Tafuta

2024.12.05 Bi Natasa Pirc Musar, Rais wa jamhuri ya Slovenia 2024.12.05 Bi Natasa Pirc Musar, Rais wa jamhuri ya Slovenia  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amekutana na Rais wa Slovenia

Katika Jumba la Kitume Vatican,Papa Francisko amekutana na Bi Nataša Pirc Musar,Rasi wa Jamhuri ya Slovenia,asubuhi tarehe 5 Desemba 2024,kwa mazungumzo ya dakika 25 na Papa.Baadaye, kulikuwa na mkutano katika Sekretarieti ya Vatican,Kardinali Parolin na Monsinyo Wachowski, ambao ulizingatia uhusiano wa Kanisa na nchi ya Slovenia,hali ya Balkan Magharibi na migogoro ya Mashariki ya Kati na Ukraine.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko amekuwa na mazungumzo ya faragha Nataša Pirc Musar, Rais wa Jamhuri ya Slovenia, Alhamisi asubuhi tarehe 5 Desemba 2024, katika Jumba la Kitume mjini Vatican, yaliyodumu kwa dakika 25, kuanzia saa 2.05 hadi 2.30. Baadaye Mkuu wa Nchi hiyo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akifuatana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Mahusiano na Mataifa.

Papa alikurtana na Rais wa Slovenia
Papa alikurtana na Rais wa Slovenia

Kama taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican ilivyo taarifa inabainisha kuwa"wakati wa majadiliano ya dhati katika Sekretarieti ya Vatican uhusiano mzuri uliopo kati ya Vatican na Jamhuri ya Slovenia ulioneshwa na baadhi ya masuala ya wazi katika mahusiano ya Vatican na nchi hiyo huki wakiakisi mchango wa Kanisa Katoliki kwa jamii ya Kislovenia." Kwa mujibu wa maelezo aidha: "Kisha kuliakisiwa masuala mbalimbali ya asili ya kimataifa, kwa kuzingatia hasa eneo la Balkan Magharibi na migogoro ya Mashariki ya Kati na Ukraine.”

Rais wa Slovenia na Sekretarieti ya Vatican
Rais wa Slovenia na Sekretarieti ya Vatican

Wakati wa kubadilishana zawadi za kitamaduni, Papa alimkabidhi Pirc Musar hati za Kipapa, ujumbe wa mwaka huu kwa ajili ya Amani, kitabu kilichochapishwa na LEV cha Njia ya Mslaba (Statio Orbis) ya tarehe 27 Machi 2020. Rais alijibu kwa kitu cha kisanii cha Mbao ambacho ni kazi inayoonesha moyo na keki za Kislovenia.

05 December 2024, 17:08