Tafuta

2024.11.30 Ujume wa Kiekumene katika maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Andrea huko Instanbul Uturuki. 2024.11.30 Ujume wa Kiekumene katika maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Andrea huko Instanbul Uturuki. 

Ujumbe wa Papa katika Siku kuu ya Mtakatifu Andrea:Ushuhuda kati wa Waorthodox na Wakatoliki

Katika ujumbe wake uliosomwa na Kardinali Koch kwa Patriaki Bartholomew wa I katika siku kuu ya Mtakatifu Andrea,Papa ameeleza migawanyiko iliyopo leo hii kati ya madhehebu mawili na kuhimiza juhudi na maombi ili kukubali zawadi ya umoja na kupyaisha nia ya kusherehekea pamoja Jubilei ya miaka 1700 ya Mtaguso wa I wa kiekumene wa Nikea."Kusikilizana bila kulaani ndiyo njia ya umoja kati ya Wakatoliki na Waorthodox."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Uwakilishi kutoka  Vatican kwa ajili ya Siku kuu ya Mtakatifu Andrea Msimamizi wa Upatriaki wa Kiekumene huko Istanbul, ulifika huko tangu tarehe 28 Novemba hadi tarehe  1 Desemba  2024 ambapo katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko alituma Ujumbe uliosomwa mara baada ya Ibada takatifu ya Siku kuu hiyo tarehe 30 Novemba 2024. Katika Ujumbe wa Papa alioulekeza kwa Patriaki Bartholomew I, Askofu Mkuu wa Upatriaki wa Kiekumene wa Constantinopoli  papa anasema kwamba Maadhimisho ya kiliturujia ya Mtume Andrea, Msimamizi wa Upatriaki wa Kiekumene wa Konstantinopoli, yamempatia nafasi mwafaka, kwa niaba ya Kanisa Katoliki lote na kwa njia yake mwenyewe, kutoa salamu za dhati kwake yeye na  wote, kwa Washiriki wa Kanisa Katoliki.,Sinodi Takatifu, kwa wakleri, kwa watawa na waamini wote waliokusanyika katika Kanisa kuu la Upatriaki la Mtakatifu George huko Phanar.

Papa Francisko vile vile alituma uhakikisho wa maombi yake ya  dhati kwamba Mungu Baba, chanzo cha kila zawadi, atawapatia baraka nyingi za mbinguni kupitia maombezi ya Mtakatifu Andrea, wa kwanza kati ya wale walioitwa na ndugu wa Mtakatifu Petro. Papa alieelezea kuwa Ujumbe aliotuma kwa mara nyingine mwaka huu unaonesha upendo wa kidugu na heshima kubwa anayoendelea kuwa nayo kwa Utakatifu  wake na  kwa Kanisa  zima lililokabidhiwa kwa usimamizi wake wa kichungaji. Siku chache tu zilizopita, tarehe 21 Novemba 2024, ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka sitini ya kutangazwa Hati ya kitume ya  (Unitatis Redintegratio, yaani Marejesho ya Umoja ) ambayo iliashiria kuingia rasmi kwa Kanisa Katoliki katika harakati za kiekumene.  Hati hii muhimu ya Mtaguso mkuu wa II  wa Vatican ilifungua njia ya mazungumzo na Makanisa mengine. “Mazungumzo yetu na Kanisa la Kiorthodox yamekuwa na yanaendelea kuzaa matunda. La kwanza kati ya matunda yaliyopatikana kwa hakika ni udugu mpya ambao tunaupata leo kwa nguvu ya pekee, na kwa hili ninamshukuru Mungu Baba Mwenyezi.”

Hata hivyo, kile ambacho Unitatis Redintegratio- Marejesho ya Umoja, kama lengo kuu la mazungumzo, ushirika kamili kati ya Wakristo wote, kushiriki katika kikombe kimoja cha Ekaristi, bado hakijatimizwa na kaka na dada zetu waorthodox. Hili haishangazi, kwa kuwa migawanyiko iliyoanzia milenia moja, haiwezi kutatuliwa ndani ya miongo michache. Wakati huo huo, kama baadhi ya wataalimungu wanavyosisitiza, lengo la kuanzisha tena ushirika kamili lina mwelekeo usiopingika wa kieskatolojia, kwa vile njia ya umoja inapatana na ile ya wokovu ambao tayari umetolewa katika Yesu Kristo, ambamo Kanisa litashiriki kikamilifu tu wakati huo mwisho wa wakati. Hii haimaanishi kwamba tunapaswa kupoteza lengo kuu ambalo sisi sote tunalitamani, wala hatuwezi kupoteza tumaini kwamba umoja huu unaweza kupatikana katika historia na ndani ya wakati unaofaa. Wakatoliki na Waorthodox hawapaswi kamwe kuacha kusali na kufanya kazi pamoja ili kukubali zawadi ya kimungu ya umoja. Ahadi isiyoweza kutenguliwa ya Kanisa Katoliki katika njia ya majadiliano ilithibitishwa tena na Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu uliofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 2 hadi 27 Oktoba 2024.

Msukumo wa kuanzishwa upya kwa sinodi katika Kanisa Katoliki bila shaka utakuza mahusiano kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodox, ambalo daima limeweka hai mwelekeo huu wa kikanisa. Zaidi ya maamuzi madhubuti yatakayotokana na kazi ya Sinodi hali ya mazungumzo ya kweli na ya uwazi ilishuhudiwa wakati wa siku hizo. Katika dunia iliyokumbwa na upinzani na mifarakano, washiriki wa Sinodi hiyo, licha ya kuwa wanatoka katika hali tofauti, waliweza kusikilizana bila kuhukumu au kulaani. Kusikiliza bila kulaani kunapaswa pia kuwa namna ambayo Wakatoliki na Waorthodox wanaendelea na safari yao kuelekea umoja." Papa alifurahi sana kwamba wawakilishi kutoka Makanisa mengine, ikiwa ni pamoja na Metropolitan wa Pisidia, mjumbe wa Patriaki wa Kiekumene wa Constantinople, walishiriki kikamilifu katika mchakato wa sinodi. Uwepo wake na kazi yake ya bidii ilikuwa ikiboresha kwa wote na ishara inayoonekana ya umakini na msaada ambao umekuwa ukitoa kwa mchakato wa sinodi. Papa Francisko aidha amewaeleza kuwa “ukumbusho wa miaka 1700 unaokaribia wa Mtaguso wa Kwanza wa Kiekumene wa Nikea utakuwa fursa nyingine ya kutoa ushuhuda wa ushirika unaokua ambao tayari upo kati ya wote wanaobatizwa katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.

Papa amesisitiza kuwa  Tayari ameeleza mara kadhaa hamu yake ya kuweza kusherehekea tukio hili pamoja nao  na anawashukuru kwa dhati wale wote ambao tayari wameanza kufanya kazi ili kufanikisha hilo. Maadhimisho haya yatahusu sio tu Maoni ya kale ambayo yalishiriki kikamilifu katika Baraza, lakini Wakristo wote wanaoendelea kukiri imani yao katika maneno ya Imani ya Nikea-Constantinopoli. Ukumbusho wa tukio hilo muhimu hakika utaimarisha vifungo ambavyo tayari vipo na kuhimiza Makanisa yote kwa ushuhuda mpya katika ulimwengu wa leo. Udugu unaoishi na ushahidi unaotolewa na Wakristo pia utakuwa ujumbe kwa ulimwengu wetu unaokumbwa na vita na jeuri. Katika suala hili, kwa hiari yangu naungana na maombi yako kwamba kuwe na amani katika Ukraime, Palestina, Israeli na Lebanon, na katika maeneo yote ambayo vita vinaendelea na ambavyo mara nyingi ameviita "vita vya dunia vilivyogawanyika  vipande vipande." Kwa hisia hizi, Papa amepyaisha  matakwa yake  mema ya kutoka moyoni kwa kwake Patriaki na wote Anawakabidhi kwa maombezi ya Ndugu Watakatifu Petro na Andrea, na kubalishana nao mkumbati wa  kidugu katika Kristo Bwana wetu.

Ujumbe kutoka Vatican Kwenda Instanbul

Hata hivyo katika mfumo wa mabadilishano ya kiutamaduni ya Wajumbe kwa ajili ya sikukuu husika za Watakatifu wasimamizi  tarehe 29 Juni jijini  Roma kwa ajili ya maadhimisho ya Watakatifu Petro na Paulo na tarehe 30 Novemba huko Istanbul kwa ajili ya sherehe ya Mtakatifu Andrea, Kadinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa  Baraza la Kupapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, aliongoza Wajumbe wa Vatican kwa ajili ya sikukuu ya Upatriaki wa  Kiekumene. Kardinali alisindikizana na Wakuu wengine wa  Baraza Monsinyo Flavio Pace, Katibu, na Monsinyo Andrea Palmieri, Katibu Mkuu,  Balozi wa Vatican nchini Uturuki,  na Askofu Mkuu Marek Solczyński, aliungana nao huko Istanbul. Wajumbe wa Vatican walishiriki katika Ibada takatifu iliyoongozwa na Patriaki wa Kiekumene, Bartholomayo, katika Kanisa kuu la Mtakatifu  Giorgio al Phanar na kufanya mkutano na Patriaki na mazungumzo na Tume ya Sinodi inayosimamia uhusiano pamoja na Kanisa Katoliki. Kardinali Koch aliwasilisha ujumbe kwa maandishi kutoka kwa Baba Mtakatifu kwa Patriaki wa Kiekumene, ambao aliusomwa hadharani wakati wa kuhitimisha Liturujia takatifu ya Mungu.

Ujumbe wa Papa katika siku kuu ya Mtakatifu Andrea
30 November 2024, 12:28