Hati ya mwisho ya Sinodi juu ya sinodi imechapishwa na LEV
Vatican News.
Nyumba ya Uchapishaji ya Vatican(LEV), imechapisha kitabu chenye kichwa: "Kwa ajili ya Kanisa la Kisinodi:ushirika, ushiriki na utume vyenye(kurasa 200, euro 7), ambacho kina hati ya mwisho ya Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu,iliyoidhinishwa na Papa Francisko tarehe 26 Oktoba 2024.
Chombo chenye mamlaka cha kuendelea kufanya kazi
Matokeo ya safari ya kusikiliza na utambuzi iliyoanza mnamo 2021, ambapo ni kifungu kinatoa miongozo kwa Kanisa la Kinodi, inayozingatia kauli mbiu yake ya “ushirika, ushiriki na utume. Viashiria vilivyomo vinanuia kuongoza Makanisa mahalia katika kutekeleza chaguo thabiti za kichungaji, kukuza umoja na heshima kwa tofauti za kiutamaduni. Chombo chenye mamlaka, Hati inawakilisha mwaliko wa kuzama zaidi katika mtindo wa sinodi kama kielelezo cha utume wa uinjilishaji wa Kanisa katika ulimwengu mambo leo.
Viashiria thabiti vya kuendelea na safari
Baada ya kunukuu shairi la Madeleine Delbrêl, "the mystic of the suburbs," ambalo linatuhimiza tusiwe wagumu, Papa Francisko alitangaza kwamba hakukusudia kuchapisha Waraka wa Kitume wa baada ya sinodi. "Katika Hati hiyo, kiukweli, tayari kuna viashiria halisi ambavyo vinaweza kuwa mwongozo wa utume wa Makanisa, na katika mabara tofauti, katika mazingira tofauti," Papa Francisko alisisitiza hayo katika hotuba yakemwishoni mwa Sinodi ya kisinodi. “Katika baadhi ya vipengele vya maisha ya Kanisa vilivyoripotiwa katika Hati, pamoja na mada zilizokabidhiwa kwa Vikundi kumi vya Mafunzo, ambavyo lazima vifanye kazi kwa uhuru, kunipa mapendekezo, muda unahitajika kufikia uchaguzi unaohusisha Kanisa zima,” aliongeza.