tafuta

Papa atakula chakula cha mchana na maskini tarehe 17 Novemba 2024. Papa atakula chakula cha mchana na maskini tarehe 17 Novemba 2024.  (Vatican Media)

Siku ya Maskini Ulimwenguni:Papa Francisko anaandaa chakula cha mchana na maskini 1300

Kama ilivyotolewa maelezo,Baba Mtakatifu Francisko ataadhimisha Siku ya 8 ya Maskini Duniani pamoja na baadhi ya watu maskini wa Roma ambao watajumuika naye kwa chakula cha mchana mara baada ya misa takatifu tarehe 17 Novemba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Imekuwa desturi sasa ya Baba Mtakatifu kuwa na Chakula cha mchana na baadhi ya watu maskini wa Roma katika siku ya Mama Kanisa anapoadhimisha Siku ya Maskini Duniani. Huu ni mwaka wa nane tangu Papa Francisko  alipoanzisha siku hiyo mnamo 2017, kwa njia hiyo tukio hili halitakuwa tofauti na matukio mengine yaliyotangulia, kwa sababu zaidi ya watu 1,300 maskini wanatarajiwa kuungana na Papa katika kwa chakula cha mchana katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.  Chakula cha mchana, kitaaandaliwa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo ambacho kimetolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Italia na kuhuishwa na Kundi lake liitwalo Fanfare ya Kitaifa. Mwishoni mwa chakula hicho cha mchana, kila mtu atagawiwa mkoba utakaotolewa na Mapadre wa Vincent(Shirika la Kimisionari linalojikita sana na maskini, )mfuko utakao kuwa vyakula na bidhaa za usafi wa kibinafsi.

Papa Francisko mwaka 2023
Papa Francisko mwaka 2023

Siku hii kwa 2024 inaanguka katika Dominika ya Tatu ya Novemba tarehe 17, 2024 ambayo itaanza rasmi kwa maadhimisho ya Misa Takatifu, itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko, mwenyewe katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro. Hata hivyo, muda mfupi kabla ya maadhimisho ya Ekaristi, Papa atakuwa amebariki funguo 13, kila moja ikiwakilisha nchi kumi na tatu ambapo Shirika la Wavicenti watakuwa wakizindua mpango wao wa “Nyumba 13.” Mpango huo unajumuisha kujenga nyumba mpya kwa watu wasiojiweza katika nchi kumi na tatu tofauti. Huko, mipango mbalimbali ya hisani ikifanyika, kama vile kulipia bili za matumizi kwa familia za kipato cha chini kupitia miunganisho ya parokia. Moja ya nchi zinazokaribisha mpango huu mpya ni Siria, ambayo imesahauliwa na vyombo vingi vya habari vya magharibi huku ikiendelea kukumbwa na athari mbaya za takriban miongo miwili ya migogoro.

Wakati wa chakula cha mchana 2023
Wakati wa chakula cha mchana 2023

Katika ujumbe wake kwa Siku ya Maskini Duniani 2024, Papa Francisko alibainisha kuwa "siasa mbaya" zinazoendeshwa na vita huzalisha umaskini mpya na waathirika wasio na hatia. Aliwasihi kila mtu kusali pamoja na maskini, na akasisitiza kwamba watu wa kujitolea wanaendelea kujitolea kuwahudumia maskini zaidi katika miji yetu, wakijumuisha majibu ya Mungu kwa kilio cha wale wanaohitaji. Kwa njia hiyo Mwaka huu, hasa, kauli mbiu iliyochaguliwa na Papa imechukuliwa kutoka katika kitabu cha Sir: "Sala ya maskini huinuka kwa Mungu"( Sira 21: 5). Kauli mbiu hii inasisitiza kwamba maskini wana nafasi ya pekee katika moyo wa Mungu. Yaya anasikia maombi yao na anakuwa “hana subira” katika mateso yao hadi haki itendeke. Kitabu cha Sira kinathibitisha kwamba "hukumu ya Mungu itakuwa juu ya maskini" (Sira 21:5). Siku ya Maskini Duniani inahimiza Kanisa “kutoka nje” ya kuta zake na kujihusisha na umaskini wa aina nyingi katika ulimwengu wa sasa. Na katika  chakula hicho cha mchana, ndivyo Papa Francisko atakavyokuwa akifanya. Tiketi za kuudhiria misa takatifu  za bure tarehe 17 Novemba 2024 ambazo zitapatikana kuanzia tarehe 13 Novemba 2024 katika Kituo Rasmi cha Taarifa za Jubilei kupitia Via della Conciliazione, 7- yaani Njia ya Conciliano jengo la 7).

Siku ya Maskini duniani 17 Novemba 2024
12 November 2024, 16:54