Papa Francisko:Tusiisahau Ukraine; tusisahau Palestina, Israel, Myanmar na mataifa mengi kwenye vita. Papa Francisko:Tusiisahau Ukraine; tusisahau Palestina, Israel, Myanmar na mataifa mengi kwenye vita. 

Wito wa Papa tusisahau nchi zinazopigana!

Papa baada ya katekesi katika salamu zake ametoa wito “Na tusisahau nchi zilizopigana. Ndugu na dada, Ukraine inayoteswa inateseka! Tusiisahau Ukraine; tusisahau Palestina, Israel, Myanmar na mataifa mengi kwenye vita.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya katekesi yake Jumatato tarehe 13 Novemba 2024, Papa Francisko kwa akisalimia wanaozungumza lugha ya kiitalino alisema “Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Hasa, ninawasalimu Polisi wa Jimbo la Campobasso na Isernia, 50&PIÙ Chamacha Lombardia, Taasisi ya damu Azizi ya  Milano, Bendi ya Giuseppe Verdi ya Vallecorsa. Ilicheza vizuri, basi tutawasikiliza wakati mwingine ...”

Kikosi cha Polisi katika katekesi ya Papa
Kikosi cha Polisi katika katekesi ya Papa

Hatimaye, mawazo yake yaliwaendea vijana, wagonjwa, wazee, na wanandoa wapya: “Ninawahimiza kila mtu kupata nguvu na ujasiri katika Mungu kila siku ili kuishi wito wao wa kibinadamu na wa Kikristo kikamilifu.”

Papa na wanandoa wapya
Papa na wanandoa wapya

Wito kwa amani

Papa Francisko kwa maskitiko amesema “Na tusisahau nchi zilizopigana. Ndugu na dada, Ukraine inayoteswa inateseka! Tusiisahau Ukraine; tusisahau Palestina, Israel, Myanmar na mataifa mengi kwenye vita. Tusisahau kundi hilo la Wapalestina waliopigwa risasi na bunduki, wasio na hatia... Tuombe amani. Tunahitaji sana, tunahitaji sana amani!”

Wapoland


Papa alisema: “Ninawasalimu kwa moyo mkunjufu mahujaji wa Poland. Katika masuala yenu ya kibinafsi, ya kifamilia na kijamii, ombeni msaada wa Mama wa Mungu, Malkia wa Poland, ambaye amelilinda taifa lenu katika nyakati ngumu sana. Mmeadhimisha kumbukumbu ya kurudi tena kwa uhuru, ambayo watu wa Kipoland walipigana hata na rozari mikononi mwao. Heshumuno moya wa mama wa Maria kwa shukrani. Nawabariki wote.”


Kwa lugha ya kijerumani


“Ninatoa salamu kwa mahujaji wote, hasa kwa kikundi cha Caritas kutoka Jimbo kuu la Alba Iulia nchini Romania. Tujikabidhi kwa Bikira Maria, Binti wa Baba, Mama wa Mwana, Bibi-arusi wa Roho Mtakatifu atusaidie daima kubaki katika upendo wa Mungu wa Utatu anayetufanya kuwa ndugu na kutusukuma kuishi hivyo. Baba Mtakatifu: “Nawasalimu waamini wanaozungumza Kiarabu. Hebu tufanye upya "ndiyo" yetu kwa Bwana na mapenzi yake pamoja, tukimtumaini Yeye, kama Maria. Hivyo atatupatia maisha mapya na bora. Bwana awabariki nyote na kuwalinda daima na mabaya yote!

Baada ya Katekesi ya Papa Francisko
13 November 2024, 17:15