Papa akutana na Waziri Mkuu wa Lebanon
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 13 Desemba 2024 alikutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Lebanon, Najib Mikati, katika Jumba la Kitume mjini Vatican pamoja na ujumbe wake, mkutano ulidumu kwa dakika 20. Mazungumzo ya faragha kati ya viongozi hao wawili yalifanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Jumba la Kitume kuanzia saa 3.35 hadi 3.55, ikifuatiwa na kubadilishana zawadi za kiutamaduni.
Mazungumzo kati ya vizazi
Katika zawadi hiyo, Papa alimpatia Waziri Mkuu mchongo wa shaba unaoitwa mazungumzo kati ya vizazi pamoja na nyaraka mbalimbali za Papa na Ujumbe wa Siku ya Amani Duniani kwa Kiarabu 2024, ambao alitia saini katika hafla hiyo. Waziri Mikati alijibu kwa zaidi inayoonesha Kuzaliwa kwa Yesu iliyoundwa na Padre kutoka Chuo Kikuu cha Antonine.