Papa amefika huko Ajaccio,Corsica kwa mara ya kwanza kisiwani Ufaransa
Vatican News
Kilomita 500 kuruka kwa kuvuka Bahari ya Mediterania hadi kutua mahali ambapo hakuna Papa aliyewahi kukanyaga kisiwani huko. Kwa hiyo ni sehemu ya historia inayoimarisha Ziara yake ya kitume iliyanza asubuhi ya Dominika tarehe 15 Desemba 2024 saa 2.06, wakati Baba Mtakatifu Francisko alipoondoka akiwa amechelewa kidogo ya ratiba kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Fiumicino wa Roma kuelekea Corsica, ambako alitua saa 2.49.
Mkutano juu ya udini maarufu
Ziara yenye jumla ya masaa tisa ambayo imempeleka Papa Francisko hadi Ajaccio, (Cité Impériale,) mji mkuu wa kisiwa hicho, mahali alipozaliwa Napoleon. Miongoni mwa ratiba yake hasa ni jambo kuu la kwenda kufunga Kongamano la "Udini Maarufu wa Watu wa Mungu katika Bahari ya Mediterania" ambalo litashuhudia uwepo wa maaskofu kutoka Italia, Ufaransa na Hispania na nchi zingine katika eneo hilo. Papa Francisko amerejea katika eneo la Ufaransa zaidi ya mwaka mmoja baada ya ziara yake ya Marseille kwa ajili ya kuhitimisha Mkutano mwingine wa "Rencontres Méditerranéennes" yaani Mkutano wa Mediteranea.
Salamu kwa kundi la watu wasio na makazi
Kama utamaduni wake uliojikita kwa miaka mingi, kabla ya kuingia kwenye gari kufika uwanja wa ndege, wa Fiumicino, Papa Francisko kwa mujibi wa taarifa ya Vyombo vya Habari vya Vatican alitaka kusalimiana na kikundi cha watu kumi wasio na makazi katika Nyumba ya Mtakatifu Marta wakisindikizwa na Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Upendo, ambapo kwa mujibu wa taarifa ni kwamba hawa ni "wanawake na wanaume ambao wanapata makazi usiku chini ya nguzo za Mtakatifu Petro.
Telegramu
"Safari hiyo kwangu mimi ni fursa ya kufanya upya mwaliko wa kuzingatia urithi wa kidini-kisanii-utamaduni wa ustaarabu wa wengi unaoelekeza Mare Nostrum, bahari yetu, ambayo licha ya matukio ya kihistoria, wamehifadhi kwa uangalifu urithi wa kiroho uliotolewa na baba zao katika pete ya harusi", na wakati huo huo fursa ya kugundua tena "maadili ya kiafya ambayo yameunda wanaume na wanawake, ili katika mazungumzo yenye matunda kati ya dini, taasisi za kisiasa na ulimwengu wa maarifa, kuheshimu mizizi ya watu, uhuru wa kushuhudia imani na wajibu wa siku zijazo."
Hayo ni mawazo ambayo Papa Francisko aliyoyaeleza katika telegramu iliyotumwa kwa Rais wa Italia Bwana Sergio Mattarella, ambaye kwa upande wake alisisitiza kwamba ushuhuda wa Papa Francisko "pamoja na maaskofu kutoka sehemu mbalimbali za Mediterania, uliokithiri kwa migogoro na majanga ya ajali za meli za wahamiaji, unahimiza kila mtu upya mitazamo ya maisha ya kidugu, kiasi na uwazi wa mazungumzo".
Fuatilia ziara hii fupi ya kitume katika kisiwa cha Ufaransa.