Papa kwa Chama cha Italia dhidi saratani ya damu na mifupa:‘kwa pamoja kutazama siku sijazo’
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 14 Desemba 2024 amekutana na wanachama wa chama cha Italia dhidi ya saratani ya leukemia,lymphoma na myeloma(Ail), katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican, akianza hotuba yake amekuwa na furaha ya kukutana nao wengi sana, katika hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya kuzaliwa kwa Chama chao. Amewashukuru kwa ziara yao na zaidi ya yote asante kwa kile wanachofanya. Mbali na utafiti wa ufadhili wa matibabu ya leukemia, lymphoma na myeloma, na ukuzaji wa vituo maalum katika eneo hilo, wanatoa ukarimu kwa wagonjwa na familia, utunzaji wa nyumbani na ukaribu na watu wengi walio na maelfu ya watu wanaojitolea. Ukaribu ni moja ya sifa za Mungu: ambayo ni ukaribu, huruma na upole. Na ameomba wafanye hivyo hivyo kuwa karibu na huruma nyingi na upole mwingi bila kusahahu hilo.
Ushuhuda wao ni wa mshikamano na ukaribu, muhimu zaidi katika ulimwengu ulio na ubinafsi, Papa amekazia kusema. "Wakati mmoja waliniuliza ni nini tabia ya chama fulani ambacho ni cha kibinafsi sana na nikasema: "Hapana, sijui sifa lakini ninajua kauli mbiu yake ni nini – wakauliza ni Ipi? Nami nilijibu ‘Umimi, pamoja nami na kwa ajili yangu mwenyewe.’ Katika kituo ni mimi, cha kujiweka katikati kwa ajili yangu. Huo ni ubinafsi mtupu," Papa alionya. Kufuatia na maonyo hayo kuhusu ubinafsi, Baba Mtakatifu Francisko alipenda kuwapa maneno matatu ambayo yanaweza kuwasaidia safari yao na kazi yao.
Ya kwanza aliitoa katika kauli mbiu waliyochagua kwa ajili ya mkutano huo: "Kwa pamoja tunaangazia siku zijazo." Na kwa nji hiyo neno ni" kuangaza." Kiukweli, ugonjwa huo mara nyingi huingiza mtu na familia yake katika giza la maumivu na uchungu, na kusababisha upweke na kufungwa. Katika ngazi ya kijamii, mara nyingi hutambuliwa kama kushindwa, kitu cha kuficha, na kuondoa na kwa hiyo, wagonjwa hutupwa kwa jina la ufanisi na nguvu, mateso yanatengwa kwa sababu yanatisha na kuzuia mipango. "Katika tamaduni zingine pia, wagonjwa wanaondolewa, na hii ni mbaya, ni mbaya sana. Badala yake, ni muhimu kumrudisha mgonjwa katikati, pamoja na historia yake, mahusiano ya kifamilia, wale wa kirafiki, wale wa matibabu hupata maana katika maumivu na kutoa majibu kwa kwa nini? Nyingi,” Papa amesisitiza. Hata wakati kila kitu kinaonekana kupotea, inawezekana kuwa na matumaini. Lakini tunahitaji mtu anayeleta nuru kidogo, mwali wa matumaini, mwenye urafiki, ukaribu na kusikiliza.
Papa akiendelea alisema neno la pili ni zawadi. Watu hawa wanaoleta nuru kidogo ndio “watoaji.”. Mantiki ya zawadi ndiyo dawa kuu ya utamaduni wa kutupa. Kila wakati tnapochangia, utamaduni wa kutupa tunadhoofika, au tuseme, tumeghairiwa; na utumiaji hovyo ambao kwa hakika tungependa kuchukua maisha yetu pia, na tunashindwa na mantiki hii adilifu. Aliyekuwa wa kwanza kujitoa ni Mungu mwenyewe, katika upendo wake wa uumbaji; ni Yesu, katika Umwilisho wake. Baada ya siku chache itakuwa Noeli, kwa hiyo basi tumtazame mtoto huyo aliyetolewa kwa ulimwengu ili sisi sote tupate kuokolewa. Tunapata nguvu kutokana na udhaifu wake, faraja kutokana na machozi yake, ujasiri kutokana na upole wake. Na mara nyingine tena neno tusisahau "huruma."
Neno la tatu ni uwanja. Chama chao kipo katika viwanja, na juhudi nyingi za usambazaji. Ni dhamira ya kutobaki kufungwa katika uwanja wa nyuma wa mtu mwenyewe ili kukuza masilahi ya mtu mwenyewe tu, badala yake kuhuisha eneo, kuwa ishara inayoonekana, na uwepo unaoonekana, lakini kamwe usifishwe bali uwe wazi wa kuingia. Katika uwanja shauku ya kukaa pamoja na watu, kushiriki maumivu, kuwa wasamaria wema inadhihirika. Hii ni zawadi wanayotoa kwa jamii yote. Wanaonekana lakini sio kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili ya watu wanaohitaji. Na kwa hivyo wanachangia kusaidia utafiti wa kisayansi, kuongeza maarifa ambayo ni sehemu ya utamaduni bora wa huduma ya afya ya Italia, na kuhakikisha umakini kwa watu ambao wanahitaji kuhisi kuwa wanasindikizwa katika matibabu.
Papa amesema kwamba wao ni kipande cha ujenzi wa matumaini mawili ambayo ni: matumaini ya tiba, daima,na katika mbinu za kisasa zaidi. Papa Francisko akikumbuka Siku ya Kiliturujia ya Mama Kanisa, kusherehekea Mtakatifu Yohane wa Msalaba, mcha Mungu mkuu, ambaye alikumbusha kuwa : "Jioni ya maisha tutachunguzwa juu ya upendo." Kwa hiyo Papa amewashukuru kwa upendo na matumaini wanayotoa! Wasonge mbele kwa kujitolea na umahiri. Amewabariki kwa moyo wote, wote waliokuwapo na wa wale wote wanaounda mtandao wa Chama chao. Na tafadhali wasisahau kumuombea!