Tafuta

Papa anakutana na Macron:'Asante kwa ishara ya kuja hapa'

Kitendo cha mwisho cha ziara ya Kitume ya 47 huko Corsica kilikuwa ni mazungumzo ya faragha katika chumba cha faragha kwenye Uwanja wa Ndege wa Ajaccio kati ya Papa na rais wa Ufaransa.Baada ya kubadilishana zawadi na utani,Papa Francisko alimwalika mkuu wa nchi ya Ufaransa kusoma kifungu kutoka katika Evangelii Gaudium kinachokumbusha mafundisho ya Mtakatifu Thomas More kuhusu 'kutopoteza ucheshi mzuri.'

Salvatore Cernuzio – Vatican

“Ninakushukuru kwa ishara hii ya kuja hapa. Ishara hii inaonesha utu wako, ukitafuta mkutano. Asante sana kwa muda wako." Papa Francisko alikaribishwa na Rais wa Ufaransa Bwana Emmanuel Macron kwa maneno ya shukrani, aliyefika Ajaccio kumuaga muda mfupi kabla ya kuondoka Corsica, kuja Roma ikiwa ni katika Ziara yake ya kitume ya 47, ambapo amefika huko katika fursa ya Kongamano kuhusu "Udini Maarufu wa watu wa Mungu katika Mediteranea."

Papa na Macron
Papa na Macron

Kitabu kuhusu Notre-Dame kama zawadi

Katika chumba kidogo kwenye Uwanja wa ndege uliopewa jina la Napoleon, aliyezaliwa katika kisiwa hicho, chumba kilichowekwa kiti cha mkono chenye koti la Papa na bendera za Jiji la Vatican, Ufaransa na Ulaya, Papa na rais waliingia pamoja kupitia lango moja kabla ya saa kumi na mbili jioni na wajumbe wao husika. Rais Macron, kama ilivyokuwa zamani katika vikao vya Vatican, au katika mikutano ya Marseille mnamo 2023 au G7, aliweka ishara za upendo kwa Papa. Mara moja alimkabidhi zawadi yake ambayo ni kitabu kikubwa kilichotolewa kwa Kanisa Kuu la Notre-Dame, (Mama Yetu la Paris) lililokarabatiwa  baada ya kuungua moto mkali  mnamo 2019 na kufunguliwa tena kwa umma Juma  moja lililopita, tarehe 7 Desemba 2024. Mkuu wa nchi alipitia baadhi ya kurasa za kitabu hicho.

Macron na Papa Francisko
Macron na Papa Francisko

Usipoteze hali yako nzuri

Papa alijibu zawadi hiyo kwa medali za upapa na hati za majisterio. Hasa, Papa Fransisko alichukua nakala ya Evangelii Gaudium kutafuta ukurasa unaotaja pendekezo la Mtakatifu Thomas More - ambalo alirudia mara kwa mara katika hotuba zake – la kutopoteza ucheshi mzuri. Papa alielekeza jambo hilo kwa Macron kumtaka asome, rais akajibu kwa tabasamu na kumpa mkono Papa.

Macron amemuaga Papa
Macron amemuaga Papa

Asante kwa ziara yako

Wakiwa wameketi kwenye viti, wawili hao walipeana mikono na kiongozi wa Ufaransa akamshukuru Papa kwa ziara yake, huku akisisitiza kwamba ameona furaha ya watu wa Corsica, "amejivunia sana" kwa kuweza kumkaribisha Papa. Rais Macron alimshukuru Jorge Mario Bergoglio "kwa niaba ya Corsica na Ufaransa"; pamoja na hayo, mateso kutokana na kimbunga katika visiwa vya Ufaransa vya Mayotte vilivyosababisha mamia ya wahanga, kukumbukwa leo hii  na Papa katika sala ya Malaika wa Bwana. Kutoka hapo, mazungumzo nyuma ya milango iliyofungwa, kitendo cha mwisho kabla ya sherehe ya kuaga katika uwanja wa ndege mwishoni mwa safari ya haraka ambayo iliashiria sura mpya katika historia kwa kisiwa cha Mediterania.

Kubadilishana zawadi
Kubadilishana zawadi
PAPA NA MACRON
15 December 2024, 19:07