Tafuta

2024.11.16 Kitabu cha  Papa Francisko: "wewe ni mkuu: 2024.11.16 Kitabu cha Papa Francisko: "wewe ni mkuu: 

"Wewe ni mkuu:”katika kitabu cha Papa juu ya mtazamo maalum wa Muumba wa viumbe wake

Katika kitabu kilichochapishwa na nyumba ya vitabu ya Vatican na Elledici chenye kichwa kidogo:"Uzuri wa kuwa maalum na kipekee",Papa Francisko kupitia muhtasari wa nyaraka,hotuba na ujumbe,anaelezea upendo wa Mungu kwa wanawake na wanaume,akiwaalika kutoa majibu.Monsinyo Dario Viganò alitia saini utangulizi kuwa:“sisi ni walezi wa upendo tuliopewa bila dhamana."

Vatican News

Katika kazi ya mikono ya Mungu, mwanadamu ndiye kitu cha thamani zaidi machoni pa Muumba wake. Anatujua mmoja baada ya mwingine, kwa jina letu na sura zetu, ambazo ni za kipekee. Baba hutuona kwa mfano wa Yesu, Mwana wake, na kwa upendo wake hutusaidia kufanana naye zaidi na zaidi.  Katika kitabu "Wewe ni Mkuu! Uzuri wa kuwa maalum na wa kipekee” kitabu kilichochapishwa na (Duka la vitabu la Vatican na Elledici). Baba Mtakatifu Francisko, mtaalamu wa kina wa nafsi ya mwanadamu, anatupatia kupitia maneno yake njia yenye uwezo wa kufuatilia utambulisho wa wanawake na wanaume wa wakati wetu. Matokeo yake ni picha ya kibinadamu inayotufanya sisi na wale wanaotuzunguka kusema, "Wewe ni mkuu!", Mkuu na wa kipekee kama vile Mungu mwenyewe alivyokufikiria. Safari, kupitia hotuba, nyaraka na ujumbe wa Papa, zinajitokeza katika sehemu mbili tofauti. “Wewe ni wa thamani” wa kwanza hufuatilia upendo wa Mungu kwa mwanadamu. Sehemu ya pili, "Ishi, Penda na Ota ndoto,” ambapo inakaribisha hatua mara tu tunapogundua upendo huu kwetu.

Katika utangulizi wa kitabu hicho , Monsinyo Dario Edoardo Viganò, makamu mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi, aliandika kwamba sisi ni “Wa kipekee na maalum si kwa sababu sisi ni mashujaa, bali ni kwa sababu sisi ni walinzi wa upendo ambao tumepewa bila kuomba dhamana au dhamana ya utendaji."  Kwa njia hiyo Sisi ni wa kipekee, kama anavyopendekezwa  “kwa sababu Mungu ameukabidhi moyo wake kwa kila mmoja wetu, kwa njia ya pekee, akiomba tutoe ushuhuda kwake katika barabara za maisha kwa kila mwanaume na kila mwanamke tunayekutana naye”. Na anaongeza: “Moyo, ule wa Baba, ambao hauogopi usaliti na dhambi, kushindwa na kukataliwa: ni upendo usio na kikomo, ambao haujui kutua kwa uchovu na nafasi za uthibitisho. Wewe ni wa thamani kwangu: ni maneno ambayo upendo wa Mungu hunong'ona kwa mioyo yetu kila wakati."

Monsinyo Viganò pia anaakisi  "umuhimu wa kutazama kabla ya uchambuzi juu ya"mahusiano katika muktadha wa dijitali. "Usiogope basi na ucheze maisha yako kwa uaminifu wa mtoto ambaye ana uhakika kwamba kila wakati baba na mama wanajua jinsi ya kukaribisha na kukausha machozi ya makosa katika kukumbatia wale wanaojua kupenda  na  ni faraja yake." Aidha  anabainisha kuwa "Sio juu ya kufikiria upeo wa utamu bila juhudi na dhambi: kila siku tunashiriki katika mapambano na kiburi kinachoishi ndani yetu, ambacho kinatuuliza tuhesabu, muda baada ya muda, katika mahusiano yetu." kwa njia hiyo " Tunaweza kupata msaada katika maombi ya Zaburi ambayo, katika uchovu wa maisha kuna manukato."

Kitabu cha Papa kuhusu "wewe ni mkuu"
19 November 2024, 11:11